Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14
DALIILI YA MIMBA KATIKA WIKI YA KWANZA NA PILI (SIKU 7 MPAKA 14)1.Kuendelea kwa joto la mwili. Kama ulikuwa makini na siku ambayo joto la mwili wako lilikuwa kubwa, kama ulishiriki tendo siku moja ama mbili kabla ama siku ile, basi endapo joto la mwili litakuwa endelevu hii huashiria huwenda ulibeba ujauzito. Kwa nini, ni kwa sababu joto la mwili hutokea baada ya mabadiliko ndani ya mwili hususani homoni mpya huzaliwa kwa ajili ya kuandaa ukuaji wa ujauzito. Mabadiliko haya ya joto yasifananishwe na joto la homa.
2.Katika wiki hii ya kwanza unaweza kuona mabadiliko ya majimaji kwenye uke. Majimaji yaliyokuwa siku za nyuma kidongo yanaweza kuanza kuchukuwa sura ya mfanano wa majimaji meupe ya yai lililovunjwa. Halikadhalika matarajio ni kuwa uke unatakiwa urudi katika hali ya ukavu baada ya kupita siku hatari. Lakini kama ujauzito ulitungwa uke hautarudi katika hali yake ya kawaida ya ukavu hivyo huanza kuzalisha majimaji kwa wingi. Mabadiliko haya si rahisi kuyaona ila endapo utakuwa manini zaidi unaweza kugundua.
3.Kutokwa na damu kidogo (implantation bleeding). damu hii inaweza kutokea mwishoni mwa wiki ya kwanza ama katikati ya wiki ya pili. Damu hii ni kidogo na inaweza kuwa ni matone kadhaa. Haifanani na damu ya hedhi na wala haitoki na maumivu. Damu hii si endelevu inaweza kutoka kwa muda mchache na kukata. Mwanamke anaweza kuona nguo yake ya ndani inamadoa ya damu. Kwa damu hii mwanamke hatahitai kuvaa pedi.
4.Maumivu ya kichwa ama kichwa kuwa chepesi. Hali hii inaweza kuandamana na kizunguzungu. Hali hii si lazima kuipata, hata hivyo wanawake wengine wanaipata ila hawafikirii kuwa ni tatizo kwani hutokea na kuondoka bila ya kuathiri mwili kwa muda mrefu. Hapa anaweza kuona ni hali ya kawaida kama hatatilia maanani mabadiliko haya.
Kumbuka dalili hizo tajwa hapo juu ni ngumu kuziona mpaka uwe makini sana kwani zinaweza kuathiriwa na hali nyingine za kiafya. Kwa mfano joto la mwili linaweza kusababishwa na mambo mengi kama maradhi, uchovu na stress. Majimaji ya ukeni yanaweza kuongezeka kwa sababu ya njia za uzazi wa mpango ama mabadiliko ya homoni.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa yanaweza kuwa ni dalili ya maradhi fulani, ama shida kwenye mfumo w uzazi. PID na UTI hutuhumiwa kuwa ni katika sababu hizo. Ila zipo nyingine nyingi tu. Kama ina hali hii vyema ukafika kituo cha afya
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili za uvimbe kwenye kizazi,hizi ni Dalili ambazo ujitokeza kwa akina mama ambao wana uvimbe kwenye kizazi kwa hiyo endapo mama ameona Dalili kama hizi anapaswa kuwahi hospitali mara moja kwa uangalizi zaidi.
Soma Zaidi...Post hii itakujulishs kwa namna gani mwanaune anaweza kupata fangasi kwenye uume wake
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa njia za kukusaidia kuacha punyeto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi wajibu wa Mama mjamzito katika kileo mimba sio yeye tu Bali na wote waliomzunguka wanapaswa kuhakikisha kuwa mama mjamzito anapaswa kufanyiwa huduma zote Ili kuweza kujifungua salama na bila shida yoyote.
Soma Zaidi...Ni kweli kuwa kutema mate mara kwa mara inaweza kuwa ni dlili za ujauzito. Lakini itambulije kuwa pekee sio kithibitishi cha ujauzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa akina dada.
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza ishara na dalili ninazoonyesha kuwa mimba ipo hatarini kutoka ama inaweza kuwa imeshatoka.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuepuka fangasi za ukeni, ni njia ambazo usaidia kuepuka madhara ya fangasi za ukeni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi maji ya Amniotic ni maji ambayo uzunguka mtoto na kufanya kazi mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...