Utajifunza dalili za fangasi mdomoni na ulimini, sababu za fangasi wa mdomoni na ulimini, matibabu yeke na njia za kukabiliana nao
Dawa ya fangasi kwenye mdomo na ulimi
Fangasi wanaweza kuathiri sehemu yeyote kwenye ngozi ya mtu. Kuanzia vidole, kichwa, kwapa, sehemu za siri na mapajani. Hutokea fangasi wakaathiri mdomo na ulimi. Hapa hali inaweza kuwa mbaya pale mtu akishindwa kula. Bila shaka ni maumivu, lakini leo nitakwenda kukutajia tiba yake.
Nini sababu ya fangasi wa mdomo na ulimi?
Fangasi hawa husababishwa na aina ya fangasi inayoitwa Candida albicans (C.albicans). hawa fangasi ni kawaida kupatikana kwenye mdomo. Kwa mtu ambaye kinga yake ipo imara hakuna shida yeyote anaweza kuipata kwa kuwa na fangasi hawa. Ila endapo watazidi kupitiliza ndipo inaweza kuleta shida.
Dalili za fangasi kwenye mdomo na ulimi
1.Vijidoma vyeupe au njano kwenye shavu kwa ndani, finzi, midomo na kwenye ulimi
2.Kuvuja kwa damu wa finzi
3.Vidonda kwenye mdomo
4.Kuhisi kama kuna pamba kwenye mdomo (vinyuzinyizi)
5.Ukavu wa kona za mdomo pamoja na mipasuko
6.Taabu katika kumeza
7.Mdomo kuwa na ladha mbaya
8.Kupotesa ladha ya unachokila.
Fangasi wa mdomoni wanaweza kuambukiza?
Yes wanaweza kuambukizwa kwa mfano ukimkisi (denda) mtu anaweza kupata fangasi hawa kama na wewe unao.
Dawa ya fanasi kwenye mdomo na ulimi
1.Fluconazole hiini ya kumeza
2.Clotrimazole (Mycelex Troche) ni kidonge pia cha kumumunyikia mdomoni
3.Nystatin (Nystop, Nyasta) ni ya kuosha mdomo
4.Itraconazole (Sporanox) ni ya kumeza, hupewa wale wenye usugu ama wenye HIV
5.Amphotericin B (AmBisome, Fungizone) hutumika kutibu hali mbaya zaidi ya fangasi wa mdomoni.
Nini ufanye ukiwa unatumia dawa hizi
1.Piga mswaki kwa mswaki ulio mlaini
2.Badili mswaki baada ya kumaliza dozi
3.Usitumie dawa za kuosha mdomo mpaka daktari akuambie.
4.Osha mdomo kwa maji ya chumvi
5.Changanya maji na juisi ya limao kisha knywa
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Kukawa na gesi tumboni kunaweza kuwa ni dalili ya shida kwenye afya, hasa katika mfumo wa chakula. Hali itakuwa sio nzuri endapo utakosea hamu ya kula na kuhisivkushiba muda wowote.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za Doxorubicin and Daunorubicin katika kupambana na kansa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya mucolytic katika kutibu kikohozi kwa watu wazima na watoto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za dawa za NMN maana yake ni Nicotinamide mononucleotide ni dawa ambazo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi homoni mbalimbali ambazo upambana na kansa, hizi homoni zikitumika vizuri matokeo yake huwa na mazuri pia kwa wagonjwa wa kansa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa ya haloperidol katika matibabu ya magonjwa ya akili, ni mojawapo ya dawa ambayo utumiwa na wagonjwa ambao wamechananyikiwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo, ni Aina mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu Minyoo inayosababishwa na bakteria mbalimbali.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ambazo zinatumika kwenye matibabu ya kansa, dawa hizi usaidia kuharibu seli ambazo ambazo hazistahili kwa kitaalamu huitwa malignant seli.
Soma Zaidi...