DALILI ZA UJAUZITO  KICHEFU CHEFU, KUTAPIKA, HEDHI, DAMU UKENI, KUJOJOAKOJOA N.K (mimba changa, mimba ya wiki moja, mimba ya mwezi mmoja )

DALILI ZA UJAUZITO KICHEFU CHEFU, KUTAPIKA, HEDHI, DAMU UKENI, KUJOJOAKOJOA N.K (mimba changa, mimba ya wiki moja, mimba ya mwezi mmoja )

DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO) Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupotea bila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua.

DALILI ZA UJAUZITO KICHEFU CHEFU, KUTAPIKA, HEDHI, DAMU UKENI, KUJOJOAKOJOA N.K (mimba changa, mimba ya wiki moja, mimba ya mwezi mmoja )

DALILI ZA UJAUZITO

DALILI KUU ZA MIMBA (UJAUZITO)
Watu wengi sana wamekuwa wakilalamika kuwa mimba zao zinatoka, ama kupotea bila ya kujulikana tatizo wala bila ya kuugua. Wapo wengine wanakujakujitambua ujauzito ukiwa na miezi kadhaa. Sasa ni zipi hasa dalili za ujauzito?. huenda swali hili kwa wanawake walio wengi lisiwe na manufaa kwao kwani tajari ni wajuzi wa swala hili. Halikadhalika wanaume wengi wanaujuzi pia. Kwani wengi wanaelewa kuwa dalili ya ujauzito ni kukosekana kwa siku za mwanamke yaani hedhi kwa vipindi zaidi ya kipoja. Lakini itambulike kuwa hii sio dalili pekee, kwani siku zinaweza kukosekana na isiwe mimba. Katika makala hii tutakwenda kuonesha kwa utani dalili kadhaa za ujauzito.

Kabla ya kiziona dalili hizo ningependa kutumia muda kidogo kueleza tatizo la kukosa kwa hedhi. Hedhi ni muhimu kwa kila mwanmke ambaye amefikia umri wa kupata ujauzito. Afya ya mwanmke huyu huwa salama kama hedhi yake ipo salama. Kwa kawaida hedhi huweza kukatika yaani kukata kutoka kabisa pindi umri wa mwanamke unapokuwa mkubwa yaani kuanzia miaka ya 45 na kuendelea. Katika kipindi hiki mwanamke huyu kupata tatizo la kutokupata siku zake ni la kawaida sana, ama siku zake kutokuwa na mpangilio maalumu.

Kwa wanawake walio wadogo kukata kwa hedhi kuna sababi nyingi sana. Watu wengi wamezoea kuwa lamda kupata ujauzito ndio sababu ya kutokupata siku zake. Hii sio swa kabisa. Kukata kwa siku za mwanamke kunaweza kusababishwa na maradhi kama kisukari na baadhi ya maradhi yanayoipata ovari ya mwanamke. Ovari ndio sehemu pekee ya mwanamke ambayo mayai huzaliwa. Hivyo sehemu hii ndio ambayo inatoa homoni ambazo huchochea upatikanaji wa hedhi ama huzuia hedhi isipatikane kutokana na kupata ujauzito. Pia matumizi ya njia za uzazi wa mpango huweza kusababisha tatizo hili la kutokuona siku zake mwanamke. Matumizi ya vyakula, hali ya hewa na madawa ni katika visababishi vikuu vya kutokupata hedhi kwa muda sahihi.

Baada ya kugusia kidogo kipengele hiko sasa tukaone baadhi ya dalili za ujauzito. Kwa hali ya kawaida dalili hizi huweza kuwa tofauti kwa mwanamke mmoja hadi mwingine. Ijapokuwa hali ni kama hii pia zipo dalili ambazo huwapata karibia wanawake wote:-

Kuonekana kwa damu iliyo chache. Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa asilimia 25% (yaani robo) ya wanawake wote wanaopata ujauzito hutokwa na damu kidogo, na rangi ya damu hii haikuiva kama ile ya hedhi. Damu hii hutokea siku 6 mpaka 12 baada ya kutungwa kwa mimba. Ila kwa wanawake walio wengi huiona damu hii kwenye wiki 12 za mwanzo za ujauzito.

Kujaa au kuuma kwa chuchu; mwanzoni mwa wiki ya 1 mpaka ya 2 ya ujauzito mwanamke anaweza kuona kuwa matiti yake yanajaa ama kuwa mazito tofauti na kawaida. Wanawake wengine chuchu za matiti yao zinakuwa ngumu na huwa zinajaa. Wanawake wengine wanaona chuchu ama maziwa yao huwa kama na maumivu wakiyaminya.

Uchovu usio wa kawaida; karibia wanawake wote wanaopata ujauzito huhisi uchovu usio wa kawaida. Mara nyingi dalili hii hutokea mwanzoni mwa wiki ya kwanza toka kupata kwa ujauzito. Na hii ni kutokana na kuwa mwili unazalisha homoni za kuweza kuufanya mwili uweze kulea ujauzito, upatikanaji nwa maziwa kwa ajili ya mtoto ajae. Pia kwa kuwa mwili wa mama unaongeza kuwango cha usukumaji wa damu, hivyo uchovu kutokea ni hali ya kawaida.

