Nitakujuza dalili za UTI na dawa za kutibu UTI. Pia tutaona njia za kujikinga na UTI pamoja na dalili za UTI
Dawa ya UTI na UTI iliyo sugu
Kama ulishawahi kujiuliza masalikama chanzo cha UTI, sababu zake, njia za kukabiliana na uti vipi uti inaenezwa na ni zipi dawa zake. Makala hii ni kwa ajili yako, nimeiandaa kwa ufupi na kwa ufanisi kiasi cha kuweza kukuridhisha kwa majibu ya maswali yako. Kama utakuwa na mawazo zaidi, tuachie maoni yako hapo chini.
Ugonjwa wa UTI ni nini?
UTI ni kifupisho cha maneno Urinary Track Infection. Ni maambukishi na mashambulizi ya bakteria aina ya E.coil katika mfumo wa mkojo. Mwanzoni bakteria huingia kwenye kibofu, figo ama sehemu yeyote kwenye mfumo wa mkojo. Kisha bakteria huyu anaanza kushambulia na kuathiri mfumo huu na ndipo dalili za UTI huanza kuonekana kama maumivu wakati wa kukojoa. Dalili za uti huonekana kuanzia siku 3 mpaka 8 toka kuambukizwa.
Ni zipi sababu za UTI
Sababu kuu za ugonjwa wa UTI ni bakteria aina ya E.coil. Bakteria huyu huishi kwenye utumbo. Sasa endapoa atapata njia kutoka kwenye utumbo kupitia haja kubwa na akaingi kwenye mfumo wa mkojo hasa hasa kwa wanawake anasababisha UTI. Pia bakteria wanaoishi kwenye uke, mkundu na kuzunguka sehemu za siri wanaweza rahisi kupata njia na kuingia kwenye mfumo wa mkojo na kusababisha uti. Pia UTI inaweza kusababishwa na baadhi ya magonjwa ya ngono kama gonorrhea, chlamydia na mengine.
Ugonjwa wa uti unaenezwa vipi?
Mtu ataweza kupata UTI kama atafanya chochote ambacho kitaletwa bakteria wanaoishi kwenye utumbo kwenye kwenye nia ya mkojo. Kwa mfano kama wakati wa kuchamba alichamba kwa kuelekea mbele kisha bakteria waliotoka kupitia haja kubwa wakafikia kwenye uume ama uuke, hawa wataingi ndani na kusababisha uti. Si kawaida sana uti kuambukizwa kupitia ngono lakini inaweza kutokea. Na ndio maana inashauriwa ukakojoe baada ya kufanya ngono.
Pia maeneo ya chooni mtu anaweza kupata UTI ila pia hii hutokea mara chache sana na ni kwa wanawake ama kwa wale ambao wanajisaidi kwenye vyoo vya kukaa na si kucuchuchumaa ama kusimama hata hivyo si ahisi kwani lamda kama choo ni kichafu ndipo utapata UTI. Hata hivyo watu hawa wapo hatarini zaidi kupata UTI
1.Kama ulishawahi kupata UTI
2.Kama una kisikari
3.Kama una kiriba tumbo
4.Kama unatumia baadhi ya njia za kidhibiti uzazi kama spermicides au diaphrahm
5.Kama una vijiwe kwenye figo au kibofu na vijiwe hivi vikawa vinazuia mkojo kutoka kwa urahisi.
6.Kama ni mjamzito
Ni zipi dalili za UTI?
1.Maumivu wakati wa kukojoa na wakati mwingine yanafanana na kuhisi kuunguwa
2.Mkojo kuwa mchafu kkama wa mawingi ivi na unatowa harufu kali sana
3.Pia mgonjwa anaweza kuona damu ama kama usaha kwenye mkojo
4.Maumivu chini ya tumbo na mgongo
5.Homa
6.Kupatwa na baridi na hatimaye utetemeka
7.Kichefuchefu
8.Kutapika
9.Kuhisi uchovu sana.
NJIA ZA KUJIKINGA NA UTI
1.Kunywa maji mengi na ya kutosha
2.Dhibiti kisukari kama na kisukari
3.Punguza kula vitu vyenye sukari kwa wingi
4.Unapochamba jifute kuelekea nyuma
5.Punguza michepuko
6.Kojoa baada ya kushiriki tendo la ndoa
7.Kojoa pindi unapohisi mkojo
8.usitumie kondomu isiyo na vilainishi
Dawa ya uti
1.Amoxicillin/augmentin
2.Cetriaxone(rocephin)
3.Trimethoprim/sulfamethoxazole
4.Cephalexin
5.Ciprofloxacin (cipro)
6.Fosfomycin
7.Levofloxacin
8.Nitrofurantoin (mecrodantin)
Dawa kama ciprofloxacin na levofloxacin hutumika kutibu UTI sugu, hivyo si vyema kutumiwa kwa uti ya kawaida. Hata hivyo kabla ya kutumia dawa hizi hakikisha unapata ushauri wa daktari kwanza.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi dawa ya streptomycin ni dawa mojawapo ya kupambana na bakteria hasa wanaoshambulia mfumo wa hewa.
Soma Zaidi...Je unasumbuliwa na maambukizi na mashambulizi ya virusi na bakteria kwenye sehemu za siri ama via vya uzazi?. Posti hii inakwenda kuupa ushauri.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea dawa ya kuzuia kuathirika kwa watu walio hatarini kupata VVU
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya pyrantel pamoate ni dawa ambayo usaidia kutibu minyoo ambayo kwa kawaida ukaa kwenye utumbo mdogo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa ya haloperidol katika matibabu ya magonjwa ya akili, ni mojawapo ya dawa ambayo utumiwa na wagonjwa ambao wamechananyikiwa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa mbalimbali ambazo uchangia katika kupunguza nguvu za kiume , hii ni kwa sababu ya wataalamu mbalimbali wanavyosema
Soma Zaidi...Ugonjwa wa manjano ni moja kati ya maradhibyanayosumbuwa ini. Ugonjwa huu unahitaji uangalizi wa haraka hospitali. Posti hii itakwenda kukujuza ninivufanyebendapobmtoto wako ana ugonjwa wa manjano.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi matibabu kwa mgonjwa wa uti wa mgongo, kwa kawaida tunajua kuwa homa hii ya uti wa mgongo usababisha na wadudu mbalimbali kama vile bakteria, virus, fungasi, sumu mbalimbali kama vile madini ya lead na arseni, na vitu kama vile Mag
Soma Zaidi...Ampicillin ni antibiotic yenye msingi wa penicillin ambayo inafanya kazi kupambana na maambukizi ya ndani ya bakteria. Ampicillin hufanya kazi ya kuharibu kuta za kinga ambazo bakteria huunda ndani ya mwili wako na kuzuia bakteria wapya kutokeza. Ampici
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya aminophylline katika kutuliza maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.
Soma Zaidi...