image

Zijue Athari za kuweka vitu ukeni.

Posti hii inahusu zaidi athari za kuweka vitu ukeni, tunajua kwa wakati huu kadri ya kukua kwa sayansi na teknolojia watu wanaendelea kugundua mbinu mbalimbali ili waweze kuwafurahisha wapenzi wao wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Zijue Athari za kuweka vitu ukeni .

1.wanawake walio wengi wanaweka vitu ukeni kama vile  vipipi, mawe, vikokoto, sukari na madawa mengine mengi wakiwa na malengo tofauti wengine wanaweka vitu mbalimbali ili kuweza kuwafurahisha wapenzi wao wakati wa kufanya tendo la ndoa na wengine wanaweka ili kuweza kuongeza uchungu wakati wa kujifungua, pamoja na hayo kuna madhara makubwa kama ifuatavyo.

 

2.Vitu hivyo uharibu kabisa hali ya uke kwa kupunguza pH ambayo iko kwenye uke kwa sababu pH ya kwenye uke ina kiwango chake ambacho ni kati ya 3.8 hadi 4.5 ukiweka vitu kama hivyo unaweza kuipunguza au kuiongeza kwa hiyo na kusababisha kuingia kwa wadudu kwa sababu kazi ya pH ni kuweka uke kwenye hali maalum ili kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali kwa hiyo matumizi ya vitu hivyo uharibifu kabisa hali ya uke.

 

3. Matumizi ya vitu ukeni ni chanzo cha kuwepo kwa magonjwa mbalimbali, kwa sababu vitu vingine vinatolewa kwenye mazingira ya uchafu na maandalizi ya vitu hivyo pengine ni ya kimila mno hali ambayo Usababisha kuwepo kwa Magonjwa kwenye sehemu ya uke, magonjwa mengine ni kama fungusi za ukeni, Maambukizi kwenye mlango wa kizazi, Maambukizi kwenye mfuko wa kizazi na pengine mtu anaweza kupata ugumba kwa sababu ya vitu hivyo na hata kansa mbalimbali zinaweza kujitokeza.

 

4. Madhara wakati wa kujifungua.

Kwa wakati mwingine wanawake wanaweka vitu hivyo na wanafikia wakati wa kujifungua bado vipo na kwa wengine wanadhubutu kuwaamini wale waliowaweka vitu hivyo ndo wawasaidie wakati wa kujifungua hali ambayo mtoto anakuja vibaya na unakuta maarifa wanayo kidogo hali hii Usababisha vifo kwa akina Mama na watoto wao kwa sababu ya matumizi ya vitu visivyoeleweka na kuweza kujiamini.

 

5. Kuchanika na kupasuka wakati wa kujifungua.

Kwa sababu ya matumizi ya vitu hivyo ukeni kuna vingine kweli vinaongeza uchungu, kwa hiyo kuna kipindi akina Mama wanakuwa na uchungu kabla ya mda kwa sababu ya matumizi ya vitu hivyo na wakija hospitalini wanasukuna mtoto kabla njia haijafunguka vizuri kwa sababu ya kuongeza uchungu kwa hiyo wanaposukuma wanapasuka na kutokwa na damu nyingi na kama alijifungulia kwenye sehemu ambayo haina vifaa vya kutosha wanaweza kupata matatizo na hata kupoteza maisha wao na watoto wao.

 

6.Kwa hiyo akina Mama vitu hivyo havina maana yoyote kabisa kwa wale wanaovitumia kwa lengo la kufanya tendo la ndoa lipendeze jua kuwa kuna hatari ya kupata magonjwa na pia kabla ya tendo la ndoa  mjiandae vizuri ili kuweza kufanya tendo la ndoa juwa tamu sio kutumia vitu hivi vya ajabu na kumbuka wewe Mama ukipata matatizo ni wewe kwa mwanaume ni kiasi kidogo kwa hiyo akina Mama jali afya zenu na maisha yenu ni ya muhimu sana.

