Zifahamu fibroids (uvimbe kwenye via vya uzazi)

Posti hii inahusu zaidi fibroids au uvimbe kwenye via vya uzazi hasa hasa utokea kwenye tumbo la uzazi ambapo kwa kitaalamu huitwa uterusi, uvimbe huu ulitokea watu wengine huwa hawawezi kutambua Dalili zake mapema kwa hiyo leo tunapaswa kujua Dalili zake

Dalili za fibroids.

1. Kwanza kabisa mama anatokwa na damu nyingi kwa ghafla inawezekana zikawa ni tofauti na damu za siku damu hizo zinaweza kuwepo kwa sababu ya kupasuka kwa uvimbe.

 

2. Kutokwa na damu nyingi wakati wa siku za mwezi na damu hizo kwa mara nyingi huwa ni za mda mrefu na uchukua mda kuweza kuisha zinaweza kufika hata siku saba.

 

3. Maumivu ya nyonga.

Kwa sababu ya kuwepo kwa uvimbe kwa hiyo ukandamiza viungo vya nyonga na kusababisha nyonga kuuma 

 

4. Kuwepo kwa haja ndogo ya mara kwa mara.

Kwa kawaida mkojo utoka kama mtu amekunywa chochote ila kama kuna uvimbe mkojo utoka mwingi na wa mara kwa mara.

 

5. Kuwepo kwa maumivu ya mgongo.

Kwa kawaida mgongo uuma  sana na kusababishwa kwa mgandamizo wa uvimbe kwa sababu uvimbe uweza kugandamiza nevu za kwenda kwenye mgongo.

 

6. Maumivu wakati wa kujamiiana.

Kwa kawaida watu wenye matatizo ya kuwepo kwa uvimbe huwa na maumivu wakati wa kujamiiana.

 

7. Kuwepo kwa upungufu wa damu.

Kwa kawaida dalili kubwa ya mtu mwenye uvimbe ni kutokwa kwa damu na damu ikitoka uwepo wa kupungukiwa kwa kiwango cha damu ni kawaida.

 

8. Maumivu ya kichwa uwapata wenye tatizo la uvimbe, kwa sababu ya kupungua kwa damu na pia maumivu ya kichwa uongezeka.

 

9. Maumivu kwenye miguu.

Hali hiyo utokea kwa sababu ya mgandamizo wa nevu zinazoenda miguuni pia na kuwepo kwa upungufu wa damu kwa hiyo Usababisha maumivu kwenye miguu.

 

10. Kuvimba kwenye sehemu za chini ya tumbo hili ni kwa sababu ya kuwepo kwa uvimbe kwenye via vya uzazi.

 

11. Kupata uzazi wa shida.

Kwa kawaida wenye uvimbe kwenye via vya uzazi wanaweza kuwa wagumba kama tatizo halijagunduliwa mapema pamoja na kupata uzazi wa shida.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/03/Friday - 08:01:30 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1025

Post zifazofanana:-

Vyakula anavyopaswa kutumia mama mjamzito
Posti hii inahusu zaidi vyakula anavyopaswa kutumia mama mjamzito, mama mjamzito ni mama ambaye amebeba kiumbe ndani kwa hiyo anapaswa kutumia vyakula vyenye virutubisho mbalimbali vitakavyomsaidia mtoto kukua vizuri. Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa sita wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Dalili za hatari kwa mtoto aliyezaliwa
Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa mtoto aliyezaliwa, ni dalili ambazo ujitokeza tu mtoto anapozaliwa kwa hiyo dalili hizi zinapaswa kuzuiwa ili zisilete madhara makubwa. Soma Zaidi...

NIMLAUMU NANI (sehemu ya sita)
Post inahusu zaidi hadithi ya NIMLAUMU NANI ambayo ni sehemu ya sita, katika kipengele hiki tunaenda kumwona msichana Amina anapambana na hatimaye anafunga ndoa ya kiserikali na Frank Soma Zaidi...

Kwanini Ni muhimu kusimamisha uislamu katika jamii
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Dalili za kujifungua
Makala hii itakwenda kukufundisha dalili za kujifunguwa, hatuwa za kujifunguwa na kuzalisha, pia utajifunza mabo muhimu kabla na wakatii wa kujifungua. Soma Zaidi...

Elimu Yenye Manufaa
Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa. Soma Zaidi...

Daliliza shinikizo la Chini la damu.
Shinikizo la chini la damu (hypotension) litaonekana kuwa jambo la kujitahidi. Hata hivyo, kwa watu wengi, shinikizo la chini la damu linaweza kusababisha dalili za Kizunguzungu na kuzirai. Katika hali mbaya, shinikizo la chini la damu linawez Soma Zaidi...

Dalilili za kidole tumbo (appendicitis)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa wa Kidole ambao kitaalamu hujulikana Kama Appendicitis. Kidole tumbo husababisha maumivu kwenye tumbo la chini la kulia. Hata hivyo, kwa watu wengi, maumivu huanza karibu na kitovu na kisha kusonga. Kadiri uvi Soma Zaidi...

Dalilili zinazotokea kwenye mrija wa mkojo
Mrija wa mkojo hutoa mkojo nje ya mwili lakini mrija huu unapoziba hufanya utoaji wa mkojo kutoka kwa shida au maumivu Soma Zaidi...

Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu.
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ambao kwa kitaalamu huitwa Dementia ugonjwa huu uwapata wale ambao umri umekwenda lakini kwa wakati mwingine Usababishwa na vitu mbalimbali kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Zijue sehemu za mwili zinazochomwa chanjo.
Posti hii inahusu zaidi sehemu ambazo zinapaswa kudungwa chanjo, hizi ni sehemu zile zilizopendekezwa kwa ajili ya kuchoma chanjo kwa kadiri ya kazi ya chanjo. Soma Zaidi...