Walio kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu

Post hii inahusu Zaidi watu walio kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu, pamoja na kuwepo Kwa sababu zinazopekekea kupata tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu ila Kuna watu wenye hali Fulani wako kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu kama

Walio kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu.

​​​​​​1. Watu wenye matatizo kwenye mfumo wa ubongo au Kwa kitaalamu central nervous system, au Kwa lugha ya kawaida wale ambao wanaanguka kifafa Kwa ujumla.

Kama tulivyoona kwenye Saba za kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu ni pamoja na kitendo Cha kuhama bakteria kutoka sehemu mbalimbali za mwili na kuingia kwenye mfumo wa hewa na kushambulia mapafu, Kwa hiyo Kwa wanaokuwa na kifafa pengine uanguka chini na kuzilai Kwa hiyo mate kutoka mdomoni yanaweza kuingia sehemu ya mfumo wa hewa na kusababisha bakteria ambao wapo mdomoni na kuingia kwenye mfumo wa hewa na kushambulia mapafu.

Kwa hiyo inawezekana kwenye jamii zetu wagonjwa Hawa tunaishi nao ni ndugu zetu,jamaa na marafiki Kwa hiyo ili kuepuka na tatizo hili ikitokea mgonjwa Kaanguka kifafa ni vizuri kabisa kumlaza vizuri ili kuepuka tatizo la kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu,ni vizuri kumlaza upange ili mate yadondoke chini au kumlaza Chali na kichwa kuangalia pembenu ili kuepuka mate yasiingie Kwenye mfumo wa hewa.

 

 

2. Pia na wale wenye kikohozi kikali Cha mara Kwa mara na wale wenye matatizo kwenye kumeza.

Kwa upande wa kikohozi Cha Mara Kwa mara wanaweza kukohoa na kusababisha makohozi kuchanganyikana na mate ya mdomoni na baadae kurudi kwenye mfumo wa hewa hasa pale mgonjwa akiwa anakohoa na akapaliwa tena,Kwa hiyo ni vizuri kabisa kutibu kikohozi Kwa watu wenye matatizo hayo .

Kwa upande wa watu wenye matatizo kwenye kumeza na wenyewe wapo hatarini kupata usaha kwenye mapafu Kwa sababu wakiwa wanameza Kwa shida pengine ni Kwa sababu ya maumbile wanaweza kusababisha baadhi ya vyakula kuingia kwenye mfumo wa hewa na kuingia pamoja na bakteria na kusababisha madhara kwenye mfumo wa.

 

 

 

3. Watumiaji wa madawa ya kulevya na wavutaji wa sigara.

Hawa nao wapo kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu Kwa upande wa wavutaji wa sigara Kuna wakati mwingine wanapovuta ule Moshi ukiingia kwenye  mfumo wa hewa uweza kushambulia mapafu na kusababisha makovu kwenye mapafu hatimaye kusababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu,Kwa hiyo wavutaji wa sigara wanapaswa kuwa makini sana Kwa kupunguza kiwango Cha sigara au ikiwezekana kuacha kabisa Kwa sababu hata kwenye viwanda vya kutengeneza sigara wanakwambia kwamba , sigara ni hatari Kwa afya yako.

 

Vile vile na watumiaji wa madawa ya kulevya nao wanapata madhara Yale yale kama wavutaji wa sigara iwe ni njia ya kuvuta au kujidunga Kwa sindano wote wanapatwa na matatizo hayo hayo,Kwa hiyo elimu ni Bora Kwa wavutaji wa madaw ya kulevya kuhusu madhara kwenye mapafu ili waweze kubadili mfumo wa maisha na kuweza kuachana na hizo bangi.

