Je unazijuwa faida za kuwa na vitamini E mwilini mwako.Unahani utapata matatizo yapi ya kiafya endapo utakuwa na upungufu wa vitamini E mwilini? Makala hii ni kwa ajili yako.
Vitamini E ni moja kati aya vitamini ambavyo vinapatikana kwenye vyakula, matunda na mboga. Pia unaweza kuvipata kwa njia ya vidonge kutoka kwenye maduka ya madawa. Kama vilivyo vitamini A, B, C, D na K vitamini E navyo endapo vitapungua mwilini kutakuwepo na madhara kiafya. Ijapokuwa upungufu wa vitamini hivi ni aghalabu sana kutokea. Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake.
YALIYOMO:
Maana ya Vitamini E
Mnamo mwaka 1922 wanasayansi wawili kwa majina ya Herbert Mclean Evans na mwenzie Katharine Scott Bishop waligundua vitamini E. baada ya ugunduzi wa vitamini E tafiti mbalimbali ziilifanywa katika kuonyesha ni zipi kazi za vitaini E mwilini. Kwa mfano Mwaka 1946 wanasayansi walikuwa wakifanya tafiti juu ya nadharia inayodai kuwa vtamini E husaidia dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu (coronary heart diseases). mwaka 1949 tafiti zilifanywa kuhusu nadharia ya kuwa vitamini E huweza kusaidia watoto njiti kuwakinga na maradhi kadhaa.
Kazi za vitamini E mwilini
Vitamini E katika miili yetu zina kazi kuu zifuatazo:
Vitamini E bi antioxidant, ndani ya miili yetu husaidia katika kuzuia athari za kemikali mbaya zifiharibu miiliyetu.
Husaidia katika utengenezwaji wa utando wa seli,na kulinda seli dhidi ya uharibifu wa kemikali.
Husaidia katika ukuaji mzuri wa misuli.
Husaidia katika utengenezwaji wa utando maeneo mbalimbali ya mwili kama kwenye neva, mapafu, na maeneo mengine
Upungufu wa vitamini E
Upungufu wa vitamini E hutokea nadra sana lakini tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E vikipungua mwilini vinaweza kusababisha matatizo kwenye mfumo wa fahamu., ukuaji mzuri wa misuli na udhaifu wa misuli. Pia upungufu wa vitamini E unaweza kuathiri macho na hivyo kupelekea mtu kutoona vizuri.
Vyakula vya vitamini E
Tafiti mbalimbali kuhusu vitamini E
Tafiti hizi zilifanya lakini zinahitaji kuendelea zaidi maana bado majibu ya uhakika hayajapatikana juu ya matokeo ya tafiti hizo. Ijapokuwa maneno ni kama hivyo lakini ukweli ni kuwa vitamini E vina faida katika afya zetu:-
1. Mwaka 2017 tafiti zilifanya na kuonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kupunguza udhaifu wa misuli wakati wa kuzeheka
2. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kulinda mtu dhidi ya maradhi ya ubongo kama kusahausahau na kuchanganyikiwa.
3. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E mwilini husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya figo, kibofu, mapafu na korodani.
4. Husaidia kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu
5. Husaidia kwa wajawazito
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi madhara ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni, haya ni madhara ambayo utokea kwa sababu ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni.
Soma Zaidi...Dalili za mimba zinaweza kuwa tata sana kuzijua mpaka upate vipimo. Kwa mfano unaweza kupatwa na maumivu yakibofu. Je unadhani nayo ni dalili ya mimba?
Soma Zaidi...Kukaza kwa misuli lunaweza kutokea muda wowote ila mara nyingi hutokea pindi mtu anapofanya mazoezi, amnapoogelea ama anapofanya kazi.
Soma Zaidi...Kushambuliwa kwa moyo na kupumua ni kitendo Cha moyo kusimama ghafla, Hali hii unapaswa kutolewa huduma ya kwanza Ili moyo ufanye kazi tena,
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea namna ambavyo mwili unapambana na maradhi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya kazi ya protin na vyakula vya protini mwilini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida ya chanjo, tunajua wazi kuwa chanjo Ina faida kubwa kwenye mwili wa binadamu na vile vile kwenye jamii kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume
Soma Zaidi...