Posti hii inahusu zaidi sifa ambazo mtoto mchanga anapaswa kuwa Nazo,ni sifa ambazo lazima zionekane kwa mtoto mchanga pale anapozaliwa na zikikosa ni lazima kuja kuwa mtoto ana matatizo mbalimbali kwa hiyo zifuatazo ni sifa za mtoto mchanga kama ifuatavy
1. Mwonekano mzima wa mtoto.
Kwanza kabisa mtoto anapaswa kuwa na uzito kuanzia mbili na nukta tano mpaka tatu na nukta tano na kwa kawaida urefu wa mtoto ni kuanzia hamsini sentimita, na rangi ya mtoto anapozaliwa ni rangi ya pinkie, kwa hiyo mtoto akiwa na uzito chini ya mbili na nukta tano anakuwa kwenye uangalizi kwa mda na pia akiwa na uzito kuanzia tatu na nukta tano na kuendelea tunasema kwamba ni mtoto aliyezidi kwa uzito kwa hiyo naye huwa kwenye uangalizi maalumu kwa mda na baadae anaweza kuruhusiwa na kuwa kwenye uangalizi wa wazazi.
2.Watoto waliochini ya uzito au juu ya uzito uwa kwenye uangalizi kwa sababu, zifuatazo.
Mwenye uzito mkubwa anaweza kuwa amezoea vyakula vya kutosha kutoka kwa Mama yake akiwa tumboni akizaliwa tu anapaswa kuhudumiwa mapema na kupewa glucose Ili kulinganisha na chakula alichokuwa anakipata akiwa tumboni kwa hiyo akicheleweshwa anaweza kushuka kwa sukari. Na pia mtoto akizaliwa na uzito mdogo anapaswa kuangaliwa kwa sababu ya kupata uzito unaotakiwa kwa kihakikisha kuwa Mama yake anapewa elimu ya kumtunza mtoto mpaka akafikia kuwa na uzito unaotakiwa.
3. Pia mtoto akizaliwa anapaswa kuwa na kitovu kilicho kwenye tumbo na kinatakiwa kukatwa kwa uangalizi unaofaa Ili kuweza kuzuia maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto, pia na Mama anapaswa kupewa elimu kuhusu namna ya kumtunza kitovu cha mtoto wafundishwe kuwa kitovu cha mtoto kinakauka baada ya siku kumi, pia akina Mama wanapaswa kukumbushwa kuwa waachane na tabia ya kuweka vitu visivyofaa kwenye kitovu kwa kufuata mila na desturi zao hali inayosababisha kuwepo kwa tetunus kwenye kitovu kikitunzwa visivyo.
4. Pia kitu kingine ambacho ni sifa ya mtoto ni kulia tu baada ya kuzaliwa hii ikiwa ni ishara ya uhai kwa mtoto,kwa hiyo mtoto asipolia wauguzi na wasaidizi wote wanapaswa kihakikisha mtoto analia kwa kutoa huduma ya kwanza kwa mtoto na walio wengi wanafanyiwa na wanapona na kuendelea kwenye hali ya kawaida
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia mara kwa mara vidonge vya P2,
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kunyonyesha kwa akina Mama, kunyonyesha ni kitendo ambacho Mama utumia maziwa yake na kumlisha mtoto pindi tu anapozaliwa mpaka wakati anapoachishwa titi, kunyonyesha huwa na faida kubwa kwa wote yaani Mama na mtoto, zif
Soma Zaidi...Unataka kujuwa sababu za mjamzito kutokwa na damu, utelezi ama majimaji kwenye uke wake. Na dalili gani zinaashiriwa na majimaji haya
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuziba kwa mrija wa kizazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapian tube, ni sababu ambazo ufanya mirija ya follapian tube kuziba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya HCG katika kupima mimba, HCG maana yake ni human chorionic gonadotropin ni homoni ambayo uonekanekana kwenye mkojo na damu kama mtu ana mimba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Ugonjwa wa kifafa cha mimba ambapo kwa kitaalamu huitwa eclampsia, utokea pale ambapo Mama anapokuwa na degedege wakati wa mimba na baada ya kujiunga.
Soma Zaidi...Kichefuchefu ni moja katika dalili za mimba za mapema, Lucinda je upo uwezekano kwa mwanamke kuwa na ujauzito bila hata ya kuwa na kichefuchefu?
Soma Zaidi...Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa.
Soma Zaidi...