image

Fahamu dawa ya sulfonamide dawa inayopambana na maambukizi ya bakteria mwilini.

Post hii inahusu zaidi dawa ya sulphonamide ni mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na bakteria ni dawa au antibiotics ya mda mrefu na pia matumizi yake sio makubwa sana kwa sababu ya kuwepo kwa antibiotics zenye ngu

Fahamu kuhusu dawa ya sulphonamide katika kupambana na bakteria .

1. Dawa hii kwa kawaida usaidia kupambana na maambukizi ya bakteria kwenye sehemu mbalimbali za mwili kama vile maambukizi kwenye sehemu ya ndani na ya nje ya sikio, matibabu ya nimonia, kuzuia maambukizi kwenye mkojo kwa lugha inayoeleweka ni UTI kutibu maambukizi ya bakteria kwenye mfumo wa upumuaji, maambukizi kwenye mifupa ambayo Kwa kitaamu huiitwa osteomyelitis, matibabu kwenye vidonda vilivyoungua, matibabu ya gonorrhea na pia kwenye tumbo kama Kuna maambukizi ya bakteria.

 

2. Pia dawa hii ufanya Kazi kwa kupitiakwenye mmengenyo wa chakula na pia uingia kwenye mzunguko wa damu na kufanya kazi ya kutibu au kupambana na bakteria,Inapambana na bakteria kwa kuzuia kuzaliana kwa bakteria na wale waliokwishazaliana Wana dumaa na hawaendelea kukua hali inayosababisha matibabu yake kufanikiwa zaidi na pia bakteria hao hawawezi kuzaliana tena na pia dawa hii uingilia kwenye nuklia ya bakteria na kuharibu Kila kitu ndani ya seli ya ya bakteria.

 

3.Dawa hii mara nyingi huwa kwenye mfumo wa vidonge kwa hiyo matumizi yake utegemea wataalamu wa afya , vile vile dawa hii utumiwa na watu mbalimbali ila Kuna watu ambao hawapaswi kuitumia hasa wale wenye aleji na dawa hii pamoja na wale wenye aleji na sulfa na wenyewe hawapaswi kutumia, pia Kuna wale wenye ugonjwa wa maumivu ya kichwa Wanaoaswa kuitumia kwa taahadhari kwa sababu dawa hii Ina maudhi ya kuwepo kwa maumivu ya kichwa kwa watumiaji kwa hiyo wakiendelea kuitumia itawafanya maumivu ya kichwa kuongezeka.

 

4. Vile vile dawa hii Ina maudhi madogo madogo ambayo yanaweza kutokea kwa watumiaji maudhi hayo ni kama kuwashwa kwenye mwili mzima na pengine kutokea kwa vi upele vidogo vidogo ambavyo uendelea kuwasha tu, pamoja na hayo Kuna hali ya kichefuchefu ujitokeza, kutapika na maumivu ya tumbo, pia Kuna upungufu w hamu ya kula uweza kujitokeza,na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara mpaka dawa itakapoisha mwilini.

 

5.kutokana na kuwepo kwa maudhi madogo madogo ni kawaida kwa watumiaji wa dawa ila maumivu hayo yakizidi ni vizuri kuwaona wataalamu wa afya Ili kubadilishiwaa dawa au kupewa dawa ya kutuliza hayo matokeo ya dawa, pia kwa wale ambao huwa na ugonjwa wa maumivu ya kichwa ni vizuri kabisa kuwepo kwenye uangalizi wa wataalamu wa afya Ili kuweza kuepuka madhara mengine ambayo yanaweza kujitokeza.

 

6. Pia dawa hii haipaswi kutumika kiholela inapaswa kutumiwa kulingana na wataalamu wa afya kwa sababu mda mwingine dawa hii Ina matokeo mbalimbali ambayo yakitokea kwa mtu akiwa nyumbani matatizo yanaweza kuwa magumu kidogo, kwa hiyo kuwaona wataalamu wa afya ni jambo la muhimu kwq sababu unakuwa na uhakika wa kutosha.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/22/Thursday - 03:05:03 pm Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 479


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Matumizi ya dawa ya vidonda vya tumbo
Posti hii inahusu zaidi matumizi ya dawa za vidonda vya tumbo, ili kuweza kutumia dawa hizi ni vizuri kabisa kufuata mashariti kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Fahamu dawa za kutuliza magonjwa ya akili inayoitwa Chlorpromazine
Post hii inahusu zaidi dawa zinazosaidis katika kutuliza magonjwa ya akili, dawa hii kwa kitaamu huiitwa chlorpromazine ni dawa ambayo utumiwa na watu wenye tatizo la magonjwa ya akili na kwa kiasi kikubwa huwa sawa. Soma Zaidi...

Njia ya kupitisha dawa kwenye mdomo na vipengele vyake
Posti hii inahusu zaidi njia ya kupitisha dawa kwenye mdomo na vipengele vyake, hii njia dawa umengenywa kwenye tumbo na kupitia kwenye utumbo mdogo na baadae kwenye damu, Soma Zaidi...

Ifahamu dawa ya furosemide.
Post hii inahusu zaidi dawa ya furosemide ni mojawapo ya dawa ambayo ipo kwenye kundi la diuretics na kwa jina linguine huitwa lasix Soma Zaidi...

dawa ya kutibu infection kwenye kizazi nisaidie doctor
Je unasumbuliwa na maambukizi na mashambulizi ya virusi na bakteria kwenye sehemu za siri ama via vya uzazi?. Posti hii inakwenda kuupa ushauri. Soma Zaidi...

Dawa za fangasi ukeni
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za fangasi ukeni Soma Zaidi...

Fahamu Dawa inayotumika kupunguza maumivu (ibuprofen)
Ibuprofen ni mojawapo ya dawa zinazotumiwa sana duniani kote! Ili kupunguza maumivu na kuvimba, agiza Ibuprofen leo na upate afya bora! Ni kiungo amilifu katika dawa za jina kama vile Motrin na zaidi. Ibuprofen pia inaweza kuuzwa kama: Advil Motrin, Soma Zaidi...

Ni dawa gani hatari kwa mjamzito?
Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu dawa ya marcolides dawa ya kuuwa bakteria, kwenye mfumo wa hewa
Post hii inahusu zaidi dawa ya macrolide ni mojawapo ya dawa ya kutibu au kupambana na bakteria na upambana na bakteria wafuatao streptococcus pyogenes, staphylococcus aureus na haihusiki na haemophilia influenza ambao usababisha maambukizi kwenye mfumo w Soma Zaidi...

Ijue Dawa ya lignocaine
Posti hii inahusu zaidi dawa ya lignocaine kama mojawapo ya Dawa ambayo utumika wakati wa upasuaji. Soma Zaidi...

Dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo.
Posti hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole katika kutibu Minyoo, ni Aina mojawapo ya dawa ambayo usaidia kutibu Minyoo inayosababishwa na bakteria mbalimbali. Soma Zaidi...

Dawa za kutibu kiungulia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za kutibu kiungulia Soma Zaidi...