Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika
Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu.
Masharti ya udhu
Ili udhu wa mtu ukamilike hapana budi kuchunga na kutekeleza masharti yafuatayo kabla ya kuanza kutawadha:
(i)Kuwa na “maji safi” ya kutosha kuweza kutitirika (yasiwe ya kupakaza tu) katika viungo vya udhu vinavyooshwa.
(ii)Kutokuwa na kitu kilichogandamana (kama vile lami, rangi, ulimbo, n.k) kitakachoweza kuzuia maji kufika kwenye ngozi ya viungo vya udhu. Ni lazima mtu aondoe hicho kilichogandamana ndio aanze kutawadha.
(iii)Kutokuwa na uchafu mwingineo au vumbi,la aina yoyote au kitu chochote juu ya viungo vya kutawadhia kitakachobadilisha rangi, harufu au tamu ya maji yatakayotiririka humo. Ni sharti mtu awe msafi kwanza ndipo aanze kutawadha.
(iv)Kuondoa najisi juu ya viungo vya udhu kabla ya kuanza kutawadha.
(v)Kukata kucha ndefu zinazozuia maji kufikia kona za vidole, kabla ya kuanza kutawadha.
Masharti haya haya ndiyo masharti ya kuoga katika kuondoa hadathi ya kati na kati na hadathi kubwa, bali pamoja na hayo,kwa wanawake wenye kusuka, hawana budi kufumua misuko yao isiyoruhusu maji kupenya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 web hosting 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Ni ipi hukumu ya kutoa talaka hali ya kuwa umelazimishwa au ukiwa umerukwa na akili
Endapo mtu atamuacha mke pasi na ridhaa yake yaani amelazimishwa ama amemuwacha wakati amerukwa na akili. Je ni ipo hukumu yake.
Soma Zaidi...Ijuwe swala ya Tawbah na jinsi ya kuiswali
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya sinnah ya tawba.
Soma Zaidi...Kiasi cha mahari kilicho bora kinachofaaa katika uislamu
Uislamu haukuwekabkiwango maalumu cha mahari. Mwanamke anaweza tajabkiasi atakacho. Ila vyema kuzingatia haya wakayi wa kutamka mahari yako.
Soma Zaidi...Yaliyo haramu kwa mtu asiyekuwa na udhu
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ambauo ni haramu kwa mtu asiye na udhu.
Soma Zaidi...