Walio kwenye hatari ya kupata Maambukizi kwenye mifupa

Walio kwenye hatari ya kupata Maambukizi kwenye mifupa

Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata Maambukizi kwenye mifupa,

Walio katika hatari ya kupata Maambukizi kwenye mifupa.

1. Waliopata ajali na kushambuliwa kwa mifupa.

Hawa waliopatwa na ajali na mifupa ikishambuliwa wapo kwenye hatari ya kupatwa na ugonjwa huu wa Maambukizi kwenye mifupa, kwa sababu wadudu au bakteria wakishaingia kwenye mifupa na wakakuta tayari kuna udhaifu fulani na pengine mgonjwa hakutibiwa vizuri ipasavyo hali ya kuwepo kwa Maambukizi inakuwepo kwa kiasi kikubwa , kwa hiyo mtu aliyepata ajali anapaswa kutibiwa vizuri na kujilinda mda wote hasipatwe na magonjwa yoyote.

 

2. Kuwepo kwa vyuma kwenye mfupa au kitu chochote ambacho kimo na hakipaswi kuwepo kwenye mifupa kwa kitaalamu tunaweza kusema foreign body, kwa Sababu vitu hivi sio mahali pake vilipo pengine vimekuwepo ili kusaidia kazi mbalimbali kwenye mwili kwa sababu ya udhaifu, kwa hiyo watu wenye vitu kama hivi wana asilimia kubwa kupatwa na Maambukizi kwenye mifupa kwa hiyo wanapaswa kuwa makini ili kuepuka na maambuy kwenye mifupa .

 

3. Kushuka kwa kinga ya mwili.

Tunajua wazi kuwa kinga ya mwili ikishuka usababisha magonjwa mengi kuwepo kwa hiyo watu wale ambao kinga zao za mwili zimeshuka wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha wanajikinga na ugonjwa huu wa Maambukizi               kwenye mifupa, kwa hiyo wale walio na magonjwa yanayopunguza kinga ya mwili kama vile HIV na mengineyo wahakikishe kuwa wanatumia dawa ili kuweza kuweka kinga yao sawa na kuepuka ugonjwa huu wa Maambukizi kwenye mifupa.

 

4. Wenye umri mkubwa nao wana hatari ya kupata ugonjwa wa Maambukizi kwenye mifupa.

Tunajua kubwa umri ukiongezeka na baadhi ya viungo vinapungua kufanya kazi kwa hiyo wale wenye umri mkubwa ute ute uisha kwenye mifupa na baadhi yao mifupa uanza kuuma kwa hiyo kiasi cha kushambuliwa na bakteria inakuwa kubwa, kwa hiyo wenye umri mkubwa wanapaswa kula vyakula vya kuongeza ute ute kwenye mifupa na kula vyakula vya kuongeza kinga mwilini.

 

5. Kwa hiyo tukumbuke kwamba ugonjwa huu ukitibiwa mapema unatibika na pia tuwe na utaratibu wa kwenda hospitali mara baada ya kusikia mabadiliko kwenye mwili na tunaweza kupunguza magonjwa mengine ambayo ni nyemelezi.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 2214

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 ai web app     πŸ‘‰2 web hosting     πŸ‘‰3 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰5 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Dalili za saratani ya kibofu Cha nyongo

Saratani ya kibofu cha nyongo ni Saratani inayoanzia kwenye kibofu cha nyongo. Nyongo yako ni kiungo kidogo, chenye umbo la peari upande wa kulia wa tumbo lako, chini ya ini lako. Kibofu cha nyongo huhifadhi nyongo, Kioevu cha usaga

Soma Zaidi...
Umuhimu wa kuandika hisia zako (Journaling) kwa afya ya akili.

​Gundua jinsi ya kuandika hisia zako (journaling) kunavyoweza kuboresha afya ya akili, kupunguza msongo wa mawazo, na kukuza utambuzi binafsi. Soma mwongozo huu wa kitaalamu kuhusu mbinu na faida za kisayansi za uandishi wa kila siku.

Soma Zaidi...
Ni Nini husababisha kukosa choo? (Constipation)

Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazopelekea kukosa choo ,yaani kinyesi kuwa kigumu au kukosa kabisa choo.

Soma Zaidi...
Dalili za VVU/UKIMWI Ni zipi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za VVU/ UKIMWI

Soma Zaidi...
Nini chanzo cha malaria

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu chanzo cha ugonjwa wa malaria

Soma Zaidi...
Mie ni mwanamke ninamaumivu chini ya kitovu upande wa kushoto, na nikishika tumbo nahisi kitu kigumu upande huo huo wa kushoto... hii itakua ni nini?

Je unasumbuliwa na maumivuvya tumbo chini ya kitovu upande wa kushito. Post hii itakuletea sababu za maukivubhayo na nini ufanye.

Soma Zaidi...