Vyakula vya kuongeza damu

Vyakula vya kuongeza damu

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuongeza damu

VYAKULA VYA KUONGEZA DAMU

 

Damu ni tishu iliyo katika kimiminika. Katika miili yetu damu ina kazi ya kusafirisha viinilishe na hewa ya oksijeni na kuondoa hewa chafu ya kabonidaiyoksaidi mwilini. Pia urekebishwaji wa joto na usafirishwaji wa homoni ndani ya mwili hutegemea damu. Kwa ufupi damu in akazi nyingi. Upungufu wowote wa damu mwilini unaweza kuleta athari nyingi mbaya za kiafya mwilini. Makala hii inakwenda kukueleza njia ya kuongeza damu kwa haraka.

 

Kazi za damu mwilini1.Kusafirisha viinilishe kutoka katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.2.Kusafirisha hewa ya oksijeni kutokakwenye mapafu kwenda maeneo mengine ya mwli.3.Kusafirisha hewa ya kabonikaiyoksaidi kutoka kwenye seli na kpeleka kwenye mapafu kwa ajili ya kutolewa nje4.Kudhibiti joto la mwili kwa kulipooza inapohitajika na kuliongeza inapohitajika5.Kusafirisha homoni kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.

 

Vyakula vya kuongeza damu mwilini1.Nyama nyekundu kama nyama ya ng’ombe, mbuzi. Kondoo2.Maini3.Nyama ya figo4.Mboga za rangi ya kijani kama mchicha na apinachi5.Maharagwe6.Kunde7.Mayai8.Nafaka nyinginezo9.Njegere10.Koeosho na karanga11.Samaki12.Nyama ya ndege13.Karoti14.Matikiti15.Zabibu16.Viazi vitamu17.Matunda yenye uchachu kama machungwa, ndimu na limao.18.Polipili nyekundu

 

Dalili za kupungua kwa damu mwilini1.Uchovu wa hali ya juu2.Udhaifu wa mwili3.Ngozi kuwa na rangi ya njano au mauko4.Kupumua kwa shida5.Mapigo ya moyo kutokuwa ya kawaida6.Kizunguzungu na kichwa kuhisi chepesi7.Maumivu ya kifua8.Miguu na mikono kuwa ya ubaridi9.Maumivu ya kichwa

 

Sababu za upungufu wa damu mwilini1.Upungufu wa madini ya chuma mwilini2.Upungufu wa vitamini A na B-12 mwilini3.Maradhi kama HIV, UKIMWI, saratani, mardhi ya figo haya huweza kuleta upungufu wa damu4.Mfumo wa kinga mwilini kuuwa na kuharibu seli hai nyekundu (autoimmune)5.Uharibifu wa seli hai nyekundu kufanyika kwa haraka kuliko utengenezwaji.6.Kuwa na maradhi ya sickle cell

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views: 2975

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Bongolite - Game zone - Play free game     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 web hosting     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

Faida za vitamin C mwilini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vitamini C mwilini

Soma Zaidi...
Vinywaji salama kwa mwenye kisukari

Vijuwe vinywaji salama kwa mgonjwa wa kisukari

Soma Zaidi...
Kupunguza tumbo na nyama za pembeni: Siri zake.

Watu wengi hutumia muda mwingi kufanya mazoezi ya tumbo (sit-ups) wakiamini kuwa ndiyo njia pekee ya kupunguza tumbo. Hii ni siri kuu ya kwanza: Huwezi kuchagua sehemu moja ya mwili ya kupunguza mafuta (spot reduction). Ili kupunguza tumbo na nyama za pembeni, lazima upunguze mafuta mwilini kwa ujumla. Makala haya yanakupa siri za kweli za kufikia lengo hilo kwa ufanisi.

Soma Zaidi...
Faida za apple kwa Mama mjamzito

Posti hii inahusu zaidi faida za apple kwa mama mjamzito, ni faida anazozipata mama akiwa mjamzito kwa sababu ya kuwepo kwa vitamini mbalimbali kwenye apple ambavyo usaidia katika makuzi ya mtoto.I

Soma Zaidi...
Faida za kula nanasi

Somo hili linakwenda kukuletea za kula nanasi na umuhimu wake kiafya

Soma Zaidi...