ZIJUE DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO


image


Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa Mama mjamzito, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama mjamzito, hizi Dalili zisipofanyiwa kazi mapema zinaweza kuleta shida kwa Mama kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua Dalili hizi na kuchukua hatua endapo zitajionyesha.


Dalili za hatari kwa Mama mjamzito 

1. Kutokwa na damu ukeni.

Kutokwa na damu kunaweza kuwa sio dalili mbaya, kwani si jambo la kuogopa na ni hali inayoweza kumtokea mjamzito. Lakini tunatarajia damu hii sio nyingi. Endapo damu hii itaambatana na maumivu makali ya tumbo, ama kizunguzungu ama maumivu makali ya kichwa, ni vyema kufika kituo cha afya. Pia endapo damu hii itakuwa nyingi kiasi cha kuhitaji kujisitiri pia ni vyema kufika kituo cha afya kwa uangalizi.

 

2. Dalili ya hatari nyingine kwa Mama mjamzito ni mtoto kushindwa kucheza tumboni, kwa kawaida uhai wa mtoto akiwa tumboni ni kuhisi kuwa mtoto anacheza pindi mtoto akishindwa kucheza hiyo ni Dalili ya hatari  ,  wakati mwingine ni mabadiliko ya Mama kama vile uchovu na sababu nyingine nyingi, kwa hiyo mama akisikia mtoto amepitisha siku  bila kucheza anapaswa kwenda hospitalini mara moja ili aweze kupata  msaada zaidi.

 

 3. Kuvimba miguu kwa wajawazito.

Na hili ni mojawapo ya Dalili ya hatari kwa Mama , ambapo maji mengi yanayoka kwenye seli yanakuja kwenye tisu na pengine ni kwa sababu ya kupungua kwa protini kwenye mwili na sababu nyingine nyingi kwa hiyo Mama akiona amevimba miguuni anapaswa kwenda hospitalini ili kupata matibabu na maelekezo zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya pia wauguzi wanapaswa kuwaambia wakina Mama kuwa pindi waonapo Dalli hizi wanapaswa kwenda moja kwa moja hospitalini.

 

4.Maumivu akali ya kichwa kwa Mama mjamzito.

Mama mjamzito akipatwa na  maumivu makali ya kichwa anapaswa kujua wazi hali yake ya kuwa ni ya hatari kwa hiyo anapaswa kwenda hospitalini kwa sababu kuumwa sana kichwa kunaweza kusababishwa na presha au mabadiliko yoyote ya mwili ambayo yasipotibiwa kwa wakati yanaweza kuleta kitu kingine kisicho cha kawaida. Kwa hiyo wauguzi na wataalam wengine wa afya wanaswa kuwaambia ukweli kuhusu Dalili hizi za hatari.

 

5. Kwa kawaida tunajua wazi kubwa akina Mama wajawazito wanapaswa kutunzwa vizuri na kuhakikisha kubwa wasipatwa na janga lolote ambalo linaweza kumfanya awe dhaifu kwa hiyo tunapaswa kujua Dalili za hatari na kuwapeleka hospitali mara moja bila kuchelewa na pia wanapaswa kwenda kliniki mara kwa mara ili kuweza kujua maendeleo ya afya zao na pia jamii iliyowazunguka inapaswa kujua Dalili hizi na kuwawaisha hospitalini bila kuchelewa 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    2 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    3 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Hadiythi za alif lela u lela    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri
Post hii inahusu zaidi tiba na huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri. Soma Zaidi...

image Dalili za uchovu wa joto mwilini.
Uchovu wa joto ni hali ambayo dalili zake zinaweza kujumuisha kutokwa na jasho kubwa na mapigo ya haraka, ambayo ni matokeo ya joto la mwili wako. Ni mojawapo ya magonjwa matatu yanayohusiana na joto, huku tumbo la joto likiwa kali zaidi na Kiharusi cha joto kilicho kali zaidi. Soma Zaidi...

image Uzazi wa mpango kwa njia ya kumwaga manii nje.
Posti hii inahusu zaidi uzazi wa mpango kwa njia ya kumwaga shahawa nje, hii ni njia mojawapo kati ya njia za uzazi wa mpango ambapo mwanaume humwaga nje mbegu ili asimpatie Mama mimba. Soma Zaidi...

image Kifuwa kinaniuma katikati kinaambatana nakichwa
Maumivu ya kifuwa yanaweza kutokea baada ya kubeba kitu kizito, ama kupata mashambulizi ya vijidudu vya maradhi. maumivu ya viungo na hata vidonda vya tumbo. Lakini sasa umesha wahi fikiria maumivu ya kifuwa kwa katikati? Soma Zaidi...

image Njia za kukabiliana na presha ya kushuka
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kushuka Soma Zaidi...

image Huduma ya kwanza kwa mwenye jeraha linalotoa damu
Posti inahusu huduma ya kwanza kwa mwenye jeraha linalotoa damu.huduma ya kwanza Ni kumsaidia mtu alie pata jeraha au ajali kabla hajamwona dactari au kufika hospitalinia. Soma Zaidi...

image Mambo ya kuzingatia unapokuwa unatoa huduma ya kwanza
Huduma ya kwanza ni huduma inayotolewa kwa mtu yeyote aliyepata ajali au mgonjwa yeyote kabla hajapelekwa hospitalini Soma Zaidi...

image Mambo ambayo yanaweza kuongeza hatari ya Ugonjwa wa Homa ya ini yenye sumu.
Posti hii inazungumzia zaidi kuhusiana na Homa ya ini yenye sumu ni kuvimba kwa ini lako kutokana na kuguswa na vitu fulani ambavyo umeathiriwa navyo. Homa ya ini yenye sumu inaweza kusababishwa na pombe, kemikali, madawa ya kulevya au virutubisho vya lishe. Katika baadhi ya matukio, homa ya ini yenye sumu hukua ndani ya saa au siku baada ya kuathiriwa na sumu.Katika hali nyingine, inaweza kuchukua miezi ya matumizi ya kawaida kabla ya dalili na dalili za homa ya ini yenye sumu kuonekana. Lakini homa ya ini yenye sumu inaweza kuharibu ini kabisa, na kusababisha kovu lisiloweza kutenduliwa la tishu za ini (cirrhosis) na katika visa vingine ini kushindwa kufanya kazi Soma Zaidi...

image Upungufu wa protin
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa protini Soma Zaidi...

image Madhara ya Tiba homoni kwa wagonjwa wa saratani
Posti hii inahusu zaidi madhara ya Tiba homoni, ni madhara- ambayo utokea kwa mgonjwa anayetumia homoni kama Tiba kwenye kutibu saratani. Soma Zaidi...