 

 

4. Watumiaji wa pombe kupita kiasi

Hawa nao wapo hatarini kupata usaha kwenye mapafu,Kwa sababu kwenye pombe Kuna kemikali mbali mbali ambazo mtumiaji anapokuwa anatumia zikifanikiwa kuingia kwenye mapafu usababisha mapafu kushambuliwa na kusababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu,na pia zike pombe zinazopikwa kienyeji ni mbaya Zaidi Kwa sababu kemikali yake ni kubwa Zaidi, mbaya Zaidi ni pale mtumiaji anapotumia Kwa kiwango kikubwa na Cha kupitiliza na hatimaye kupoteza fahamu na kuanza kutapika hali ambayo usababisha baadhi ya matapishi kutoka kwenye mmengenyo wa chakula na kuingia kwenye mfumo wa hewa na kusababisha mapavu kushambulia na kusababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

Kwa hiyo wanywaji wa pombe wanapaswa kuwa makini katika matumizi ya pombe na kuwa na kiasi ,wanywe pombe za starehe sio kuzidisha na hatimaye kujiletea matatizo ya ki afya 

 

 

5. Walio na maambukizi kwenye koromeo au Kwa kitaalamu oesophagus.

Kuna wakati mwingine maambukizi kwenye sehemu ya kiromeo usababisha kuwepo na wadudu, wanaweza kuwa bakteria , virus au wadudu wowote wale, kwa hiyo tunapaswa kufahamu kwamba kwenye sehemu ya koromeo wadudu wanaweza kuhama na kwenda kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

 

 

6. Pia na wale wenye Kansa ya mapafu wapo tayari kupata usaha kwenye mapafu.

Kwa Sababu ya kuzalishwa Kwa seli ambazo usababisha kuwepo Kwa kitu kingine kwenye seli za kawaida usababisha kuwepo Kwa maambukizi kwenye mapafu na kusababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu,Kwa hiyo katika kutoa huduma Kwa wagonjwa wa Kansa ya mapafu ni wazi kwamba kunakuwepo na uwezekano wa kupata usaha kwenye mapafu.

 

 

7. Wale wanaotumia mionzi kwenye matibabu ya Kansa ya mapafu au sehemu yoyote ile inayohusika na mfumo wa upumuaji.

Kwa kawaida katika matumizi ya mionzi kwenye matibabu ya Kansa yoyote ile ya mfumo wa hewa Kuna uwezekano kabisa wa kuharibu mfumo wa hewa ambao uambatana na kuwepo Kwa kemikali inayohusika na kuuua seli ambazo hazihitajiki Kwa kitaalamu huitwa abnormal sell,Kwa hiyo na hali hii usababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

 

 

8. Vile vile na watu wenye upungufu wa Kinga mwilini.

Tunafamu kwamba Kinga mwilini ikishapungua Kuna uwezekano kabisa wa kuwepo Kwa magonjwa nyemelezi Kwa hiyo na hii inawezekana kabisa kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu Kwa sababu ya kuwepo Kwa Kinga ndogo kwenye mwili.

 

 

 

9.kuwepo Kwa magonjwa kwenye mfumo wa upumuaji ambayo utumia mda mrefu.

Pengine Kuna tatizo la kuwepo Kwa magonjwa kwenye mfumo wa upumuaji ambayo utumia mda mrefu  na bila matibabu Kwa kitaalamu huitwa prolonged infections of respiratory system,kwa mfano nimonia ya mda mrefu na ambayo haina matibabu nayo inawezekana kusababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu,na vile vile pumu ya mda mrefu hasa hasa kama hakuna matibabu na yenyewe usababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu,Kwa hiyo ni vizuri kabisa kutibu magonjwa yote yanayohusika na mfumo wa upumuaji Kwa wakati Kwa sababu bakteria au virusi na maambukizi mengine yote yanaweza kuhama kutoka kwenye sehemu yoyote ile ya mfumo wa hewa na kushambulia mapafu na kusababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

 

 

 

10. Upasuaji kwenye mapafu.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na upasuaji kwenye mapafu ili kutoa pafu moja kama limeshambuliwa sana na magonjwa,Kwa kawaida upasuaji wa namna hii uhitaji umakuni wa hali ya juu Kwa wakati mwingine Kuna complications  baada ya upasuaji ambazo usababisha kuwepo Kwa maambukizi kwenye sehemu ya mapafu ambapo upasuaji umefanyika, Kwa hiyo inawezekana pia kwenye pafu ambalo limefanyiwa upasuaji likapatwa ma tatizo kama Hilo la maambukizi na kusababisha kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu Kwa hiyo ni vizuri kabisa baada ya kumaliza upasuaji ni kutumia antibiotics ambazo zina uwezo wa kuzuia maambukizi kwenye mapafu.

