Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za zabibu
1.Zabibu (grapefruit).
Hili ni tunda ambalo lina historia kubwa kwenye maisha ya wanaadamu. Tunda hili linaweza kupatikana maeneo mengi duniani. Zabibu ni moja kati ya matunda yanayotambulika kuwa na mchango mkubwa katika kuboresha Afya ya mwanadamu tka zamani sana.
Zabibu linatambuliwa kuwa ni chanzo kizuri sana cha vitamini na madini kwenye miili yetu. zabibu ni katika matunda ambayo yana vitamini kwa wingi kuliko mengi katika matunda ambayo tunayala. Itambulike kuwa vitamini na madini ni katika virutubisho muhimu vinavyofanya mwili wako kuwa madhubuti na afya njema sikuzote.
Tunda hili pia hitambulika kuwa na uwezo mkubwa wa kusaidia kupunguza uzito wenye madhara mwilini mwako. Itambulike kuwa uzito ukizidi mwilini kuna matatizo mengi ya kiafya unaweza ukayapata kama kupata maradhi ya kisukari na shinikizo la damu. Hivyo tunda hili husaidia katika kupunguza uzito mwilini mwako. Ni vyema ukala tunda hili kabla ya kula chochote.
Tunda hili pia linatambulika kuwa na uwezo wa kusaidia kuweka madhubuti insulini iwe katika hali ya kawaidi. Itambulike kuwa insulin ikisumbua huweza kusababisha ugonjwa wa kisukari. Pia tunda hili husaidia katika kudhibiti afya ya figo. Kwa mfano zabibu hupunguza hatari za kupata maradhi ya figo yanayoitwa kidney stone yaani vijiwe vinavyokaa kwenye figo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula karanga
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula apple/tufaha
Soma Zaidi...FAIDA ZA MATUNDA Makala hii inakwenda kukuletea faida za matunda mbalimbali na mboga upatikanaji wake na faida zake kiafya.
Soma Zaidi...Hivi ni vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo. mwenye vidonda vya tumbo hatakiwi kula vyakula hivi
Soma Zaidi...Kitunguu saumu ni tiba mbadala ya presha yabkushuja. Hakitatui tatizo yaani hakiponyeshi, ila husaidia katika kushusha presha iliyo panda.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula spinach
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za tangawizi
Soma Zaidi...