Imam Ahmad bin Muhammad bin Hambal

Imam Ahmad bin Muhammad bin Hambal

Imam Ahmad bin Muhammad bin Hambal


Imam Abu Abdallah Ahmad bin Muhammad bin Hambal alizaliwa huko Marwa mwezi 20 Rabi-al-Awwal 164 A.H. Baba yake Muhammad alikuwa mujahid aliyesifika wakati akiishi Basra, Iraq. Baba yake alihamia Baghdad ambapo alifariki muda mfupi baadae na kumuacha Ahmad bin Muhammad akiwa bado mchanga. Pamoja na uyatima wake, kijana Ahmad alikuwa mwenye akili na akautumia ujana wake wote katika kujielimisha. Alisoma zaidi Hadith na akawa mwanasheria na mtaalam wa fiqh katika zama zake. Kwa hiyo Imam Shafii na Imam Ahmad Hambal walikuwa karibu sana. Imam Hambal alimheshimu mwalimu wake Shafii, na Imam Shafii alimheshimu mwanafunzi wake mashuhuri Hambal.


Imam Ahmad Hambal alikuwa mwanachuoni Mcha Mungu sana aliyejitoa maisha yake yote kusoma na kufundisha Hadith na Fiqh. Kwa ucha Mungu wake alikataa kufanya kazi Serikalini, kwani aliona Serikali ilikuwa haiongozwi kwa mujibu wa Qur'an na Sunnah. Zaidi ya hivyo alivunja uhusiano wa karibu na wote wale waliokubali kuwa ndani ya Serikali ya kidhalimu. Alikataa hata kupokea fedha au chakula kutoka kwa mtoto wake ambaye alikuwa akifanya kazi katika Serikali ile ya kidhalimu. Hata wakati alipokabiliwa na hali ngumu ya uchumi hakukubali kupokea msaada wowote ila kwa kuufanyia kazi.


Katika kipindi cha uhai wa Imam Ahmad waliibuka wanafalsafa waliokuja na falsafa iliyoitwa Mu'tazili. Falsafa hii iliwaita watu wawe huria katika fikra. Walichanganya imani na kufr hata kufikia kuleta hoja kuwa Qur'an imetengenezwa tu. Harakati hizi za kuleta kufr ndani ya Uislamu zilitokana na athari ya falsafa za Wagiriki zilizowalevya baadhi ya Waislamu wa zama hizo.


Bahati mbaya watawala wa zama hizo nao waliathiriwa na falsafa hizo za Kigiriki na wakataka kuifanya kuwa imani rasmi ya dola ya Kiislamu. Viongozi waliotaka kuisimika imani hiyo ni Khalifa Ma'mun al-Rashid; Mu'taslim Billah na Al-Wathiq. Imam Ahmad bin


Hambal alikataa kuikubali imani hiyo mpya ya watawala na akaendesha harakati kuipinga. Mtawala Mu'taslim alitoa amri akamatwe afungwe minyororo na kuhamishiwa Tarsus toka Baghdad. Huko alitupwa gerezani na kuteswa sana mpaka viungo vyake vingi vikavunjika. Imam Ahmad aliachwa adumu amefungwa minyororo mizito ndani ya chumba chenye giza gerezani. Pamoja na kuteswa sana ikiwa ni pamoja na kuchapwa mpaka kutoka damu, Imam Ahmad hakutetereka katika msimamo wake. Msimamo huu wa Imam Ahmad ulimstua Khalifa Mu'taslim. Aliikumbuka Akhera akahofia khatima yake. Aliamuru Imam Ahmad atolewe gerezani mwezi 25 Ramadhan mwaka 221 A.H na akamuomba msamaha, Imam Ahmad akamsamehe.


Miongoni mwa kazi muhimu alizofanya Imam Ahmad ni kuandika vitabu vifuatavyo: Kitab al-Amal al-Tafsir; Kitab al- Nasikh wal-Mansukh na kadhalika. Lakini kazi muhimu zaidi aliyoiacha Imam Ahmad ni ukusanyaji wa Hadith elfu nyingi na kuandika kitabu cha Hadith cha Musnad ya Ibn Hambali. Ulipofika mwaka wa 241 A.H Imam Ahmad alifariki dunia. Maelfu ya watu wa Baghdad walifurika kumzika.





                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 215


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Makatazo ya kujiepusha nayo
Soma Zaidi...

Haki na wajibu wa mtoto kwa wazazi na katika jamii
Soma Zaidi...

Imam Abu Hanifa: Nuuman Ibn Thabit
Soma Zaidi...

Msisitizo juu ya kutoa zaka na sadaka
Soma Zaidi...

fadhila za kusoma quran
Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

Kwa nini imefaradhishwa kufunga katika Mwezi wa ramadhani?
Soma Zaidi...

Tofauti kat ya sura za Maka na Madina
Sura za Makka na Madina Kutokana na historia ya kushuka kwake sura za Qur-an zimegawanywa katika makundi mawili - sura za Makka na sura za Madina. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME AL-YASA'A(A.S)
Mtume Alyasa'a(a. Soma Zaidi...

DUA ZA SWALA
DUA ZA SWALA 1. Soma Zaidi...

HADITHI 40 ZA IMAM NAWAW AROBAIN AN-NAWAWIY
Soma Zaidi...

HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)
HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara. Soma Zaidi...

Umuhimu, Ubora na Fadhila za kufunga
Soma Zaidi...