image

Dalili za mimba ya mtoto wa kiume ama mtoto wa kike

Posti hii inakwenda kukueleza jinsi ya kuwjuwa kama mtoto ni wa kike ama wa kiume.

Kila mwanamke mwenye mina ana hamu ya mujuwa jinsia ya mtoto wake. Huwenda ili aweze kujiandaa kununua mavazi mapema, ama kupata pongezi kutoka kwa mwenzi wake ambaye amemuahidi kuzipata endapo atakuwa na mtoto wa jinsia fulani. Dalili za mimba iwe ya mtoto wa kike ama wa kiume ni zilezile isipokuwa kuna mambo flani yanaongezeka.  Katika post hii nitakueleza dalili ambazo watu wengi wanaamini kuwa zinaonyesha jinsia ya mtoto. Hata hivyo pia nitakueleza usahihi wa maoni yao kitaalamu.

 

Dalili za kawaida za ujauzito wa mtoto bila kujali jinsia:

  1. Kutoka na matone ya damu iliyo nyepesi
  2. Kukosa hedhi
  3. Maumivu ya kichwa bila ya sababu
  4. Mwili kuongezeka joto
  5. Mapigo ya moyo kuongezeka
  6. Kupata kizungzungu
  7. Kupatwa na kichefuchefu
  8. Kuchoka bila ya kufanya kazi
  9. Maumivu ya tumbo

 

Sasa wacha tuje kwenye swali letu la awali kuhusu dalili za mimba ya mtoto wa kiume ama wa kike. katika kuelezea kkila dalili nitakwenda kukuambia uhakika wa dalili hizo. Jambo la kuzingatia ni kuwa dalili pekee hazithibitishi bila ya kupata vipimo kwa kitaalamu. kwani misingi ya dalili hizo imewekwa kutokana na imani za watu vile wanavyodhani ama mazoea yao ama historia ya yale yaliowakuta.

 

Dalili za mimba ya mtoto wa kiume ama wa kike:

  1. Uzito wa tumbo; Inaaminika kuwa endapo mjamzito atahisi tumbo ni zito sana basi mtoto ni wa kiume. lakini endapo tumbo siuo zito sana basi mtoto ni wa kike. Wanaamini kuwa mtoto wa kiume ni mzito kuliko wa kike. Hata hivyo nadharia hii haina uithibitisho wa kitaalamu ijapokuwa watu wanaamini hivyo.

 

  1. Kichefuchefu: Wanadai wamama kuwa endapo mjamzito atakuwa na kichefuchefu sana basi mtot ni wa kiume. na endapo hatapata kabisa ama itakuwa ni cha kawaida basi mtoto ni wa kike.

 

  1. Mabadiliko kwenye ngozi: Dhana hii ni kuwa endapo mwanamke atapata mabadiliko kwenye ngozi yake, mabadiliko ambayo yatakwenda kuharibu muonekano wa ngozi na uzuri wake basi mimba hiyo ni ya mtoto wa kike. Pia wnaamini kuwa mtoto wa kike anachukuwa urembo wa mama yake. Miongoni mwa mabbadiliko hayo ni chunusi, ngozi kupauka na kukosa mvuto. Kwa uoande mwiungine mtoto wa kiume hawezi kumfanya majamzito abadilikwe na ngazi yake. pia nadharia hii haina ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa madaktari.

 

  1. Mabadiliko ya nywele waumini wa dhana hii wanasema kuwa mtoto wa kiume hana shida na uzuri wa mama yake. Kwa kuwa nywele ni moja ya uzuri wa mama basi zitabaki kama zilivyo. kwanamke hatakuwa na mabadiliko ya nywele akiwa na mimba ya mtoto wa kiume. Kwa upande mwingine mimba ya mtoto wa kike itamfanya nywele kunyonyoka ama kukatika. Imani hii pia haina ushahidi wa kisayansi.

 

  1. Kuchaguwa sukari na chumvi: Inaaminika kuwa mwanamke mwenye mimba ya mtoto wa kike anapenda sana vitu vitamu. lakini ikiwa mimba ni ya mtoto wa kiume anapendelea sana vitu vyenye chumvi chumvi. hata hivyo hakuna ushahidi wa kitaalamu kuthibitisha nadharia hii.

 

  1. Utofauti wa kwenye mapigo ya moyo: Wanaamini kuwa endapo mimba ni ya mtoto wa kike mapigo ya moyo huwa mengi zaidi. kwa mfano yakiwa ni zaidi ya 140 ndani ya dakika basi mimba ni ya mtoto wa kike. na yakiwa chini ya 140 mtoto ni wa kiume. nadharia hii inaonekana ni ya kitaalamu zaidi, hata hivyo haina ushahidi wa kuthibitisha.

 

Je nitajuwaje kwa uhakika kuwa mtoto ni wa kiume ama wa kike?

