image

Vyumba vidogo vidogo kwenye chumba cha upasuaji

Post hii inahusu zaidi juu ya vyumba vidogo vidogo ambavyo Vimo kwenye chumba cha upasuaji, ingawa chumba cha upasuaji ni kimoja ila kuna vyumba vingine vidogo ambavyo vinatumika kwa kazi mbalimbali kama tutakavyoona.

Vyumba vidogo vidogo kwenye chumba cha upasuaji.

1.chumba cha mapokezi na kuruhusu mgonjwa kutoka kwenye upasuaji.

Hiki ni mojawapo ya vyumba vidogo ambavyo Vimo kwenye chumba cha upasuaji katika chumba hiki mgonjwa upokelewa na kuangalia kama ana sifa za kuingia kwenye upasuaji na vile vile kwenye chumba hiki mgonjwa akimaliza kufanyiwa upasuaji upitia hapa ili kuhakikisha kuwa kama mgonjwa yu hai au ana tatizo lolote lililompata kama mgonjwa yuko vizuri huweza kupelekwa kwenye chumba muhimu kwa ajili ya kupona.

 

2.Chumba cha mtoa dawa ya usingizi,

Hiki ni chumba maalum ambako mtoa huduma ya usingizi ukutana na mgonjwa na kumuuliza pamoja na kujadiliana kuhusu dawa ya usingizi anayotaka kupewa kama ni ya mwili mzima au niya nusu kwa hiyo Mgonjwa uweza kuchagua, pamoja na uchaguzi wa mgonjwa na mtoa huduma hii anapaswa kumshauri kulingana na hali halisi ya mgonjwa.

 

3.Chumba cha kupumzika Mgonjwa baada ya upasuaji.

Hiki ni chumba ambacho mgonjwa anapumzika baada ya upasuaji katika chumba hiki mgonjwa uangaliwa zaidi na kupewa huduma zote mpaka pale atakapopona na kurudia kwenye hali yake ya kawaida kwenye chumba hiki panapaswa kuwepo na gasi ya oxygen, maji ya kutosha kwa ajili ya mgonjwa mgonjwa anapaswa  kuwa makini ili kuepuka matatizo baada ya upasuaji kama vile kuishiwa damu na mengine kama hayo.

 

4.Chumba maalum cha kusafishia vifaa.

Hiki ni chumba ambacho vifaa vyote vinavyotumika wakati wa upasuaji vinasafishiwa kwa hiyo chumba hiki kinapaswa kuwepo kwa maji safi ya sabuni, maji yenye chlorine, maji ya kusuuzia na baada ya kutoa uchafu huu vinapaswa kupelekwa ili kuingizwa na kuua bakteria wote na mtu anayefanya kazi kwenye chumba hiki anapaswa kuwa na Elimu  ya kutosha na awe amesomea kazi hiyo kwa kufanya hivyo wadudu wote wataweza kufa na kuzuiliwa kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

 

5. Chumba cha kubadilishia nguo.

Tukumbuke kuwa kabla ya kuanza upasuaji ni lazima kubadilisha nguo za nyumbani na kuvaa nguo za upasuaji hii ufanyika ili kuzuia kusambaa kwa bakteria kutoka kwa mhudumu kwenda kwa mgonjwa kwa hiyo ndo maana kuna chumba maalum kwa ajili ya kubadilisha nguo





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 525


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kitabu Cha Afya
Soma Zaidi...

DONDOO 100 ZA AFYA
Pata dondoo 100 za Afya Soma Zaidi...

Umuhimu wa kuvaa nguo za upasuaji.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa nguo za upasuaji, tunajua wazi kuwa, wakati wa upasuaji tunapaswa kusafisha chumba na mazingira yake lengo ni kuhakikisha kuwa tunazuia wadudu wasisambae au kuingia kwenye mwili wa binadamu. Soma Zaidi...

UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
2. Soma Zaidi...

DARASA LA AFYA, AFYA YA UZAZI, MARADHI NA LISHE BORA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

AFYA YA UZAZI (UJAUZITO, KULEA WATOTO, AFYA YA MIMBA NA MTOTO, MAGONJWA YA KINAMAMA NA WANAUME)
Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

MAANA YA AFYA, ni nani aliye na afya?
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Dondoo za afya 81-100
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dondoo za afya Soma Zaidi...

DARASA LA AFYA NA AFYA YA UZAZI
Jifunze mengi kuhusu Afya, kuwa nasi kwenye makala hii hadi mwisho. Soma Zaidi...

ilinde Afya yako
Hiki ni kitabu kilichosheheni masomo zaidi kuhusu Afya yako, vyakula pamoja na maradhi sugu. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuepuka magonjwa ya figo
Figo ni moja katika orgn zenye umuhimu sana mwilini na endapo itaatirika kwa namna yeyote ile, madhara makubwa kwenye mwili yanaweza kutokea na hata kifo. Katika post hii utajifunza jinsi ya kulinda mwili wako dhidi ya matatizo ya figo Soma Zaidi...