image

Vyanzo vya mwanamke kushindwa kupata ujauzito

Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya mwanamke kushindwa kupata ujauzito, kwa sababu kuna sababu nyingi ambazo Usababisha mwanamke kushindwa kupata ujauzito kama tutakavyoona hapo mbeleni

Vyanzo vya mwanamke kushindwa kupata ujauzito.

1. Mayai kushindwa kupevuka.

Hili ni tatizo ambalo uwakumba wanawake kwa kiwango cha asilimia arobaini kwa hiyo

mayai yakishindwa kupevuka usababisha kuwepo kwa ugumba.

 

2. Maambukizi sugu ya PID.

Kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi ya PID usababisha sehemu mbalimbali za via vya uzazi kuziba na kushindwa kuruhusu mayai kupita kwa ajili ya urutubishaji.

 

3. Mvurugiko wa homoni.

Na lenyewe hili ni tatizo kubwa ambapo homoni uweza kuongezeka au kupungua kwa hiyo kama ni homoni za uzazi zikapungua  ni shida na ikiwa zikaongezeka na nalo ni tatizo jingine kwa hiyo homoni zinapaswa kulinga kabisa na kuwa sawia.

 

4. Kuwepo kwa uvimbe au maji maji kujaa kwenye sehemu ya kupitisha mayai.

Kuna wakati mwingine mirija ya kupitisha mayai inaweza kujaa maji maji au kwa wakati mwingine kuziba kabisa kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha maambukizi , kwa hiyo mayai hayawezi kupita kutoka kwenye ovaries na kuingia kwenye mirija kwa ajili ya urutubishaji.

 

5. Au wakati mwingine Kuna wakati panakuwepo na uvimbe , na pia uvimbe huo hauwezi kuruhusu mayai kupita kutoka kwenye ovaries mpaka kwenye mirija ya urutubishaji mpaka uvimbe huo kuondolewa ndipo mayai yanaweza kupita kwa ajili ya urutubishaji.

 

6. Mayai kuharibika kabla ya umri.

Kuna wakati mwingine mayai yanaweza kuwepo kabisa na ya kutosha na kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi mayai hayo uharibika kabla ya umri wake hali ambayo usababisha kuwepo kwa kiwango kikubwa cha ugumba kwa akina Mama kwa hiyo matibabu ni lazima Ili kuweza kuzuia maambukizi ya nayosababisha kutokomaa kwa mayai.

 

7. Kuwepo kwa matatizo au asidi nyingi kwenye mlango wa kizazi na uke .

Kwa sababu asidi ya kwenye uke uwa ni ya kawaida kwa ajili ya kuruhusu mbegu kupita na kurutubisha mayai Kuna wakati asidi inakuwa nyingi na kusababisha kuuua megu za kiume kabla hazijaendea kurutubisha mayai.

 

8. Kuwepo kwa makovu kwenye mji wa mimba.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na makovu kwenye mji wa mimba hali ambayo usababisha mimba kutoweza kutungwa kwa sababu ya kutokuwepo sehemu ya kutungwa.

 

 

9. Kulegea au kuziba kwa shingo ya kizazi.

Kuna wakati kunakuwepo kwa tatizo la kulegea na kuziba kwa shingo ya kizazi hali ambayo usababisha  mimba bkushindwa kutungwa.

 

10. Uzito wa kupita kiasi.

Kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta mwilini usababisha kitendo cha urutubishaji kuleta shida na kusababisha ugumba, kwa hiyo akina Mama wenye uzito wa kupita kiasi ni vizuri kabisa kupunguza Uzito na kupata uja uzito.

 

11. Unywaji wa pombe kupita kiasi na uvutaji wa sigara kupita kiasi.

Kuna akina Mama wenye tatizo la kuvuta sigara kupita kiasi na kupiga pombe ya uhakika hali ambayo usababisha baadhi ya homoni kushindwa kufanya kazi vizuri na hatimaye kuwepo kwa ugumba.

