image

Vyakula hatari kwa mjamzito hasa mimba changa

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya hatari kwa mjamzito hasa mimba changa

VYAKULA HATARI KWA MJAMZITO HASA KWA MIMBA CHANGA

1.Mayai mabichi: Mayai ni chakula kizuri kila mtu anatambuwa hili. Hata hivyo si jambo jema kula mayai mabichi. Hii inaweza kuwa hatari kwa ujauzito hasa kwa mwenye ujauzito mchanga. Hivyo epuka kula mayai mabichi ama yasiyowiva vyema.

 

2.Maini ya wanyama kwa wingi: Maini ni katika vyakula ambavyo vina virutubisho vingi sana. Kama ijulikanavyo ini lina kazi nyingi mojawapo ni kuondoa sumu mwilini. Hivyo unahitajika kutokula maini kwa mjamzito.

 

3.Shubiri: shubiri hufahamika kwa uchungu wake. kwa mwenye ujauzito hasa mimba changa shubiri sio salama. Shubirilinaweza kutoa ujauzito kama litatumika kwa kulinywa. Onyo hili linaandamana na miti mingine michungu.

 

4.Viazi mbatata vilivyoanza kuota: onyo hili ni kwa nafaka zote zinazoanza kuota sio nzuri kula. Hasa hasa viazi mbatata ambavyo vimeanza kutoa miche sio salama kwa mwanamke mjamzito kutuia kama chakula.

 

5.Mapapai hasahasa mapapai yasiyowiva: Matunda nimuhmu sana kwa mjamzito kwa afya yake na ya mtoto wake. Hata hivyo kuna matunda sio mazuri kuyala kwa wingi kwa mwenye mimba changa. Mapapai ni mojawapo, hasa papai ambalo halikuwiva, yaani lile la kijani lililokomaa.

 

6.Mananasi: nanasi ni kama papai, kama mjamzito atatumia kwa wingi, inaweza kuwa hatari kwa mimba iliyochanga.

 

7.Vyakula ambavyo havijawiva vyema hususani samaki na nyama: sio samaki tu na nyama, chakula chochote ambacho hakikuwiva vyema ni hatari sana kwa mwenye uauzito. Hii ni sawa na nyama ya kuku na vyakula vingine.

 

8.Kutumia majani ya chai yenye caffein kwa wingi. Mjamzito hakatazwi kunywa chai ya majani ya chai. Kilichokibaya ni kuzidisha unywaji wa chai yenye majani ya chai kupitiliza. Majani ya chai yana kemikali inayoitwa caffein, hii ikiwa nyingi inakuwa hatari kwa ujauzito.

 

9.Chumvi kwa wingi10.Energy drink





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 6619


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula Fenesi
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula pera
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula pera Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
2. Soma Zaidi...

Hasara za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi hasara za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito. Soma Zaidi...

Vyakula vya kuongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha
Post hii itakwenda kukufundisha vyakula ambavyo ni vizuri kwa mwanamke anayenyonyesha ili kumsaidia kupata maziwa kwa wingi. Soma Zaidi...

FAIDA ZA MAJI MWILINI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Faida za kula tango
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula tango Soma Zaidi...

Faida za kafya za kula asali
Post hii itakwenda kukufundisha faida za kiafya za kula asali Soma Zaidi...

Vyakula vya fati
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za vyakula vya fati na umuhimu wake mwilini Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamin K
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin K Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Kunazi
Soma Zaidi...