Mwanzoni mwa wiki ya kwanza ya ujaozito, mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya ghafla ya kichwa. Na hii ni kutokana kuwa mwili umeongeza kazi ya uzalishaji wa homoni, hivyo ongezeko hili linaweza kusababisha maumivu ya kishwa. Hali si kwa siku nyingi hali hii itapotea.

Kutapika; kwa kawaida hii hali huwapata wanawake wenye ujauzito kuanzia wiki ya pili mpaka wiki ya nane. Kitaalamu hali hii hutambulika kama โ€œmorning sicknessโ€. na huenda hali hii ikaendelea katika kipindi chote cha ujauzito.

Kukojoa mara kwa mara; hali hii hutokea kwa sababu mwili huzalisha homoni iitwayo human chorionic gonadotropin ambayo hii huongeza damu kupita maeneo ya chini yaani kuzunguka sehemu za siri, hivyo hali hii hupelekea mwanamke kwenda kukojoa mara kwa mara.

Kutokupenda baadhi ya vitu ama vyakula. Hii hutokea kwa ghafla mwanamke anachukia baadhi ya vitu ama hususani vyakula bila ya sababu yotyote.


                   

Bongoclass
Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 2253

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰4 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰5 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO
TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO

KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito.

Soma Zaidi...
Sababu za mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Sababu za mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa.

Posti hii inahusu zaidi sababu za mwanamke kukosa tendo la ndoa, ni sababu ambazo uwakuta wanawake wengi unakuta mama yuko kwenye ndoa ila hana hata hamu ya lile tendo la ndoa hali ambayo umfanya mwanamke kuona kitendo cha tendo la ndoa ni unyanyasaji au

Soma Zaidi...
Huduma za msingi kwa mama mjamzito na mtoto.
Huduma za msingi kwa mama mjamzito na mtoto.

Posti hii inahusu zaidi huduma muhimu anazopaswa kupewa mama mjamzito wakati akiwa na mimba, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua yaani ndani ya masaa ishirini na manne, tunajua wazi kuwa Mama akiwa mjamzito anaweza kupata matatizo mbalimbali kwa h

Soma Zaidi...
Je ?kipimo kikionyesha misitar miwili mmoja hafifu mwingine umekolea ni mimba au sio
Je ?kipimo kikionyesha misitar miwili mmoja hafifu mwingine umekolea ni mimba au sio

Kipimo chamimba cha mkojo, huonyesha nestory miwili kuwa una mimba, na mmoja kuwa huna mimba. Sasa je ukitokea mmoja umekoleana mwingine hafifu? Endelea na pasti รขล“ยรฏยธย hadi mwisho

Soma Zaidi...
Mimi imepita miezi mitatu sioni hedhi na wala sioni dalili ya kuwa na mimba unaweza ukaniambia tatizo la kuwa na hali hii
Mimi imepita miezi mitatu sioni hedhi na wala sioni dalili ya kuwa na mimba unaweza ukaniambia tatizo la kuwa na hali hii

Kama na wewe una tatizo la kupitiliza siku zako za hedhi hli ya kuwa huna ujauzito, soma post hii ina majibu yako.

Soma Zaidi...
CHANGAMOTO ZA UJAUZITO, NA DALILI ZAKE NA NAMNA YA KUKABILIANA NAZO
CHANGAMOTO ZA UJAUZITO, NA DALILI ZAKE NA NAMNA YA KUKABILIANA NAZO

Utawezaje kukabiliana na changamoto za ujauzito, je ni zipi changamoto hizo. Hapa nitakujuza.

Soma Zaidi...
Signs and symptoms of pregnancy.
Signs and symptoms of pregnancy.

In fact there is a lot of signs and symptoms of pregnancy a mother experiences throughout pregnant. These signs may start to be revealed immediately after conception or in the first week after conception. A term pregnancy is traditionally calculated by mi

Soma Zaidi...
Huduma kwa mama mwenye mimba Inayotishia kutoka.
Huduma kwa mama mwenye mimba Inayotishia kutoka.

Post hii inahusu zaidi huduma ambayo Mama anapaswa kutolewa pindi mimba inapotishia kutoka huduma hii utolewa kulingana na Dalili tulizoziona zinazohusiana na mimba kutishia kutoka.

Soma Zaidi...
Kwa nini hujapata siku zako za hedhi.
Kwa nini hujapata siku zako za hedhi.

Unaweza kupitiliza siku zako za hedhi kwa sababu nyingi. Post hii itakueleza ni kwa nini umechelewa kupata siku zako.

Soma Zaidi...
Namna ya kumpima mtoto uzito
Namna ya kumpima mtoto uzito

Posti hii inahusu namna ya kumpima mtoto uzito, ni njia ambayo utumika kujua uzito wake na maendeleo ya mtoto.

Soma Zaidi...