image

Vyakula kwa wagonjwa wa sukari na utaratibu wao wa lishe

Post hii inakwenda kukufundisha utaratibu wa lishe kwa wagonjwa wenye kisukari pamoja na vyakula salamakwao.

Matibabu ya ugonjwa wa kisukari yanagharimu fedha nyingi. Kwa hiyo ni muhimu kuzuia na kudhibiti athari za kisukari mapema. Ili kudhibiti ugonjwa wa kisukari mgonjwa anapaswa kupatiwa matibabu sahihi, kufuatilia na kupima hali yake ya afya mara kwa mara pamoja na kuzingatia mtindo bora wa maisha na taratibu zinazofaa za ulaji wa chakula.

 

Zifuatazo ni kanuni za ulaji unaofaa zinazopaswa kuzingatiwa na mgonjwa wa kisukari:

1.Kula mlo kamili (angalau mara 3 kwa siku) kwa kuzingatia muda mahususi aliojipangia kwani hashauriwi kukaa na njaa kwa muda mrefu.

 

2.Dhibiti kiasi cha nishati – lishe (wanga) katika chakula ili kisizidi mahitaji ya mwili. Kiasi kitegemee mahitaji ya mtu binafsi.

 

3.Ongeza ulaji wa vyakula vyenye makapi – mlo kwa wingi. Kiasi kikubwa cha nishati-lishe kitokane na vyakula vya asili ya nafaka isiyokobolewa, mizizi na ndizi za kupika. Sukari inayotoka katika vyakula hivi hufyonzwa kwa taratibu na hivyo kupunguza kasi ya ongezeko la sukari katika damu.

 

4.Punguza kiasi cha vyakula vinavyozalisha nishati lishe kwa wingi hususani vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

 

5.Panga utaratibu wa kula chakula na matumizi ya dawa. Iwapo unatumia insulin au dawa za kushusha kiwango cha sukari katika damu unapaswa kujipangia muda wa kula chakula na kumeza dawa ili kuzuia kupungua kwa sukari katika damu. Epuka kukaa kwa muda mrefu bila kula chakula.

 

6.Kula mbogamboga kwa wingi katika kila mlo.

7.Kula tunda katika kila mlo.

8.Epuka kunywa pombe.

9.Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi kama soda, keki, biskuti, pipi na asali.

 

Kanuni nyingine za kuzingatia ni:

1.Punguza uzito iwapo una uzito uliozidi - au dhibiti uzito wa mwili ili usifikie uzito uliozidi. Ni muhimu kuwa na uwiano sahihi wa uzito wa mwili kulingana na urefu wako.

 

2.Zingatia usafi na usalama wa chakula





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 894


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula panzi, senene na kumbikumbi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula senene, panzi na kumbikumbi Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula korosho
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula korosho Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Miwa
Soma Zaidi...

magonjwa na lishe
DARASA LA AFYA MAGOJWA YANAYOHUSIANA NA VYAKULA 1. Soma Zaidi...

Faida za kula apple (tufaha)
Posti hii itakwende kukueleza kuhusu faida za kula apple na umuhimu wake kiafya Soma Zaidi...

Vitamini na kazi zake
Posti hii inahusu zaidi vitamini mbalimbali na kazi zake kwenye mwili,vitamini ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Faida za kula viazi mbatata
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula viazi mbatata Soma Zaidi...

Faida za kungumanga/nutmeg
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kungumanga Soma Zaidi...

Zijuwe faida za kula njegere
zijuwe faida za kula njegere kiafya na umuhimu wa kula jegere pia jifunze njegere zina kazi gani mwilini? Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula ubuyu
Soma Zaidi...

Faida za kula stafeli/soursop
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za stafel/soursop Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Bamia
Soma Zaidi...