Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni.
Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni. Kitaalamu fangasi hawa hujulikana kama tinea” au “dermatophytosis. Na kwa maarufu sana wanafahamika kama ringworm kwa kuwa wanatoa mabako ya mduara kwenye ngozi.
Fangasi hawa wanaweza kukaa kwenye ngozi, kuta, nguo, taulo na maeneo mengine. Miongoni mwa dalili zao ni kuona maduara kwenye ngozi, mara nyingi dalili za fangasi hawa huweza kuonekana kuanzia siku 4 mpaka 14 baada ya ngozi kupata maambukizi ya fangasi hawa. zifuatazo ni katika dalili za fangasi hawa:-
Fangasi hawa wanaweza kukaa katika maeneo mbalimbali ya mwili na kusababisha dalili tofautitofauti kulingana na eneo lililo athirika. Kwa mfano;-
Fangasi hawa wakiwa kwenye nyayo (sthlete’s foot) huweza kuonesha dalili kama nyayo kuwa nyekundu, kuvimba ama kujaa maji, ngoxi kutoka ama kubabuka, kuwasha kwa ngozi katikati ya vidole na kidole na mara nyingi kati ya kidole kidogo na kinachomfatilia. Wakati mwingine kisigino na nyayo huweza kuathirika na kuweka mabumbuza.
Kwenye kichwa, fangasi hawa huweka maduara yaliyo nyonyoka ngozi, yakiwa na ukurutu, ngozi kavu, na kuwasha. Maduara haya maarufu tunayaita mapunye, yanaweza kuwa mengi na kuungana kufanya duara moja kubwa. Mara nyingi sana fangasi wa kichwani huwapata sana watoto kuliko watu wazima.
Kwenye pachipachi za mapaja (jock itch). Fangasi hawa hukaa sehemu ya ndani ya mapaja karibu na sehemu za siri ama kuzungukia eneo hilo, lakini wanashambulia mapaja. Miongoni mwa dalili zao ni mapaja kufanya wekundu, kuwasha na hali inaweza kuwa mbaya mpaka ngozi ikababuka na hatimaye kufanya vidonda kwa kujikuna. Wanaweza kushambulia pia korodani na kufanya ibabuke, iwe nyekundu na kuweka vidonda.
Fangasi wa kwenye ndevu (tinea barbae). fangasi hawa wanashambulia maeneo ambayo ndevu zinapatikana kama kwenye kidevu na shavu. Dalili zao ni kuwasha kwa kidevu, shavu, na sehemu ya juu ya shingo. Fangasi hawa wanaweza kuwa hatari zaidi na kusababisha mapele yenye usaha kwenye eneo hili.
Huweza kuwapata wenye ndevu ama ambao wananyoa ndevu. Dalilizao ni kama za fangasi wa maeneo mengine, kama eneo kuwa jekundu, kuwasha kuwa na madoamadoa na kunyonyoka kwa ndevu katika eneo lililo athirika.
Walio hatarini zaidi kupata fangasi hawa
Watu wote wanaweza kupata fangasi hawa wa mapunye. Lakini kuna watu wengine wapo hatarini zaidi. Na hii ni kutokana na shughuli zao wanazofanya, mazingira wanayoishi ama staili za maisha yao.
Namna ya kujilinda na mapunye
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia ugonjwa wa Homa ya inni, ni njia ambazo utumiwa Ili kuepuka kusambaa kwa ugonjwa wa Homa ya inni kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine,
Soma Zaidi...Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces, hawa ni fangasi wanaosababisha maradhi yajulikanayo kama blastomycosis.
Soma Zaidi...Mie ni kijana wa kiume umri 33, nna tatizo la kujaa mate mdomoni nimeambiwa nna minyoo lakini hata nikinywa dawa sioni afadhali, niliona labda ni pombe nikapumzika kunywa tatizo lipo pale pale japo nisipokunywa haliwi kwa ukubwa ule ila lipo.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kichaa cha mbwa ni virusi hatari vinavyoenezwa kwa watu kutoka kwa mate ya wanyama walioambukizwa. Virusi vya kichaa cha mbwa kawaida hupitishwa kwa kuuma.
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na Upotevu wa kusikia unaotokea hatua kwa hatua kadri umri unavyozeeka (presbycusis) ni jambo la kawaida. T Kwa wale walio na umri wa zaidi ya miaka 75, idadi ya watu walio na upotezaji wa kusikia inakaribia 1 kati y
Soma Zaidi...Shinikizo la chini la damu (hypotension) litaonekana kuwa jambo la kujitahidi. Hata hivyo, kwa watu wengi, shinikizo la chini la damu linaweza kusababisha dalili za Kizunguzungu na kuzirai. Katika hali mbaya, shinikizo la chini la damu linawez
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu. Ni katika maumivu amaboyo kwa wanaume mara nyingi huhusishwa an ngiri na kwa upande wa wanawake huhusishwa na chango hasa pale wanapokaribia kuingia katika siku zao. Ma
Soma Zaidi...Pumu ni ugonjwa wa njia ya upumuaji unaojulikana na kizuizi cha muda mrefu cha njia ya upumuaji. Inahusisha mfumo wa upumuaji unaobana njia ya hewa, Inaweza kuwa ya nje (hii hutokea kwa vijana kutokana na mizio) au ya ndani (hutokea kwa wazee)
Soma Zaidi...