VITU VINAVYOCHOCHEA KUWEPO KWA UGONJWA WA UKIMWI.


image


Posti hii inahusu zaidi vitu ambavyo vinasababisha kuongezeka kwa Ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na baada ya watu kujua Ugonjwa huu na matokeo ila bado ugonjwa unazidi kuongezeka.


Mambo yanayosababisha kuongezeka kwa Ugonjwa wa Ukimwi.

1. Kwanza kabisa kitu kikubwa ni watu kutokuwa wazi kuhusu maisha yao.

Kwa sababu watu wengi wanakuwa ni waathirika na wana wapenzi wengi wanaendelea kujamiiana na watu wengine ambao hawana Ugonjwa hali ambayo inafanya kuendelea kuwepo kwa Ugonjwa huu na kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa hiyo uaminifu na uwazi ni lazima.

 

2.Watu wengine kutojali afya zao 

Hali hii inatokea pale ambapo mtu anakuwa anasafiri akifika kituoni yuko radhi kulala na kahaba anayeuza mwili wake bila kutumia kinga ili mradi atulize hamu yake, kwa hiyo hali ya namna hiyo usababisha kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi kila siku na kuwepo kwa Maambukizi mapya.

 

3. Mila na desturi za jamii.

Kuna baadhi ya mila na desturi ambazo Usababisha kuenea kwa Maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi, mila hizo ni pamoja na kuridhishwa mke au mme wa marehemu aliyefariki kwa Ugonjwa wa Ukimwi na pia yule aliyeridhishwa utakuta naye ana wapenzi wengine na wapenzi wana wapenzi wengine hali ambayo Usababisha kusambaa kwa ugonjwa wa ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

 

4.umaskini katika jamii.

Umaskini pia nao unasababisha kuwepo kwa ongezeko la Ugonjwa wa Ukimwi kwa sababu unaweza kukuta familia moja wanatumia wembe mmoja, pini na vitu vyote vya ncha kali vinatumiwa na pia kama kuna mgonjwa ambaye yuko katika hatua ya nne ya Maambukizi wanahudumia kwa kutumia mikono bila kujikinga.

 

5. Pia kwa upande wa umaskini unakuta tajiri analala na watoto wa shule na wengine ambao hawasomi kwa lengo la kuwapatia hela kidogo ya kununua matumizi yao ya kawaida na watoto wanakuwa tayari kufanya hivyo ili wapate mahitaji yao yanayokosa kwenye familia zao



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Vyakula vya madini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya madini mwilini Soma Zaidi...

image Dalili za mawe kwenye kibofu Cha mkono
Mawe ya kibofu ni mkusanyiko mgumu wa madini kwenye kibofu chako. Mawe kwenye kibofu hukua wakati mkojo kwenye kibofu chako unapokolea, na kusababisha madini katika mkojo wako kung'aa. Soma Zaidi...

image Mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe
Post hii inahusu zaidi mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe, ni kipindi ambacho ni kutoka utotoni kwendea ujana. Soma Zaidi...

image Dawa za maumivu ya jino
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za maumivu ya jino Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa coma
Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la Kichwa, Kiharusi, Uvimbe kwenye ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi, Soma Zaidi...

image Utaratibu wa lishe kwa wazee
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu utaratibu wa lishe kwa wazee Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ambao kwa kitaalamu huitwa Dementia ugonjwa huu uwapata wale ambao umri umekwenda lakini kwa wakati mwingine Usababishwa na vitu mbalimbali kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

image Dalili za mimba ya siku 4
Unaweza kutaka kujuwa je naweza kupata dalili za mimba baada ya siku nne toka ujauzito kutungwa? ama baada ya siku nne toka kushiriki tendo la ndoa. Makala hii itakwenda kujibu maswali haya na mengineyo. Soma Zaidi...

image Vipimo vya minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vipimo vya minyoo Soma Zaidi...

image Maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada Soma Zaidi...