Zijue sababu za chakula kushindwa kumengenywa kwenye tumbo.

Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali za chakula kushindwa kumengenywa kwenye tumbo,ni sababu mbalimbali hasa za kiafya kama tutakavyoona hapo mbeleni

Sababu za kutomengenywa chakula tumboni.

1. Kuwepo kwa vidonda vya tumbo.

Kama tunavyofahamu kwamba vidonda vya tumbo ni kizuizi kikubwa cha chakula kushindwa kumengenywa kwa hiyo kama mtu ana matatizo ya vidonda vya tumbo na hajapima ila anaona kwamba chakula hakimengenywi ni vizuri kabisa kuchukua matibabu ili kuangalia tatizo zaidi.

 

 

 

 

2. Kuwepo kwa uvimbe tumboni.

Na hili ni tatizo kubwa zaidi ambalo usababisha chakula kutomengenywa kwa sababu kuna watu wengi wamepatwa na tatizo hili la kuwepo kwa uvimbe na bila kujua na dalili mojawapo ni kujaribu kuwepo kwa shida katika mmeng'enyo wa chakula kwa hiyo ni vizuri kabisa kupima ili kuona chanzo ni nini?

 

 

 

 

3. Kuwepo kwa mawe kwenye figo.

Hili nalo ni tatizo la nawe kwenye figo ni ugonjwa ambao uwapata watu mbalimbali kwa sababu mbalimbali kwa hiyo kama tatizo hili halijagunduliwa na kuna Dalili ya chakula kushindwa kumengenywa vipimo ni lazima.

 

 

 

 

4. Kuvimba kwa kongosho.

Kama kuna matatizo kwenye kongosho nayo usababisha chakula kushindwa kumengenywa tumboni.

 

 

 

 

5. Saratani kwenye utumbo.

Nalo ni mojawapo ya tatizo la kusababisha chakula kushindwa kumengenywa kwa sababu baadhi ya mifumo kwenye mmeng'enyo uaribiwa.

 

 

 

 

6. Kuziba kwa utumbo.

Nalo ni mojawapo ya tatizo ambalo usababisha chakula kushindwa kumengenywa kwa sababu mifumo mbalimbali kwenye utumbo ushindwa kufanya kazi na kusababisha chakula kushindwa kumengenywa.

 

 

 

7. Kupungua kwa mzunguko wa damu.

Kuna wakati mwingine kuna tatizo la kupungua kwa tatizo la mzunguko wa damu hivyo usababisha. Chakula kushindwa kumengenywa.

 

 

 

8. Ukosefu wa choo na Bawasili.

Nacho ni mojawapo ya sababu ya kushinda kumengenywa kwa chakula kwa sababu chakula kikishindwa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kutoa choo ni vizuri kabisa kupima uenda ni kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo katika kumengenywa kwa chakula.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/16/Saturday - 01:47:07 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1103


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-