Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Hitimisho
Maimamu wote wanne walikuwa wanachuoni wacha Mungu na waadilifu katika zama zao. Walifanya juhudi kubwa kusoma na kufanya ijtihada ya kutafsiri na kutoa maoni yao juu ya sheria na masuala mbalimbali ya Fiqh. Ni vizuri tunufaike na matunda ya juhudi zao, lakini tusigawike wala kubaguana kutokana na maoni tofauti ya Maimamu hao juu ya masuala mbalimbali. Wao wenyewe walisoma pamoja au kusomesha na wakaheshimiana na wakaafikiana kutofautiana katika mambo ya msingi bila ya kugombana.
Jambo jingine la msingi la kuzingatia ni kuwa Maimamu hawa walipata mateso makubwa kutokana na misimamo na juhudi zao katika kuuhuisha na kuusimamisha Uislamu katika
jamii. Walichapwa viboko, walifungwa gerezani na kufungwa minyororo na watawala madhalimu. Zaidi ya hivyo hawakukubali kununuliwa na Serikali. Walikataa kabisa kuwa vibaraka wa Serikali. Je, wakati tunafuata Fiqh na Fatβwa zao tunao pia uadilifu kama wao? Misimamo yetu juu ya Serikali za kidhalimu ni kama wao? Je, hatununuliwi na Serikali na kuifanyia kazi kinyume na maslahi ya Uislamu? Je, tupo tayari kufungwa na kuchapwa viboko kwa ajili ya kusimamisha haki kama Imam Abu Hanifa, Malik, Shafii na Hambal?
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π2 ai web app π3 Kitabu cha Afya π4 Dua za Mitume na Manabii π5 web hosting π6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
HISTORIA YA BANI ISRAIL
Nabii Musa na Harun walikuwa na kazi kubwa mbili; kwanza, kuwakomboa Bani Israil kutokana na dhuluma waliyokuwa wakifanyiwa na Firaun na Serikali yake, na pili, kuwarudisha kwenye nchi yao takatifu ya Palestina.
Soma Zaidi...MAMA YAKE MTUME MUHAMMAD (S.A.W) ANAMLEA MTUME MUHAMAD AKIWA NA UMRI WA MIAKA MINNE (4)
KULELEWA NA MAMA YAKE ALIPOFIKA MIAKA MINNEMtume (s.
Soma Zaidi...Msonge wa uongozi na siasa katika serikali ya kiislamu mafinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hija ya kuaga kwa mtume, na hutuba ya mwisho aliyotowa mtume katika hija
Mwaka mmoja baada ya msafara wa Tabuuk Bara Arab zima ilikuwa chini ya Dola ya Kiislamu.
Soma Zaidi...tarekh 09
KULELEWA NA BABU YAKE:Mzee βAbdul Al-Muttalib alimchukuwa mjukuu wake na wakarejea Makkah na aliendelea kuishinae na kumlea kwa mapenzi makubwa sana.
Soma Zaidi...Shukurani za Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Allah(s.w)
Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Is- haqa(a.
Soma Zaidi...