Sasa wacha tuangaie kitaalamu zaidi kwa namna gani utaweza kujuwa jinsia ya mtoto. Ukweli ni kwamba utaweza kuwa na uhakika wa jinsia ya mtoto kwa kutumia vipimo. Hivyo hapa nitakueleza baadhi ya vipimo ambavyo vinatumika kujuwa jinsia ya mtoto.

  1. Kwa kutumia kipimo cha damu cha DNA kwa mfano kipimo cha panorama kinachojulikana kama Noninvasive prenatal testing (NIPT). Kipimo hiki kinaweza kuonyesha jinsia ya mtoto kuanzia wiki ya 7 hadi ya 10 toka ujauzito kutungwa.

 

  1. Kwa kutumia kipimo cha utrasound: Kipimo cha utrasound hutumika kumulika ndani ya tumbo la mjaozito na kumuona mtoto na jinsia yake. kipimo hilki kinaweza kuona jinsia ya mtoto kuanzia ujauzito wa wiki ya 18 hadi 20.

 

Mwisho nimalizie kusema kuwa bila ya kutumia vipimo vya kitaalamu hatuwezi kuwa na uhakika juu y jinsia ya mtoto. Hivyo kwa mwenye kutaka kujuwa jinsia ya mtoto afanye vipimo vya kitaalamu. kwa mfano kipimo cha utrasound sio cha ghali kukifanya ukilinganisha vipimo vinginevyo.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 38957


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

sas na karibia mwezi nawashwa sehem Zang za sili kwenye shingo ya uume najikuta najikuna mpk natoka vidonda
Soma Zaidi...

Dalili za maumivu ya hedhi
Maumivu ya hedhi (dysmenorrhea) ni maumivu makali au ya kubana sehemu ya chini ya tumbo. Wanawake wengi hupatwa na Maumivu ya hedhi kabla tu na wakati wa hedhi zao. Kwa wanawake wengine, usumbufu huo ni wa kuudhi tu. Kwa wengine,  Soma Zaidi...

Habari Mimi ni mjamzito was miezi Tisa sasa nimeanza kutokwa na maji kidogo kidogo ukeni bila uchungu na no mimba yangu ya kwanza he Kuna shida?
Ujauzito husababisha mabadiliko mengi mwilini, ikiwepo ongezeko la Majimaji ukeni ifikapo tarehe za kukaribia kujifunguwa. Majimaji haya ni muhimu kwa afya ya mtoto aliye tumboni. Soma Zaidi...

je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba?
Nina swali langu:-je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba? Soma Zaidi...

Mapendekezo muhimu kwa wajawazito
Posti hii inahusu zaidi mapendekezo muhimu kwa wajawazito, haya ni mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu wa afya ili wajawazito waweze kule mimba zao vizuri na kuweza kujifungua vizuri na kupata watoto wenye afya njema na makuzi mazuri pasipokuwepo na ule Soma Zaidi...

Post hii inahusu zaidi umuhimu wa kondo la nyuma
Kondo la nyuma ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamziti,kondo la nyuma husaidia katika kazi mbalimbali katika ukuaji wa mtoto. Soma Zaidi...

Sababu za kutokea kwa saratani ya matiti
Saratani ya matiti ji moja kati ya saratani zinazosumbuwa wqnawake wengi. Katika somo hili utajifunza chanzo cha kutokea saratani ya matiti Soma Zaidi...

Mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo
Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo chini ya umri wa miaka mitano ili kuweza kuweka afya yake kwenye njia safi. Soma Zaidi...

Sababu za Ugonjwa wa kifafa cha mimba.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kifafa cha mimba, kwa kawaida mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu sababu za kuwepo kwa kifafa cha mimba ila kuna visababishi vinavyofikiliwa kama ni Dalili za kifafa cha mimba kama ifuatavyo Soma Zaidi...

Kwa nini hujapata siku zako za hedhi.
Unaweza kupitiliza siku zako za hedhi kwa sababu nyingi. Post hii itakueleza ni kwa nini umechelewa kupata siku zako. Soma Zaidi...

Dalili kuu za mwanzo za mimba changa, kuanzia siku ya kwanza
Ni ngumu ila nitakujuza namna ya kuitambuwa mimba ya siku moja hadi 3, mimba ya wiki moja na mimba ya miezi mitatu kwa dalili. Soma Zaidi...

Dalili za mimba yenye uvimbe
Mimba ya tumbo - pia inajulikana kama hydatidiform mole - ni ugumu usiyo na kansa (benign) ambayo hutokea kwenye uterasi. Mimba ya molar huanza wakati yai linaporutubishwa, lakini badala ya mimba ya kawaida, yenye uwezo wa kutokea, plasenta hukua na kuwa Soma Zaidi...