Zijue kazi za madini ya chuma mwilini
Posti hii inahusu zaidi kazi za madini ya chuma mwilini,Ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini na pia utokana na vyakula mbalimbali ambavyo upatikana kwenye wanyama na mimea. Zifuatazo ni kazi za madini ya chuma.
1. Madini ya chuma usaidia kusafilisha gasi ya oxygeni kutoka sehemu mbalimbali za mwili na kwenda sehemu nyingine za mwili ambapo oxgeni inahitajika.
2. Madini ya chuma usaidia katika kazi za haemoglobini ambayo ubeba gasi ya oxygeni kutoka kwenye mapafu kwenda sehemu mbalimbali za mwili na pia haemoglobini hiyo ubeba carbon dioxide kutoka kutoka kwenye sehemu mbalimbali za mwili mpaka kwenye mapafu kwa ajili ya kutafuta oxgeni kwa hiyo kazi ya kusafilisha hizi gasi mbili usaidia na madini ya chuma.
3. Madini ya chuma usaidia kusafilisha damu ya oxgeni kwenye misuli ambapo kitendo hiki kwa kitaalamu huitwa myoglobin ambayo ni sehemu ya protein kwenye misuli,kwa hiyo myoglobini asili yake ni protini ambayo inaweza kusafilisha gasi ya oksijeni kwenye misuli, hii kazi usaidiwa na madini ya chuma.
4. Madini ya chuma yanasaidia katika upumuaji kwa sababu ya kuwepo kwa cytochrome ambayo ni sehemu ya madini ya chuma, cytochrome usaidia katika kusafirisha hewa wakati wa kupumua, kwa sababu cytochrome imetengenezwa na madini ya chuma, ndo maana tunaaweza kusema kuwa madini ya chuma usaidia katika upumuaji.
5. Madini ya chuma usaidia katika kuzalisha protini hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa baadhi ya vitu ambavyo vimetengenezwa kwa madini ya chuma ambayo usaidia kutengeneza protein kwa kitaalamu huitwa xanthine oxidase - enzyme ambayo ni sehemu ya madini ya chuma.
6.Madini ya chuma ni sehemu ya enzyme, tunajua kuwa enzyme ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili, kwa hiyo madini ya chuma ni sehemu ya enzyme ambazo kwa kitaalamu huitwa peroxide, catalase na enzyme nyingine nyingi ambazo ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.
7.Madini ya chuma usaidia katika kuzalisha homoni ambazo utumika kufanya kazi mbalimbali kwenye mwili kama vile kuhakikisha kiwango Cha sukari kipo sawa kwenye mwili, kutengeneza protini kwenye mwili, kukua na kuzaliana na kazi zote mwilini ambazo utengenezwa na homoni.
Wapi tunaaweza kupata madini ya chuma?
1. Madini ya chuma tunaaweza kuyapata katika sehemu mbalimbali kama vile nyama, samaki, vyakula kama vile njegere, maharage,soya beans, njugu Mawe na vyakula vyote ambavyo ni jamii ya kuunde hivi vyote tunaviita kwa kitaalamu heme - iron .Kuna vyakula vingine ambavyo tunaviita non- heme iron kama vile vyakula vinavyopatikans kwenye mboga za majani, mayai na maziwa.
Nini madhara ya kukosa madini ya chuma mwilini.
1. Madini ya chuma yakikosa mwilini mtu anaweza kupata upungufu wa damu mwilini ambapo kwa kitaalamu huitwa Anaemia, ambayo upelekea mwili kuchoka, kizunguzungu, kichwa kuuma na mwili una kiss kinga mwilini kwa hiyo unaweza kupata magonjwa nyemelezi .
2. Madini ya chuma yakikosa mwilini mtu anaweza kupata ugonjwa wa kuvimba matezi ambao kwa kitaamu huitwa goitre yaani ni kuvimba kwenye shingo ambapo ugonjwa huu usababisha madhara makubwa kwa watu wengi, kwa hiyo tunapaswa kula vyakula vyenye wingi wa madini ya chuma usaidia sana katika shughuli mbalimbali kwenye mwili wa binadamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 ai web app 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Vyakula vya wanga
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za vyakula vya wanga na umuhimu wake mwilini
Soma Zaidi...Asili ya Madini ya shaba
Posti hii inahusu zaidi asili ya madini ya Shaba, ni sehemu ambapo madini ya Shaba yanaweza kupatikana ni katika mimea na wanyama
Soma Zaidi...Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake
Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake
Soma Zaidi...Madhara ya vyakula vya kisasa
Posti hii inahusu zaidi madhara ya kuwepo kwa vyakula vya kisasa, vyakula vya kisasa ni vyakula vya madukani ambavyo vimetengenezwa na kuwekwa kwenye maduka
Soma Zaidi...Madhara ya mafuta mengi mwilimi
Post hii itakufundisha madhara ya kuwa na mafuta mengi mwilimi
Soma Zaidi...