image

Vyakula vyenye madini kwa wingi

Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula vyenye madini kwa wingi

VYAKULA VYENYE MADINI KWA WINGI

Kwa kuwa umesha jifunza kazi za madini zilizotajwa hapo juu, basi tambuwa kuwa kuna aina nyingi za madini ambazo baadhi yake zimetajwa hapo juu. Madini haya unaweza kuyapata kwenye mchanganyiko wa vyakula vingi. Lakini kuna vyakula ambavyo madini huwa ni mengi kuliko vyakula vingine. Hapa chini ninakuletea vyakula ambavyo vina madini kwa wingi ambavyo ni:-

 

1. Kwenye mbegu kama mbegu za maboga. Mbegu za maboga zina madini mengi sana. Unaweza kula mbegu za maboga kwa kutafuna, kutumia unga wake kama kiungo cha mboga ama kukaanga na kula kama bisi. Mbegu za maboga na m,begu nyingine zenye mfano wake kama mbegu za matango zina madini kama magnesium, zinc, manganese, copper, selenium, na madini ya phosphorus.

 

2. Kwenye samaki hasa samaki wenye magamba magumu kama kobe (shellfish) jamii ya tondo. Kama umeshawahi kula tondo, utakuwa unaelewa nini klimaamnishwa.kama hutambui nitakujuza. Angalia mfano wa konokono, basi samaki wenye kufanana na konokono wanatembea na majumba yao, ukimshituwa anaingia ndani. Samaki hawa ndio wanaozungumziwa hapa. Samaki hawa wana madini kama selenium, zinc, copper na chuma

 

3. Mboga za majani jamii ya kabichi. Mboga hizi zina madini kama magnesium, potassium, manganese na calcium

 

4. Kwenye nyama hasa nyama za viungo maalumu kama maini na figo. Nyama hizi zina madini kama selenium, zinc, madini ya chuma, na phosphorus.

 

5. Mayai ni moja kati ya vyakula vyema virutubisho vingi sana. Katika mayai kuna madini ya chuma kwa wingi sana, phosphorus, zinc na selenium.

 

6. Maharagwe, maharage ya na madini kama cailcium, magnesium, madini ya chuma, phosphorus,potassium, madini ya shaba na zinc.

 

7. Palachichi, tunda hili lina madini kama magnesium, potasium, manganese na madini ya shaba.

 

8. Maziwa yana madini kama cailcium, potassium, phosphorus, zinc na selenium.

 

9. Viazi mbatat vina madii kama potassium, magnesium, manganese, calcium, madini ya chuma na madini ya shaba.

 

10. Pia madini kama potassium, manganese, shamba na magnesium tunaweza kuyapata kwenye matunda kama, ndizi, fenesi, machungwa, pasheni, nanasi na mapera.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 3189


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Vyakula vya protini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya protini Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula ukwaju
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ukwaju Soma Zaidi...

Kazi za vitamini B na vyakula vya vitamini B
Makala hii inakwenda kukuletea kazi za vitamini B, pia tutajwenda kuona makundi ya vitamini B na kazi za kila kundi. Pia makala hii inakwenda kukufundisha vyanzo na vyakula vya vitamini B. Utajifunza pia kazi kuu za vitamini B kwa ujumla wake. Soma Zaidi...

Faida za kula uyoga
Kula uyoga kwa faida kubwa, ja unazijuwa faida za kula uyoga kiafya Soma Zaidi...

Faida za kiafya za mchaichai/lemongrass
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za mchaichai/lemongrass Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kisamvu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kisamvu Soma Zaidi...

Namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa matumizi mbalimbali
Posti hii inahusu zaidi namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa ajili ya matumizi mbalimbali, Ili kutumia mmea wa mchai chai zifuatazo ni mbinu za kuandaa mmea huu. Soma Zaidi...

VYAKULA VYA VITAMINI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Yafahamu magonjwa nyemelezi kwa watoto chini ya miaka mitano
Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano,. Ni magonjwa yanayowapata watoto wadogo kwa sababu kinga Yao bado ni ndogo. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Epo ama tufaha
Soma Zaidi...

Faida za kula Tango
Matunda ya zamani na ya asili, zijuwe faida za kiafya za tango Soma Zaidi...

Vyakula vizuri kwa vidonda vya tumbo
Hii ni orodha ya vyakula salama na vizuri kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo Soma Zaidi...