 

7.Na kwa wale wanaotumia vitu hivi ili kuongeza uchungu na kujifungua mapema sio kweli kwa sababu uchungu ukija ukiwa hospitalini watakusaidia wakunga kwa sababu wenyewe wanajua mda gani utajifungua na kwa wakati kwa hiyo acha kuharakisha mambo acheni short cut kwa sababu kwa kutumia vitu hivi ni kuhatarisha maisha yako na mtoto wako.

 

8.Pia jamii inapaswa kutoa elimu kwa jamii kwa ajili ya kuepukana na mila na desturi ambazo zinahatarishwa maisha ya watu na wanawake wanapaswa kuhudhuria kliniki ili kuweza kupata maelekezo muhimu kwa sababu huko kila kitu kinafundishwa huko, asilimia kubwa ya wanawake wanaokwenda kliniki mda umeenda ndio wanafanya vitu vya hivyo kwa hiyo mama maisha ni ya kwako tunapaswa kuungana kwa pamoja ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto.

            

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/10/Thursday - 11:27:19 am Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2505


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Njia za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha.
Posti inahusu zaidi njia maalum za uzazi wa mpango kwa wanaonyonyesha,Ni njia za uzazi ambazo wanaonyesha wanatumia kwa sababu kuna njia nyingine zikitumiwa na wanaonyonyesha zinaweza kuleta matatizo kwa watoto au kusababisha maziwa kutokuwa na vitamini v Soma Zaidi...

Nguvu za kiume Ni nini?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya nguvu za kiume Soma Zaidi...

Fahamu Ute unaotoka wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi Ute unaotoka wakati wa ujauzito, kwa kawaida wakati wa ujauzito Kuna Ute ambao utoka na ni tofauti na kawaida pale mwanamke akiwa Hana mimba. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa kisukari wakati wa ujauzito.
Posti hii inaelezea ugonjwa wa kisukari wakati mama akiwa mjamzito.na yafuatayo ni Mambo hatari yanayotokea wakati Mama akiwa na ujauzito. Soma Zaidi...

Fahamu Mambo ya hatari yanayosababisha kuzaliwa kabla ya wakati (premature)
Kuzaliwa kabla ya wakati humpa mtoto muda mdogo wa kukua tumboni. Watoto waliozaliwa kabla ya wakati, hasa wale waliozaliwa mapema, mara nyingi huwa na matatizo magumu ya matibabu. Soma Zaidi...

Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya kujifungulia.
Postii inafundisha maandalizi ya mama kwa ajili ya kujifungulia hii Ni muhimu Sana kwa wale ambao hawajawahi kujingua Ni mara yao ya kwanza wanatakiwa kujua na kuelewa vifaa na mahitaji kujifungulia na kwa wale wanaohudhuria clinic huwa wanafundisha. Soma Zaidi...

Madhara ya tumbaku na sigara
Post hii itakwenda kuangalia madhara ya tumbaku na sigara anayoweza kuyapata mvutaji Soma Zaidi...

Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoa
Kutokwa na damu baada ya tendo la ndoabkunaweza kuashiria kuwa kuna majeraha yametokea huwenda ni michubuko ilitokea ndio ikavujisha damu. Lakini kwa nini hali kama hii itokee. Posti hii itakwwnda mujibu swali hili. Soma Zaidi...

Dalili za kuharibika kwa mimba
Katika post hii utajifunza ishara na dalili ninazoonyesha kuwa mimba ipo hatarini kutoka ama inaweza kuwa imeshatoka. Soma Zaidi...

mambo HATARI KWA UJAUZITO (MIMBA) mambo yanayopelekea kujauzito kuwa hatarini kutoka
Tofauti na mambo matano yaliyotajwa hapo juu kuwa yanapelekea ujauzito kutoka, kuna mambo mengine ambayo yanaweza kuuweka ujauzito kuwa hatarini. Soma Zaidi...

Maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada Soma Zaidi...

Dalili za mimba ya watoto mapacha
Makala hii itakwenda kukupa dalili ambazo zinaonyesha kuwa mimba ni ya mapacha. Dalili hizi zitahitajika kuthibitishwa na kipimo cha daktari ili kujuwa kuwa ni kweli. Soma Zaidi...