image

Yajue magonjwa nyemelezi.

Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi ambayo kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili inashuka.

Magonjwa nyemelezi

1.Ugonjwa wa kifua kikuu

 Ni mojawapo ya magonjwa nyemelezi kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili ikishuka huu ugonjwa unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa au endapo mgonjwa hajaanza kutumia dawa na pengine uambukizwa pale mtu akishika makohozi ya mgonjwa wa kifua kikuu na kama hajanawa mikono anaweza kushika kitu chochote Cha kula akajiambukiza, zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa kifua kikuu.

_ kukohoa ndani ya wiki mbili na zaidi

_ kupungua uzito

_ kuwa na joto hasa wakati wa usiku

_ Homa za mara kwa mara

_ makohozi kuwa na damu

 

2. Magonjwa ya ngozi

Huu ni ugonjwa ambao pia ni nyemelezi kwa mtu ambaye kinga yake Iko chini, ambapo ngozi ya mgonjwa ushambulia sana na bakteria na kufanya mwili uwe na maupele upele ambayo hayaponi au uchukua mda mrefu kupona na pengine vidonda uweza kusababisha maambukizi mengine kama vile Homa kupanda zaidi na kusababisha madhara makubwa hasa kwa watoto kama vile degedege kwa hiyo tunapaswa kuwa macho iwapo kinga ya mwili ikishuka na kutafuta njia ya kuipandisha.

 

3.Kandidiasisi

Ni ugonjwa nyemelezi ambao utokea ikiwa kinga ya mwili ikishuka na hasahasa ushambulia sehemu za Siri na kusababisha maupele na kumfanya mtu aanze kujikinga , huu ugonjwa usababishwa na fangasi ambazo ushambulia sehemu za Siri,kwahiyo unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana kwa mtu Mwenye ugonjwa na ambaye Hana,kwa hiyo mtu akiwa na huu ugonjwa anapaswa kwenda hospitalini Ili akapatiwe dawa maana ugonjwa huu upo na unatibika

 

4. Mkanda wa jeshi.

Huu ni ugonjwa ambao utokea Baada ya kinga ya mwili kushuka, ugonjwa huu usababishwa na virusi ambaye ushambulia kulingana na sehemu ya nevu zinapopita kwa hiyo maambukizi uendana na nevu ya sehemu ndo maana utakuta mtu amishambuliwa sehemu fulani, Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na Homa kutokea, maumivu kwenye sehemu ya maambukizi. Mgonjwa wa mkanda wa jeshi anaweza kupatiwa dawa kwa kufuata nadalili na hali ya maumivu na vidonda vilivyopo.

 

Magonjwa nyemelezi yakitokea ni lazima mgonjwa apelekwe hospitali mara moja Ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kwa sababu iwapo kinga imeshuka sana magonjwa zaidi ya mawili yanaweza kutokea kwa wakati mmoja, kwa hiyo tuwe makini kulinda afya nzetu na kutumia dawa zinazohitajika .

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1715


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Dalili za ugonjwa wa vericose veini
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa vericose veini Soma Zaidi...

Dalili za malaria
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu kwa kitaalamu anaitwa Anopheles.na anasambazwa na mbu jike pale anapotafuta chakula hasa wakati akiwa na mimba. Mbu hawa hupenda kuishi kwenye mnyasi, madibwi haswa kwenye maji yaliyo simama. Soma Zaidi...

Kupambana na kisukari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na kisukari Soma Zaidi...

KAMA UNASUMBULIWA NA FANGASI
Post hii fupi inakwenda kukujuza juu ya tatizo la fangasi na nini ufanye. Soma Zaidi...

Huduma kwa wanawake wenye mahitaji maalum.
Posti hii inahusu huduma kwa wanawake wenye mahitaji maalum, ni wanawake ambao wana shida ya akili, walionyanyaswa kijinsia, wakimbizi na wote wenye matatizo mbalimbali. Soma Zaidi...

Dalili za kuvimbiwa kwa watoto.
Kuvimbiwa kwa watoto ni shida ya kawaida. Kuvimbiwa kwa watoto mara nyingi huonyeshwa na kinyesi kisicho kawaida au kinyesi ngumu na kavu. Soma Zaidi...

Sababu za maambukizi kwenye nephoni
Posti hii inahusu zaidi sababu za maambukizi kwenye nephroni, ni vitu vinavyosababisha mabukizi kwenye nephroni. Soma Zaidi...

Sababu za maumivu ya uti wa mgongo
Posti hii inahusu zaidi sababu za uti wa mgongo, ni ugonjwa unaotokana na kuwa na maumivu kwenye uti wa mgongo, hasa hasa ugonjwa huu ushambulia watu kuanzia miaka ishilini mpaka kwenye arobaini hivi, zifuatazo ni sababu za maumivu katika uti wa mgongo. Soma Zaidi...

Matatizo yanayosababisha mshtuko wa moyo.
Mshtuko wa moyo hutokea wakati mtiririko wa damu kwa moyo umezuiwa, mara nyingi kwa mkusanyiko wa mafuta, cholesterol na vitu vingine, ambayo huunda plaque katika mishipa inayolisha moyo (mishipa ya moyo). Mtiririko wa damu ulioingiliwa unaweza kuharibu Soma Zaidi...

Dalili za macho makavu.
Posti hii inahusu zaidi njia za kutambua Dalili za macho makavu, kama tulivyotangulia kuona kubwa macho kuwa makavu Usababishwa na sehemu ya kuzalisha maji kwenye jicho kushindwa kufanya kazi na jicho hilo huwa kavu na Dalili zake ni kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Je mtu anaweza kushiriki mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya ukimwi pasipo kuambukizwa?
Naomba kuuliza swaliJe mtu anaweza kushiriki mapenzi na mtu mwenye maambukizi ya ukimwi pasipo kuambukizwa? Soma Zaidi...

Zijue dalili za maambukizi ndani ya sikio na madhara yake
Sikio ni mojawapo ya milango ya fahamu inayotumiwa kwa ajili ya kusikia, Kuna wakati mwingine hushambulia na bakteria na virusi Soma Zaidi...