image

Dalili za ugonjwa wa ngiri

Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo mgonjwa wa ngiri anaweza kuzipata, kwa hiyo baada ya kusoma na kuelewa dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospitali mapema kwa ajili ya kupata matibabu.

Dalili za ugonjwa wa ngiri.

1​​​​​​. Kwanza kabisa tunajua kuwa ugonjwa wa ngiri utokea pale ambapo misuli au kuta za tishu mwilini ambazo ushikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kubwa na uwazi na kufanya viungo hivyo kutoshikilia vizuri katika sehemu inayostahili hali ambayo Usababisha mtu kuhisi maumivu na pengine kuwepo kwa uwazi  katika sehemu mbalimbali za mwili hali ambayo Usababisha nyama kuota na kuelekea kwenye sehemu hizo za uwazi. 

 

2.Kuna Dalili mbalimbali ambazo ujitokeza iwapo  mtu amepata tatizo hili na dalili hizi utofautiana kutoka kwa mtu mmoja na mwingine kwa sababu ugonjwa huu ushika sehemu tofauti kama vile kwenye kifua, kwenye kitovu na kwenye mshipa wa ngiri na pengine kwa sababu ya upasuaji kwa hiyo Dalili utofautiana kulingana na Ugonjwa umeshika sehemu ipi.

 

3. Mtu mwenye tatizo la ngiri anaweza kubanwa na tumbo hasa chini ya kitovu wakati wa baridi na pengine pale anapokuwa ameshiba au amekula vitu vitamu, hiyo huwa ni dalili ya ngiri ya kitovu kwa walio wengi.

 

4. Kupinga mingurumo tumboni.

Kwa kawaida ngiri nyingi ili kutokea uanzia kwenye tumbo ambapo sehemu ya utumbo inaota kuelekea kwenye uwazi fulani inawezekana kwenye kifua au na sehemu mbalimbali za mwili ambapo ngiri inaweza kutokea kwa hiyo hali hii usababisha mingurumo kutokea kwenye tumbo.

 

5. Kuhisi una haja kubwa na ukifika chooni unatoa gesi tu, kwa hiyo kama kuna tatizo hili la ngiri tumbo ukaa na  gesi sana ,hii ni kwa sababu ya hali ya tumbo kutokuwa kwenye hali yake ya kawaida.

 

6. Kukaa siku kadhaa bila kupata haja kubwa , inawezekana kwa siku kama mbili au zaidi bila kuwepo kwa choo, au ukibatiwa kupata choo ni kidogo sana na huwa kama choo ya mbuzi.

 

7. Pengine Mgonjwa anakwenda haja mara kwa mara, hasa anakuwa anahisi haja kubwa na akienda uko ni gesi na choo kidogo hali hiyo usumbua sana na kufikia kiasi cha mgonjwa kukaa karibu na choo na hatoi kitu cha maana.

 

8. Kupotea kwa nuru ya macho.

Mara nyingine kuna wagonjwa ambao nuru za macho upotea, ila hali hii utokea kwa mara chache sana na sio kupotea kwa nuru ni tatizo la ngiri kwa hiyo mgonjwa anapaswa kupima kwanza ili kujua tatizo ni nini.

 

9. Maumivu makubwa ya mgongo na kiuno.

Kuna wagonjwa wengine wanahisi kuwa na maumivu makali ya mgongo na kiuno na pengine hali inaweza kufikia kiasi kwamba Mgonjwa anashindwa kutembea, kwa hiyo ni vizuri kupima haraka na kugundua tatizo ni lipi.

 

10. Makende kuwa kwenye sehemu moja.

Kuna wakati mwingine makende yote yanakuwa kwenye sehemu moja kwa hiyo ni vizuri kujua Dalili hii ili kuweza kutibu na pengine mgonjwa anahisi maumivu makali sana kwenye sehemu za siri hasa kwa wanaume.

 

11.Pamoja na kujua Dalili zote za ngiri ni vizuri kabisa kujua kuwa sio Dalili zote ni za kuwepo kwa ngiri kwa hiyo vipimo ni lazima na kuwaona wataalamu wa afya ni jambo la muhimu sana ili kuweza kugundua kuwae ni tatizo gani kwa sababu kuna Magonjwa mbalimbali ambayo yana Dalili kama hizi.

 

12.Pia tunapaswa kutoa wito kwa jamii kuwa ugonjwa wa ngiri upo na unatibika kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa kwa jamii ili kuepuka hali ya kuwaficha wagonjwa wakiwa na umani kuwa ni magonjwa ya zinaa na kuona kuwa ni aibu kwa familia na kuwatibu wagonjwa ki mila hali inayosababisha kuongezeka kwa maumivu na tatizo kubwa kubwa zaidi.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 3831


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Naomb niulize ukiingiliana na mwanmke mweny ukimwi unaweza kuambikizwa na kusaambaaa kwa mda gan ndan ya mwil
Muda gani ukimwi huweza kuonekana mwilini ama kugundulika kama umeathirika, ni dalili zipo hujitokeza punde tu utakapoathirika Soma Zaidi...

Maambukizi kwenye mfumo wa usagaji chakula unaotokea kwenye utumbo mkubwa (diverticulitis)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na mifuko midogo midogo, iliyobubujika ambayo inaweza kuunda kwenye utando wa mfumo wako wa usagaji chakula. Wao hupatikana mara nyingi katika sehemu ya chini ya utumbo mkubwa (koloni). Hali hiyo inajulikana kama Divert Soma Zaidi...

Aina za kisukari
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za kisukari Soma Zaidi...

Dalili za UTI kwa wanaume
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za UTI upande wa wanaume Soma Zaidi...

Fahamu Magonjwa yanayowapata watoto chini ya miaka mitano
Posti hii inaelezea kuhusiana na Magonjwa mbalimbali ambayo watoto chini ya miaka wanaweza kuyapata kiurahi. Soma Zaidi...

NINI CHANZO CHA UGONJWA WA MALARIA? NI YUPI MBU ANAYESAMBAZA MALARIA
Malaria husababishwa na vimelea (parasite) ambavyo husambazwa ama kubebwa na mbu aina ya anopheles. Soma Zaidi...

Dalili za za kuwepo kwa maambukizi chini ya kitovu
Posti hii inahusu zaidi dalili za kuonyesha kuwa Kuna maambukizi kwenye kitovu hasa hasa chini ya kitovu. Soma Zaidi...

Nini hasa chanzo cha pumu, na je inarithiwa?
Ugonjwa wa pumu ni moja katika magonjwa hatari yanayoweza kutokea kwa ghafla, na endapo itacheleweshwa kudhibitiwa inaweza sababisha athari mbaya zaidi Soma Zaidi...

Matatizo yanayosababisha saratani ya mapafu
Posti hii inaonyesha matatizo yanayosababisha saratani ya mapafu . Soma Zaidi...

Namna ya kuzuia Ugonjwa wa ini
Posti hii inaelezea namna na jinsi ya kujikinga au kuzuia Ugonjwa wa ini. Soma Zaidi...

Dalili za tetekuwanga
Tetekuwanga (varisela) ni maambukizi ya virusi ambayo husababisha kuwasha, upele kama vile malengelenge. Tetekuwanga huambukiza sana watu ambao hawajapata ugonjwa huo wala kupewa chanjo dhidi yake. Kabla ya chanjo ya kawaida ya tetekuwanga, karibu watu Soma Zaidi...

Watu walio hatarini kupata ugonjwa wa pumu
Kila mtu anaweza kupata ugonjwa wa pumu, hata hivyo kuna ambao wapo hatarini zaidi kupata pumu. Soma Zaidi...