image

Vyakula vya vitamini na faida zake

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamini na faida zake

VYAKULA VYA VITAMINI NA FAIDA ZAKEVitamin ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mwili unatumia virutubisho vingine kufanya kazi zake. Kuna vitamin A,B,C,D,E na K. vitamin B vimegawanyika katika makundi kama vitamin B1,B2,B6, na B12. Ukosefu wa vitamin vyovyote kati ya hivi unaweza ukapelekea matatizo makubwa kwa afya ya mtu.Vitamin A,D,E na K, vinaitwa fat soluble vitamin. Hivi nhuweza kuhifadhiwa ndani ya mwili. Hivyo hatuhitaji kula vyakula kuvipata kwa kila siku. Kwa upande mwengingine vitamin B na C huitwa water soluble vitamin, hivi havihifadhiwi ndani ya mwili, hivyo tunahitaji kula vyakula vyenye vitamin hivi kwa kila siku.Vitamin A hupatikana kwenye maziwa, maini, karoti,machungwa, na mboga za rangi nya njano.. vitamin hivi ni muhimu kwa kusaidia afya ya macho na mfumo wa upumuaji (respiratory track). Ukosefu wa vitamin hivi unapelekea mtu kushindwa kuona wakati wa usiku. Mwili unakuwa ni rahisi kupata mashambulio pindi mtu akiwa na vitamin A kwa uchache.Vitamin B1 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, mayai,hamira na mchele. Husaidia katika kuhakikisha michakato ya kikemikali ndani ya seli inafanyika vizuri (metabolism). Pia husaidia katika kuunganisha taarifa za misuli. Ukosefu wa vitamin hivi unapelekea ugonjwa wa beriberi ambopo mtu anakosa hamu ya kula. Misuli kukaza pia ni dalili ya upungufu wa vitamin hivi. Wakati mwingine moyo kushindwa kufanya kazi ni kutokana na upungufu wa vitamin hivi.Vitamin B2 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, nafaka na hamira. Husaidia katika ufanyikaji wa michakato ya kikemia ndani ya seli (metabolism). Kupasuka kwa midomo ni dalili ya ukosefu wa vitamin hiviVitamin B3 hupatikana kwenye samaki, karanga,nyama, mchele usio kobolewa na hamira.. huhitajika kwa ajili ya kuwasaidia enzymes kubadilimchakula kuwa energy. Pellagra ni ugonjwa unaotokana na upungufu wa vitamin hivi. Mgonjwa anakosa hamu ya kula, misuli kukosa nguvu na kuharibika kwa ngozi.Vitamin B12 hivi hupatikana kwenye samaki,nyama, mayai,maziwa na maini. Husaidia katika utengezaji wa damu, na utengezaji wa genetic meterials. Ugonjwa wa anaemia, upungufu wa uzito na nerve damage hutokana na upungufu wa vitamin hivi.Vitamin C hivi hupatikana kwenye matunda yenye uchachu kama limao na machungwa. Mboga za kijani,na nyanya. Husaidia mwili kufyonza madini ya chuma. Kukosa nguvu za misuli,na maumivu ya viungio(joints)kutokwa na damu kwenye mafinzi kuchelewa kupona kwa vidonda na kuumwa mara kwa mara ni dalili ya upungufu wa vitamin hivi.Vitamin D hupatikana kwenye mayai, maziwa, samaki na maini. Husaidia katika kukuwa na kuimarisha meno na mifupa. Ugonjwa wa matege kwa watoto na osteoporosis yaani mifupa kuwa milaini husababishwa na upungufu wa vitamin D.Mitamini E hupatikana kwenye alizeti, butter, mchele na peanuts. Husaidi akatika kulinda utando uliopo ndani ya mwili. Mfumo wa fahamu kutokuwa katika hali ya kawaida ni dalili ya upungufu wa vitamin EVitamin K hupatikana kwnye maini na mboga za majani. Husaidia katika kuganda kwa damu baada ya kupata jeraha. Damu kutoka kwa wingi baada ya jeraha ni upungufu wa vitamin K.Mtu atapata matatizo pia kama hata kunywa maji ya kutosha kwa siku. Maumivu ya kishwa huweza kusababishwa na kutokunywa maji ya kutosha. Choo kuwa kigumu huweza kusababishwa na uchache wa kunywa maji.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1855


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za Asali
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za stafeli/soursop
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za stafeli ama soursop Soma Zaidi...

Kazi kuu tatu za Vitamini C mwilini
Vitamini C tunaweza kuvipata kwenye matuinda kama machunwa vina kazi kuu tatu ambazo ni hizi hapa Soma Zaidi...

Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini
hapa Tutakwenda kuona Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini Soma Zaidi...

Ni katika kiungo kipi cha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula virutubisho hufonzwa?
Post hii itakupa elimu kuhusu mfumo wa mmrng'enyobwa chakula unavyo fanyankazi Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Korosho
Soma Zaidi...

Vyakula vyenye madini kwa wingi
Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula vyenye madini kwa wingi Soma Zaidi...

VINYWAJI SALAMA KWA MWENYE KISUKARI
Kuchaguwa vinywaji si jambo rahisi, lakini inabidi iwe hivyo kama una tatizo la kisukari. Je unasumbuka kujuwa vinywaji salama? makala hii ni kwa ajili yako, hapa tutaona vinywaji ambavyo ni salama kwa mwenye kisukari. Soma Zaidi...

Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake
Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake Soma Zaidi...

Faida za kiafya za peaz/ peas
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula peazi Soma Zaidi...

Sababu za kuwa na fangasi ukeni
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwa na fangasi ukeni, ni vitu ambavyo usababisha fangasi ukeni kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

Umuhimu wa kutumia maembe kiafya.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia maembe kiafya, tunajua wazi kuwa maembe ni tunda ambalo lina umuhimu kwenye afya na uwa na vitamini C kwa hiyo tunapaswa kujua faida zake kama ifuatavyo. Soma Zaidi...