image

Fahamu vitamini D, kazi zake vyakula vya vitamini D na athari za upungufu wake

Fahamu vitamini D, kazi zake vyakula vya vitamini D na athari za upungufu wake


VITAMINI D NA FAIDA ZAKE MWILINI

Vitamini D ni vitamini inayosaidia miili yetu iweze kuvyonza madini ya calcium, magnesium na phosphate. Vitamini D hutengenezwa chini ya ngozi kwa kutumia mwanga wa jua. Vitamini D ipo katika makundi makuu mawili nayo ni vitamini D2 na vitamini D3. Vitamini vipo katiaka makundi mengi kuna vitamini A, B, C, D, E na K . katika makala hii tutakwenda kuona zaidi kuhusu vitamini D, namna ambavyo vitamini D hutengenezwa mwilini, Je ni zipi kazi za vitamini D, na upungufu wake unasababisha athari gani mwilini?.



YALIYOMO:
1.Maana ya vitamini D
2.Makundi ya vitamini D
3.Kazi za vitamini D
4.Chanzo cha votamini D
5.Upungufu wa vitamini D



Maana ya Vitamini D
Vitamini D ni matika fat soluble vitamin ambayo imetokana compound za cholesterol. Vitamini D vimegunduliwa mwaka 1922 na Mwanasayansi anayefahamika kwa jina Elmer McCollum. Historia ya uchunguzi huu wa vitamini D ulianzia toka mwaka 1914 wakati Elmer McCollum na Marguerite Davis walipogundua vitamini A



Vitamini hivi vimeitwa D kwa sababu ndio vitamini vya nne kugundulika toka A, B, C na sasa ni vitamini D. ugunduzi wa vitamini D ulianzia kwenye mbwa mgonjwa ambaye alikuwa ana matege. Baadaye ikajulikana kuwa mbwa aliweza kupona matege kwa sababu ya chembechembe amazo baadaye ndiyo zikaitwa vitamini D.



Makundi ya vitamini D
Kama ilivyokuwa vitamini K na vitamini B zina makundi mengi. Basi hata hivyo vitamini D vimegawanyika katika makundi kadhaa, makuu katika kundi hilo ni vitamini D2 na bitamini D3. makundi haya mawili kwa pamoja ndiyo hufahamka kama vitamini D.



Vitamini D1 na vitamini D2 kwa pamoja pia huitwa calciferol. Vitamini D2 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwa ka 1931 na vitamini D3 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwaka 1935.



Kazi za vitamini D
Katika miili yetu vitamini D ina kazi kuu ya kufanya metabolism ya madini ya calcium. Kwa lugha nyepesi ni kuhakikisha kuwa unyonzwaji wa madini ya chumvi ambayo ni calcium, magnesium na phosphate unafanyika vyema ndani ya utumbo mdogo.



Faida za vitamini D:
1.Husaidia kufyonza mwili kufuonza madini ya calcium
2.Husaidia kuboresha afya ya mifupa
3.Husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani
4.Husaidia kuboresha mfumo wa faya
5.Kupunguza uzito na kitambi



Chanzo cha vitamini D
Chanzo kikuu cha vitamini D ni mwanga wa jua ambao husaidia katika utengenezwaji wa vitamini D chini ya ngozi. Kama mtu hataweza kupata mwangaza wa jua vyema kuna uwezekano wa kupata upungufu wa vitamini D.



Pia tunaweza kupata vitamini D kutoka katika vyakula na mboga, kama vile:-
1.Uyoga
2.Yai lililopikwa
3.Maini
4.Samaki



Upungufu wa vitamini D
Upungufu wa vitamini D unaweza kusababisha athari kubwa kwenye afya. Miongoni mwa athari hizo ni:-
1.Matege
2.Udhaifu wa mifupa
3.Mifupa kuvunjika kwa urahisi



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1354


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Vyakula vyenye protini kwa wingi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vyenye protini kwa wingi Soma Zaidi...

Fahamu Fati na kazi zake, vyakula vya fati na athari za upungufu wake
Makala hii inakwenda kukueleza kuhusu fati, vyakula vya fati, kazi zake na athari za upungufu wake Soma Zaidi...

Vyakula vya madini, kazizake na athari za upungufu wa madini mwilini
Je ungependa kujuwa vyakula hivyo ama vyanzo vya madini? Na je ungependa kujuwa ni zipi hasa kazi za madini katika miili yetu?. makala hii ni kwa ajili yako, hapa utakwenda kujifunza mengi kuhusu somo hili. Soma Zaidi...

ELIMU YA UJAUZITO, MIMBA NA KIZAZI
Soma Zaidi...

MATUNDA YENYE VITAMINI C KWA WINGI
Matunda yenye vitamni C kwa wingi ni machungwa, maembe, ndimu na limao, endelea kusoma Soma Zaidi...

Fahamu vitamini K na kazi zake, vyakula vya vitamini k na athari za upungufu wake
kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake mwilini. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Kunazi
Soma Zaidi...

Vyakula anavyopaswa kutumia mama mjamzito
Posti hii inahusu zaidi vyakula anavyopaswa kutumia mama mjamzito, mama mjamzito ni mama ambaye amebeba kiumbe ndani kwa hiyo anapaswa kutumia vyakula vyenye virutubisho mbalimbali vitakavyomsaidia mtoto kukua vizuri. Soma Zaidi...

Habari ndugu naomba kuuliza eti mtu akipaliwa na asali anakufa?
Post hii inakwenda kukujulisha hatari za kupaliwa na asali ama kitu kingine kama muulizaji alivyouliza. Soma Zaidi...

FAIDA ZA VITAMINI C NA UMUHIMU WA VITAMINI C MWILINI
Utafahamu faida za vitamini C mwilini pamoja na kujuwa umuhimu wa vitamini C Soma Zaidi...

VYANZO VYA VYAKULA VYA FATI, PROTINO NA WANGA NA FAIDA ZAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Faida za kula Palachichi
Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako Soma Zaidi...