Maumivu ya Uke na Uume baada ya tendo la ndoa na wakati wa tendo la ndoa

Utajifunza sababu za maumivu ya uume na uke wakati wa tendo la ndoa na baada ya tendo la ndoa na matibabu yake.

Maumivu ya Uke na Uume baada ya tendo la ndoa na wakati wa tendo la ndoa

MAUMIVU YA UKE AU UUME BAADA YA TENDO LA NDOA NA WAKATI WA TENDO LA NDOA.



Tendo la ndoa ni katika vilele vya furaha. Lakini furaha hii wakati mwingine hupelekea machungu. Usaliti, maradhi na umasikini huwenda ikawa sababu ya machungu katika ndoa na kusababisha kutofurahia tendo landoa. Wapo watu wanasumbuliwa na maumivu ya viungo vyao vya siri baada ya kushiriki tendo la ndoa. Hapa nazungumzia uke na uume. Maumivu haya ni ngumu kuelezea ila wakati mwingine utahisi kama unaunguwa ivi, ama maumivu tu kwenye uke na uume kwa ujumla.



Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa tendo la ndoa na hata baada. Je na wewe ni mwenye kusumbuliwa na maumivu haya. Je uume wako ama uke wako unauma unaposhiriki tendo la ndoa, ama baada ya kumaliza kushiriki?. makala hii ni kwa ajili yako, tutaona sababu zinazopelekea maumivu kwenye uke ama uume wakati wa kushiriki tendo la ndoa na baada.



Sababu za maumivu ya uke au uume
1.Kutokuwepo na vilainishi vya kutosheleza kwenye uke.
Tendo la ndoa hufanyika kati ya msuguano wa uume na uke. Katika hali ya kawaida pindi mwanamke anaposhawishika kufanya tendo la ndoa, homoni za mwili wake huzalisha majimaji kwa ajili ya kulainisha uke ili kuruhisu uume kuingia vyema na kutoka. Msuguano huu ndio huzalisha ladha ya tendo. Sasa ikiwa mwanamke hakupandisha hisia vyema homoni hizi hazitolewi, na matokeo yake uke hubakia katika ukavu wake. Sasa msuguano huu utakaofanyka pindi uke ukiwa mkavu unaweza kupelekea maumivu ya uke na ume wakati wa tendo la ndoa na baada ya tendo la ndo.



Matibabu ya tatizo hili:
Mwanamke hakikisha unapandishwa hisia vyema na uke una majimaji kisha ruhusu kuingiliwa. Na mwanaume usimuingilie mwenzio kama uke hauna majimaji ya kutosha. Pia kuna wanawake wengine wana matatizo ya homoni, hivyo hawazalishi majimaji ya kutosha kwenye uke wao. Hawa wanaweza kusaidiwa kwa kupewa matibabu ya kuboresha mfumo wa homoni. Pia ni bora kutumia vilainishi maalumu kama mwanamke hazalishimajimaji ya kutosha ukeni.



2.Ukubwa wa uume na urefu wake ukilinganisha na maumbile ya uke na mwanamke kwa ujumla.
Uke siku zote unasifa ya kuendana na ukubwa wa uume, yaani unatanuka kulingana na ukubwa wa uume na husinyaa kulingana na udogo wa uume. Hutokea wakati mwingine uume ukawa mkubwa kupitiliza, hii ikasababisha msuguano ukawa mkubwa sana na hivyo kusababisha maumivu wakati wa tendo na baada.



Matibabu ya tatizo:
Kama uume ni mnene sana, hakikisha unatumia vilainishi vyema, na kuwa makini uke ukipoteza majimaji chomoa kwanza. Pia fika hospitali kuangaliwa urefu wa uume kama mwenzio analalamika sana mauivu ya tumbo baada ya tendo na wakati wa tendo.



3.Namna ambavyo tendo limefanyika
Kuna wakati mwingine wenza kufanya tendo hovyohovyo. Mara mkao huu mara afanye hivi nara vile. Haya wakati mwingine huathiri viungo hivi na kuasababisha maumivu ya yke na uume. Pia haya hutokea kama tendo linafanyika kwa kasi sana, yaani kasi ya kupushi nje ndani ikawa ni kubwa sana.



Matibabu:
Hakiisha tendo linafanyika kipolepole na kwa ufanisi. Angalia mikao mnayotumia kama haina shida ama haiwezi kubana uume ama uke.



4.Kuwa na aleji na manii.
Hii hutokea kwa baadhi ya watu, wanaume ama wanawake. Yaani yeye akipatwa na manii kwenye kiungo chake yaani uume ama uke wanapatwa na maumivu. Aleji hii hutokea mara chache ila inawezekana. Aleji hii pia inaweza kutokea kutokana na vifaa vinavyotumika katika tendo. Kwa mfano kondom,. kuna wengine wao mwili wake ukigusa kondomu wanapata maumivu



Matibabu
Ongea na daktari wako, kama tatizo ni aleji atakupatia dawa za kuzuia aleji.



5.Kuwa na ugonjwa wa UTI
Sambamba na kuwa ugonjwa wa UTI unaweza kuathiri mfumo wa mkoji kwa mfano maumivu wakati wa kukojoa. Lakini kwa wengine shida inaweza kutokea wakti wa kushiriki tendo la ndoa, na baada ya kumaliza. Ni maumivu kwenda mbele. Uke ama uume utauona unauma, ama kama unaunguwa.



Matibabu
Pata vipimo ikithibitika ni UTI utapatiwa matibabu na utapona mapema tu. Zipo dawa nyingi za UTI na za uhakika katika kupona.



6.Kuwa na maradhi ya ngono
Maradhi mengi yanayoambukizwa kwa njia ya ngono yanapelekea kupata maumivi. Ila mangine yamezidi. Kwa mfano gonoria, chlamydia, na mapele maple ya nayoitwa herpes. Maradhi haya yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada.



Matibabu
Hakikisha unatibiwa gonoria na maradhi mengine ya ngono.



7.Kuwa na maradhi kwenye mirija ya mkojo ugonjwa unaojulikana kama urethritis.
Haya ni maradhi yanayosababishwa na bakteria ama virusi na huathiri mirija wa mkojo unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu kuja nje. Mrija huu unaitwa urethra. Sasa kama umeathiriwa na bakteria ama virusi hali hii inaweza kupelekea maumivu ya uke ama uume wakati wa tendo la ndoa na baada ya tendo la ndoa.



8.Fangasi
Fangasi wanaweza kuathiri maeneo mengi mwilini, kuanzia kichwa mapaka mapaja hadi kufikia sehemu za siri. Fangasi hawa wakiwa kwenye uke na uume huwa ni tatizo zaidi. Mara nyingi sana maumivu haya ya uke ama uume husababishwa na fangasi.



Sabau nyingine
1.Homoni kutokuwa sawa
2.Kuathirika kwa tezi dume
3.Kuwa na uvimbe
4.Kuwa na majeraha
5.Kama mwanaume hajatahiriwa
6.Kama mwanamke amekeketwa
7.Kama tendo limefanyika kwa muda mrefu zaidi ya dakika 30





                   





Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 506


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-