 

12. Magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji.

Kwa kawaida Kuna tatizo la magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji nayo uharibu  ubora wa  mayai na mzunguko wa damu kwa hiyo ni vizuri kabisa kutibu magonjwa haya kabla hayajaleta matatizo.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2286


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Yajue mazoezi ya kegel
Posti inahusu zaidi mazoezi ya kegel, ni mazoezi ambayo ufanywa na watu wengi na sehemu yoyote yanaweza kufanywa kama vile chumbani, sebuleni, uwanjani na sehemu yoyote ile na kwa watu tofauti. Soma Zaidi...

Fahamu Mambo ya hatari yanayosababisha kuzaliwa kabla ya wakati (premature)
Kuzaliwa kabla ya wakati humpa mtoto muda mdogo wa kukua tumboni. Watoto waliozaliwa kabla ya wakati, hasa wale waliozaliwa mapema, mara nyingi huwa na matatizo magumu ya matibabu. Soma Zaidi...

Watu ambao hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango
Post hii inahusu zaidi watu ambao hawapaswi kutumia njia za uzazi wa mpango, Ni watu ambao Wana matatizo mbalimbali endapo wakitumia wanaoweza kuleta madhara mbalimbali. Soma Zaidi...

Je siku ya kwanza kabisa ya ovulation mimba inakuwa ni uhakika kupata mimba?
Watu wengi wanadhania kuwa kufanya tendo la ndoa katika siku hatari ni lazima kuwa utapata ujauzito. Hili sio sahihi kabisa. Post hii itakwenda kuangalia jambo hili zaidi. Soma Zaidi...

Mambo muhimu kuhusu mbegu za kiume
Post hii inahusu zaidi mambo muhimu ambayo tunapaswa kujua au kufahamu kuhusu mbegu za kiume, kwa kuwa mbegu za kiume usaidia katika utungaji wa mimba kwa hiyo ni vizuri kabisa kuzitunza Ili kuweza kuepuka matatizo mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kwa s Soma Zaidi...

Madhara ya kutumia madawa ya kupunguza maumivu
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya kupunguza maumivu,ni madhara ambayo utokea kwa mtu anayetumia madawa ya kupunguza maumivu. Soma Zaidi...

Habar doctor mm nahc kuwa ni mjamzito tumbo la chin ya kitovu linaniuma muda mwingine linaacha chuchu zinawasha na cku niliyokutana na mume wangu ni cku 11
Kuna uwezekano una ujauzito ila hujajijuwa, huwenda hujapata dalili zozote. Unataka kujuwa kama una ujauzito baada ya tendo la ndoa. Soma Zaidi...

Namna ya kutunza uke
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza uke, tunajua wazi kuna magonjwa mbalimbali yanayoweza kutokea iwapo uke hautaweza kutunzwa vizuri na pia uke ukitunzwa vizuri kuna faida ya kuepuka maradhi ya wanawake kwa njia ya kutunza uke. Soma Zaidi...

Kutokwa maji yan seminal swhemu za siri kwa mwanamke nidalili ya ugojwa gan?
Kutokwa Majimaji sehemu za siri kwa mwanamke sio jambo la kushangaza na kuhisivunaumwa. Majimajivhaya ndio huboresha afya ya uzazi kwa kusafisha na kulinda via vya uzazi. Lakini majimajivhaya yakiwa mengi, ama yanawasha ama yanaharufu haa ndipo kwenye tat Soma Zaidi...

Mambo yanayopelekea ugumba.
Post huu inahusu zaidi mambo yanayopelekea ugumba kwa wanaume, ni mambo ambayo uchangia au upelekea mwanaume kukosa uzazi. Soma Zaidi...

UUME KUWASHA
Post yetu imebeba mada inayohusiana na wanaume wanaowashwa Uume embu tuone dalili zinazopelekea kuwashwa kwa penis. Uume(penis) ni party ya mwanaume ya sehemu za siri.pia wanaume ambao hawajatahiriwa(unsircumside) kwasababu Ile ngozi ya juu husababishwa k Soma Zaidi...

Dalili kuu za mwanzo za mimba changa, kuanzia siku ya kwanza
Ni ngumu ila nitakujuza namna ya kuitambuwa mimba ya siku moja hadi 3, mimba ya wiki moja na mimba ya miezi mitatu kwa dalili. Soma Zaidi...