 

 

11. Familia kuwa na historian ya kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu.

Kuna wakati mwingine na ni Kwa mara chache Kuna familia nyingine unakuta Kuna tatizo hili la kuwepo Kwa wagonjwa wa usaha kwenye mapafu , inawezekana isiwe Kwa familia yote ila akatokea mgonjwa mmoja mmoja mwenye tatizo hili,Kwa hiyo ikitokea kwenye familia ni kuwepo Kwa umakini na matibabu yanapaswa kutokatika kwenye familia hiyo yenye kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu,na pia kuhakikisha kuwaleta wagonjwa hospital ili waweze kupata matibabu na vile vile kuepuka inyanyasaji Kwa wagonjwa wa tatizo hilo.

 

 

12. Kwa hiyo hapo juu sio sababu za moja Kwa moja ila ni viashilia au watu walio kwenye hatari ya kupata usaha kwenye mapafu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 749

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Kitabu cha Afya    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

UGONJWA WA KASWENDE

Kaswende ni maambukizi ya bakteria kawaida huenezwa kwa kujamiiana pia ugonjwa huu hujulikana kama syphilis. Ugonjwa huu huanza kama kidonda kisicho na maumivu kwa kawaida kwenye sehemu zako za siri, rektamu au mdomo

Soma Zaidi...
Dalili za za kuwepo kwa maambukizi chini ya kitovu

Posti hii inahusu zaidi dalili za kuonyesha kuwa Kuna maambukizi kwenye kitovu hasa hasa chini ya kitovu.

Soma Zaidi...
Vidonda vya tumbo chanzo chake na dalili zake

Katika post hii utajifunz akuhusu vidonda vya tumbo na jinsi vinavyotokea. Utajifunza pia tahadhari anazopasa mtu achukuwe na vyakula salama anavyopaswa kula.

Soma Zaidi...
Kichwa kinaniuma mbele sielewi nini

Zijuwe sababu za kuumwa nankichwa upande mmoja wa kichwa.

Soma Zaidi...
Tatizo la kujaa mate mdomoni nimeambiwa nina minyoo

Mie ni kijana wa kiume umri 33, nna tatizo la kujaa mate mdomoni nimeambiwa nna minyoo lakini hata nikinywa dawa sioni afadhali, niliona labda ni pombe nikapumzika kunywa tatizo lipo pale pale japo nisipokunywa haliwi kwa ukubwa ule ila lipo.

Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo kitomvuni, sababu zake na dalili zake

Hapa utajifunza sababu za kuwepo na maumovu ya tumbe kitomvuni.

Soma Zaidi...
VYANZO VYA MINYOO: nyama isiyowiva, maji machafu, kinyesi, uchafu wa mazingira, udongo

VYNZO VYA MINYOO Kama tulivyoona hapo mwanzo kuusu aina za minyoo, pia tumeona vyanzo vya minyoo hao kulingana na aina zao.

Soma Zaidi...
Dalili na ishara za shambulio la moyo

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Dalili na ishara za shambulio la moyo. Shambulio la moyo huzuia damu yenye oksijeni kufika kwenye moyo hivyo hupelekea tishu kufa. Na Ugonjwa huu mtu akicheleweshewa matibabu huweza kupata mshtuko wa moyo mpaka kifo.

Soma Zaidi...
Dalili za tonsillitis (mafindo mafindo)

Tonsillitis kwa kiswahili hujulikana kama mafundomafundo ambayo hutokea pande mbili karibu na Koo na huwa na uvimbe na zikikaa kwa muda bila matibabu hutoa usaha.Dalili na dalili za ugonjwa wa tonsillitis ni pamoja na

Soma Zaidi...
Mtoto Kutokwa na matongo tongo tiba ake nin sababu

Hili ni swali lililowahi kuulizwa na moja ya wasomaji wetu

Soma Zaidi...