Matatizo yahusianayo na nguvu za kume na kukosa hamu ya tendo la ndoa kwahuweza kuchangiwa sana na mpangilio mbovu wa vyakula pamoja na saikolojia ya mtu.
Matatizo yahusianayo na nguvu za kume na kukosa hamu ya tendo la ndoa kwahuweza kuchangiwa sana na mpangilio mbovu wa vyakula pamoja na saikolojia ya mtu. Ni vyema kujiweka tayari kisaikolojia kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Kwa upande wa vyakula ni vyema kuchaguwa vyakula vilivyo salama kwa afya. Vyakula vyenye mafuta kupitiliza vinaweza kuleta athari mbaya kwa afya ya nguvu za kiume. Katika makala hii nitakuletea vyakula vitano ambavyo husaidia katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa:
Vyakula hivyo ni:
1. Vyakula vyenye arginine . Vyakula hivi vina ni vyakula vyenye chembechembe itambulikayo kama arginine. Ndani ya miili yetu arginine huweza kubadilishwa kuwa oxide ya nitric (nitric oxide). Arginine ni chembechembe za asidi ya amono (amino acid). vyakula vyenvye arginine ni kama maharage ya soya, mbegu za maboga, karanga, korosho, samaki, nyama, kuku na samaki.
Arginine imafaida nyingi sana mwilini. Chembechembe hii huweza kutibu tatizo la kusinyaa kwa uume kabla ya kumwaga, ama kusinyaa mapema, ama kugoma kabisa kusiama. Kama tatizo hili linahusiana na mishipa ya damua kama kuziba kwa mishiba ya damu basi arginine ni msaada mkubwa. Pia husaidia kuimarisha afya kwa wenye kisukari na wenye maradhi ya moyo hususani yanayohusiana na mishipa ya damu kama kujaa mafuta ama kuziba.
2. Vyakula vyenye phytochemical: vyakula hivi ni kama maepo (apples),mboga za apricots, broccoli, Brussels sprouts, kabichi (cabbage), karoto (carrots), cauliflower, kitunguu thaumu (garlic), mimea jamii ya kunde (legumes), kitunguu maji (onion), pilipili kali (red peppers), maharage ya soya (soybeans), viazi vitamu (sweet potatoes), na nyanya (tomatoes).
3. Vyakula vya fati iliyo salama kwa afya ya moyo. Afya ya moyo huchukuwa nafasi kubwa katika tendo la ndoa. Uzima wa moyo huweza kufanya damu kutembea vyama maeneo yote ya mwili hususani maeneo yanayohusika katika tendo la ndoa.
Miongoni mwa vyakula hivi ni palachichi. Ndani ya palachichi kuna fat, vitamini B6 asidi ya folik (folic acid) kwa hamoja hizi husaidia kuongeza nishati mwilini na kuimarisha afya katika kushiriki tendo la ndoa. Vyakula vingine ni kama aina flani ya samaki, mayai, mbegu za chia, chokleti, bidhaa za maziwa kama siagi n.k
4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe hii ni kuwa arginine. Faida za arginine tumeshaziona hapo juu. Chemikali hizi pia husaidia katika kuufanya mwili uweze kuwa shwari (relax) kama vile viagra inavyofanya kazi.
Miongoni mwa vyakula hivi ni tikitimaji. Tunda hili lina citrulline kwa wingi sana tofauti na matunda mengi. Vyakula vingine ni kama maboga, matang n.k. citrulline pia husaidia katika kutanua misuli na kuboresha mishipa ya damu kufanya kazi vyema hivyo ni nzuri kwa wanaofanya mazoezi. Kwa upande wa afya ya tendo la ndoa husaidia katika kupeleka damu kwenye maeneo nyeti.
5. Vyakula vyenye Indole-3-carbinol: hii husaidia katika kuboresha homoni hasa kwa wanaume. Huweza kupatikana kwenye mboga za majani kama kabichi, broccoli na mboga nyinginezo. Tofauti na faida hizi pia huweza kusaidia katika kuzuia na kupunguza athari za saratani ya matiti, tumbo, na nyinginezo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Njoo ujifunze vyakula vya kuboresha mbegu za kiume na nguvu za kiume.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14
Soma Zaidi...Maumivu ya matiti ni malalamiko ya kawaida miongoni mwa wanawake yanaweza kujumuisha uchungu wa matiti, maumivu makali ya kuungua au kubana kwenye tishu zako za matiti. Maumivu yanaweza kuwa ya mara kwa mara au yanaweza kutokea mara kwa mara tu. Maumiv
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo chini ya umri wa miaka mitano ili kuweza kuweka afya yake kwenye njia safi.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za kujaa tmgesi tumbon
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Ugonjwa wa kifafa cha mimba ambapo kwa kitaalamu huitwa eclampsia, utokea pale ambapo Mama anapokuwa na degedege wakati wa mimba na baada ya kujiunga.
Soma Zaidi...Post hii itakujulishs kwa namna gani mwanaune anaweza kupata fangasi kwenye uume wake
Soma Zaidi...Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi, tunajua kabisa wakati wa hedhi damu inapaswa kuwa nyepesi na ya kawaida ila kuna wakati mwingine inakuwa na mabonge zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi.
Soma Zaidi...