picha

NAMNA YA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME, NA VYAKULA VYA KUBORESHA NGUVU ZA KIUME

Njoo ujifunze vyakula vya kuboresha mbegu za kiume na nguvu za kiume.

NAMNA YA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME, NA VYAKULA VYA KUBORESHA NGUVU ZA KIUME

VYAKULA VYA KUBORESHA MBEGU ZA KIUME




Ugumba si kwa wanawake tu, wapo hata wanaume wanatatizo hili. Lakini kutokubebesha mimba ama kubeba mimba pekee haimaanishi kuwa wewe ni mgumba. Mwanaume kumbebesha mimba mwanamke kunategemea mambo mengi kutoka kwa mwanaume mwenyewe na kwa mwanamke mwenyewe. Katika makala hii nitazungumzia kipengele kimoja tu nacho ni tatizo la kutokuwa na mbegu bora za kiume.



Mwnaume anapokojoa bao moja anatoa mbegu zaidi ya milioni 300. katika mbegu hizo ni moja tu ndiyo intakayofanikiwa kitungisha mimba. Mamimioni ya mbegu haya yanakufa bila hata ya kulifikia yai, kutokana na udhaifu wao, kutoweza kuogelea vyema, ukali wa tindikali katika tumbo la mwanamke n.k. sasa ili mwanaume aweze kubebesha ujauzito anatakiwa atoe mbegu bora na imara zinazoweza kuishi ndani ya tumbo la mimba kwa muda mrefu.



Inatokea baadhi ya wanaume mbegu zao zinakuwa sio imara kutosheleza. Hii inakuwa ni ngumu kubebesha ujauzito. Lakini kumbuka kama mambo mengine yakiwa sawa hata mwenye mbegu dhaifu inaweza kubebesha mimba endapo itakuwa ni siku sahihi ya kukutana na yai, hazitachukuwa muda kukutana na yai ama zilitolewa nyingi.



Sasa ikiwa tatizo ni hili la mbegu ni dhaifu, je nitawezaje kuboresha mbegu zangu? Yes ni swali zuri sana, na inapasa hasa kulijuwa jibu lake. Mbegu utaweza kuziporesha kwa kubadilisha mlo ama kutumia dawa ama njia nyinginezo. Miongoni mwa njia hizo ni:-



Njia za kuboresha mbegu za kiume.
1.Badili mlo wako.
Muonekano wako leo ni sawa na chakula unachokila. Ladha na ubora wa manii na mbegu za kiume pia hutegemeana na unachokila. Kama unataka kuboresha mbegu za kiume kwanza anza na kubadili mlo wako. Jitahidi kula vyakula vifuatavyo:-



A.Vitamini B-12
Vitamini hivi unaweza kuvipata kwenye nyama, samaki na maziwa. Vitamini hivi husaidia sana katika afya ya mbegu za kiume.



B.Vitamini C
Hivi unaweza kuvipata kwenye machungwa, viaz mbatatai, nyanya, apinach na kwenye matunda yenye uchachu na mapapai na mananasi. Vitamini C pia ni muhumu kwa afya ya mfumo wa kinga



C.Kula vyakula jamii ya korosho na karanga



D.Kula vyakula vyenye lycopene. Vyakula hivi kuwa na rangi nyekundu kama tikiti na nyanya



E.Kula vyakula vyenye madini ya zinc kwa wingi. Unaweza kupata madini haya kwenye nyama, samaki wa baharini kwenye magobeta jamii ya kaa, mimea jamii ya kunde, kula mbegu kama mbegu za maboga na nyingine, maziwa, mayai, jamii ya korosho, baadhi ya mboga za majani kama maharagwe ya kijani na nafaka nzima.



2.Fanya mazoezi ya mara kwa mara.
Mazoezi si kwa ajuli ya hili tu bali pia ni kwa ajili ya kuboresha afya kwa ujumla. Si lazima ufanye mazoezi mareefu, hapana kwa uchache pia inatosha.



3.Punguza kuvaa nguo za ndani zenye joto.
Afya ya mbegu za kiume inategemea pia joto la mwili wako. Hakikisha korodani unazipa hewa ya kutosha. Usivae nguo za kubana nyingi kama chupi, si salama kwa wanaume. Boxa kama haibani sana inatosha.



4.Punguza unywaji wa pombe, na soda kama unakunywa kwa kiasi kikubwa.





                   



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 9935

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 web hosting    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Jinsi ya kushusha homoni za kiume.

Posti hii inahusu zaidi njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kupunguza homoni za kiume kwa akina dada.

Soma Zaidi...
Fahamu madhara ya Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke PID

Posti hii inazungumzia kuhusiana na mathara yanayosababisha Ugonjwa wa Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke

Soma Zaidi...
Ijue kazi ya homoni ya HCG wakati wa kupima mimba.

Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya HCG katika kupima mimba, HCG maana yake ni human chorionic gonadotropin ni homoni ambayo uonekanekana kwenye mkojo na damu kama mtu ana mimba.

Soma Zaidi...
Mwezi juzi niliingia tarhe 21 ila mwez uloisha nmeingia tarh 25 maana mzunguko wangu umekuwa mrefu nikahs naujauzito kumbe mzunguko umebadilika hapo tatz n nn

Posti hii utakwenda kutoa sababu kuu za kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi. Kama na wewe numiongini mwaka endelea kusoma

Soma Zaidi...
Sababu za mimba kutoka

Post hii inahusu zaidi sababu za mimba kutoka, hili ni tatizo ambalo linawakumba wanawake wengi ambapo mimba utoka kabla ya kumfikisha mda wake, kwa kawaida Ili kawaida mimba nyingi utoka zikiwa na miezi chini ya Saba au wengine wanaweza kusema kwamba mim

Soma Zaidi...
Madhara ya mwili kushindwa kutengeneza projestron ya kutosha

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo mtu anaweza kupata ikiwa mwili utaeweza kutengeneza progesterone ya kutosha.

Soma Zaidi...
Samahani naomba kuhuliza je unaweza kutokwa na maji maji ambayoa ayana rangi Wala harufu Ni dalili gani kwa mimba ya mwezi mmoja

ukiwa na ujauzito unaweza kuona mabadiliko mengi katika mwili wako yakiwemo kutokwa na majimaji. je majimaji haya yana dalili gani kwenye ujauzito?

Soma Zaidi...
Sababu za kuwepo fangasi ukeni

Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa Ugonjwa wa fangasi,ni sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha fangasi.

Soma Zaidi...
Uhusiano uliopo kati ya Mama Mjamzito na kibofu cha mkojo.

Posti hii inahusu zaidi uhusiano uliopo kati ya Mama Mjamzito na kibofu cha mkojo.ni mwingiliano unaokuwepo ambao usababisha Mama kukojoa sana wakati wa ujauzito.

Soma Zaidi...