DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo.
DALILI ZA HIV ZA MWANZO NA DALILI ZA UKIMWI ZA MWANZO
Kama ilivyo magonjwa mengi hupitia hatua kadha kadha na kuonyesha dalili kadha katika hatua hizo. Basi HIV nayo ina hatua zake mpaka kuwa UKIMWI.
DALILI ZA MWANZO ZA HIV AMA UKIMW
Dalili hizi huanza kuonekana kuanzia wiki mbili mpaka nne na wakati mwingine mpaka sita toka kuingia mwilini. Mara chache sana huweza kuonekana mwanzoni mwa wiki ya kwanza. Katika kipindi hiki mtu anaweza kuona dalili zifuatazo:
1.kufimba kwa tezi za kwenye makwapa, mapaja na shingo
2.Homa
3.Uchovu
4.Kuharisha
5.Kupungua uzito
6.Kikohozi
7.Pumzi kutoka kidogodogo
8.Mafua
Dalili hizi pia zinaweza kuhusiana na maradhi mengine, hivyo inaweza kuwa vigumu kujuwa nini chanzo zaidi. Wengi katika wanaopata HIV wametaja kuwa kuvimba kwa tezi ndio dalili pekee walioweza kuopata mwanzoni mwa kuathirika kwao. Wengine wanataja mafua kuwa ndio dalili yao ya kwanza.
Baada ya kipindi hiki kupita mgonjwa hatapata dalili yeyote ile. Hiki ni kipindi hatari sana kwani mtu hataweza kujijua kama ameathirika. Kipindi hiki kinaweza kudumi mpaka miaka 10. katika kipindi hiki virusi vinaendelea kuathiri seli za mwili. Baada ya mwili kuwa umeathirika sana na kudhoofu mtu ataanza kupata dalili za UKIMWI.
DALILI ZA UKIMWI
1.kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku
2.Kupata homa za mara kwa mara na kuhisi baridi
3.Kikohozi
4.Kushinwa kupumua vyema
5.Madoa madoa kwenye ulimi na mdomoni
6.Maumivu ya kichwa
7.Uchovu usiokuwa na sababu na usioisha
8.Kutokuona vyema
9.Kupungua uzito
10.Mapele na ukurutu kwenye ngozi
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
AINA ZA MINYOO Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu ambao kwa kitaalamu huitwa Dementia ugonjwa huu uwapata wale ambao umri umekwenda lakini kwa wakati mwingine Usababishwa na vitu mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na tatizo la Kurithi ambapo Damu inatoka kwa muda mrefu wakati au baada ya jeraha bila kuganda.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na dadili na sababu zinazopelekea Ugonjwa wa ulemavu wa ubongo na mfumo wa fahamu ambao kitaalamu hujulikana Kama multiple sclerosis.
Soma Zaidi...Hili ni swali lililowahi kuulizwa na moja ya wasomaji wetu
Soma Zaidi...Kisukari cha Aina ya 2, ambacho wakati mmoja kilijulikana kama Kisukari cha watu wazima au kisichotegemea insulini, ni ugonjwa sugu unaoathiri jinsi mwili wako unavyobadilisha sukari (glucose), chanzo muhimu cha nishati ya mwili wako.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na kujikinga au kuzuia virusi vya ukimwi.
Soma Zaidi...Post hii inahusu Zaidi aina za ajali kwenye kifua,pamoja na kifua kuwa na sehemu mbalimbali na pia na ajali ambazo utokea Huwa za aina mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...