Posti hii inahusu zaidi wajibu wa Mama mjamzito katika kileo mimba sio yeye tu Bali na wote waliomzunguka wanapaswa kuhakikisha kuwa mama mjamzito anapaswa kufanyiwa huduma zote Ili kuweza kujifungua salama na bila shida yoyote.
Wajibu wa Mama mjamzito.
1. Mama mjamzito anapaswa kuwa na mda wa kutosha wa kupumzika.
Kwa sababu mama anakuwa na matalajio ya kujifungua salama anapaswa kupumzika kwa mda mrefu na hasa hasa anapaswa kuinua miguu juu anapokuwa amelala na anapaswa kulala chini wakati wa alfajiri hayo yote yana mpatia mazoezi ya kufaa na kutosha anapokaribia kujifungua na hivyo kumwezesha mtoto kukua vizuri na Baadae kujifungua bila shida, kwa hiyo jamii na ndugu wa familia wanapaswa kuhakikisha kuwa Mama anapata mda wa kutosha wa kupumzika.
2. Mama anapaswa kipata chakula Bora chenye virutubisho.
Kwa kumpatia Mama chakula chenye virutubisho umfanye Mama kuwa na madini yabayohitajika mwilini kama vile madini ya chuma ambayo usaidia wakati wa ujauzito, vyakula vyenye vitamini A ambavyo umsaidie mtoto aweze kuona, kwa hiyo Mama anapaswa kupatiwa Aina zote za vyakula kama vile wanga, protein, mafuta na mboga mboga za majani ambazo uongeza damu mwilni na wakati wa kujifungua anakuwa na damu ya kutosha. Kwa hiyo jamii ziachane na Mila potofu kuhusu vyakula kwa wanawake.
3. Kuepuka Aina yoyote ya kemikali .
Mama mjamzito anapaswa kuepuka Aina yoyote ya kemikali kama vile pombe ambayo ikiingia ndani uweza kuaribu ubongo wa mtoto katika makuzi anapokuwa tumboni mwa mama,Moshi wa sigara nao ni hatari kwa Mama mjamzito kwa sababu unaweza kuharibu mapafu ya mtoto akiwa tumboni kwa mama, Madawa ya kulevya pia nayo ni hatari kwa afya ya Mama na Mtoto, kwa hiyo mtoto akiwa tumboni kwa mama anaweza kuzaliwa akiwa zezeta kwa Sababu ya madawa ya kulevya.
4. Kuwepo kwa mhudumu karibu na Mama mjamzito.
Mama mjamzito anapaswa kuwa na mhudumu wa karibu kwa mfano wataalamu wafya au mkunga Ili kuhakikisha kujua siku na mda wa kujifungua kwa Mama kwa kufanya hivyo tunaweza kuepusha madhara mbalimbali ambayo uweza kuwakuta wanawake wakati wa kujifungua kwa hiyo Mama mjamzito anapaswa kwenda klinic mara kwa mara Ili kuangalia afya yaka na maendeleo ya mtoto kwa ujumla .
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya kuharibika kwa mimba kuanzia miezi zero mpaka miezi mitatu, kwa sababu hii ni miezi ya kwanza kabisa Kuna sababu au vyanzo vya kuharibika kwa mimba katika kipindi hiki.
Soma Zaidi...Nitakujulisha siku ya kupata mimba na sifa zake, na namna ya kuweza kuitafuta
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kutunza joto la mtoto mara tu anapozaliwa,tunajuwa wazi kuwa Mama anaweza kujifungulia sehemu yoyote ile kabla hajafika hospitalini kwa hiyo mtoto anapaswa kuwa na joto la mwili la kutosha i
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mtoto aliyetanguliza matako wakati wa kuzaliwa, kwa kawaida tunajua kwamba mtoto wakati wa kuzaliwa ni lazima atangulize kichwa ila Kuna kipindi mtoto anatanguliza matako, kuna aina nne za mtoto kutanguliza matako.
Soma Zaidi...Je kupata maumivu sehemu zinazoota mavuzi na kuwa namaumiv wakat wa haja ndogo na pia kwenye kichwa cha uume kunakua kama kunavimb hizo syo dalili moja wapi?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za mtoto kuzaliwa akiwa na miezi Saba na nane kwa kawaida mtoto wa hivi anakuwa hajafikisha mda wake kwa hiyo uzaliwa akiwa na miezi saba na nane, kwa hiyo kuna sababu mbalimbali kama tutakavyoona
Soma Zaidi...Je ni kweli kupima kimoja cha mloka kinaweza kupima mimba zaidi ya mara moka?
Soma Zaidi...Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hatari za kutokwa na damu wakati wa ujauzito, hali hii utokea wakati wa ujauzito ambapo Kuna baadhi ya wajawazito utokwa na damu jambo ambalo hatupaswi kutarajia kwa sababu tunafahamu kabisa mama akishapata ujauzito na damu zinakom
Soma Zaidi...