picha

Hadithi Ya 29: Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote

Hadithi Ya 29: Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote

Hadithi Ya 29: Muabudu Allaah Na Usimshirikishe Na Chochote

الحديث التاسع والعشرون

"تعبد الله لا تشرك به شيئا"

عن معاذِ بن جبلٍ رضي الله عنه قال: قلت: يا رسول الله، أخْبِرني بِعَمَلٍ يُدْخِلُني الجنَةَ ويُبَاعِدُني عَنِ النارِ. قال: ((لَقَدْ سألْتَ عَنْ عَظيمٍ، وإنَهُ لَيَسيرٌ عَلى من يَسَّرَهُ اللهُ تعالى عَلَيْهِ : تَعْبُدُ اللهَ لا تُشْرِكُ بِهِ شَيئاً، وتُقيمُ الصَّلاةَ  ،وتُؤتي الزكاةَ، وتصومُ رمضانَ، وتَحُجُّ البيتَ)) .ثم قال:  (( ألا أَدُلُّكَ على أبْوَابِ الخيرِ؟: الصَّومُ جُنَّةٌ، والصَّدقةُ تُطْفِىءُ الخَطِيئةَ كما يُطْفىءُ الماءُ النارَ، وصَلاةَ الرَّجُلِ في جَوْفِ الَّليْلِ، ثم تلا: {تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنْ الْمَضَاجِعِ} - حتى بلغ - {يَعْمَلُونَ}   السجدة: 16-17 .

ثم قال:  ((ألا أُخْبِرُكَ بِرَأسِ الأمْرِ وَعَمودِهِ وَذِرْوَةِ سَنَامِهِ؟)) قلتُ: بَلىَ يا رسول الله. قال:  (( رَأْسُ الأمْرِ الإسلامُ، وعَمُودُهُ الصَّلاةُ، وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الجِهادُ )).

ثم قال: (( ألا أخْبِرُكَ بِمِلاكَ ذَلِكَ  كلِّهِ ؟)) فَقُلْتُ بَلَى يا رَسول الله، فأخَذَ بِلِسانِهِ وقال:   ((كُفَّ عَلَيْكَ هذا)) . قلت : يا نبيَّ الله، وإنَّا لمؤاخَذُونَ بِما نَتَكَلَّمُ بِه ؟)) فقال: (( ثَكِلَتْكَ أمُّكَ يَا مُعَاذُ,  وَهَلْ يَكُبُّ الناسَ في النارِ على وُجُوهِهِمْ ))   أو قال: ((على مناخِرِهِم - إلاَّ حَصَائدُ  ألسِنَتهم))

 

رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ   وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ. 

 


HADITHI YA  29 MUABUDU ALLAAH  NA USIMSHIRIKISHE NA CHOCHOTE

 

Kutoka kwa  Mu'aadh Ibn Jabal رضي الله عنه  amesema:

Nilisema: Ewe Mtume صلى الله عليه وسلم  , niambie kitendo ambacho kitanipeleka peponi na kitaniokoa na moto.  Akasema : Umeniuliza jambo kubwa lakini ni rahisi kwa yule ambae Mola anaemsahilishia.   Muabudu Allaah wala usimshirikishe na chochote, Swali, toa Zaka, funga             Ramadhani, nenda kuhiji (Makka).  Kisha akasema:  Je? Nikuonyeshe  milango ya kheri?  Saumu ni ngao, sadaka inazima dhambi kama vile maji yanavyozima moto, na kuswali katikati ya usiku: Kisha akasoma  {Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku. Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda}

 Sura As-Sajda  32: 16 na 17

Tena akasema:  Je, nikwambie kilele cha hilo jambo; nguzo yake na sehemu yake ya juu kabisa?  Nikasema : Ndio ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu.  Akasema:  kilele chake ni Uislamu, nguzo yake ni Swala na sehemu yake ya juu kabisa ni Jihaad.   Kisha akasema : Je, nikwambie muhimili wa yote haya?  Nikasema:  Ndio ewe Mjumbe  wa Mwenyeezi Mungu.   Akaukamata ulimi wake na akasema;  Uzuie huu.  Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu; yale tunayoyasema tutahukumiwa  kwayo? Akasema:  mama yako akuhurumie ewe Mu'aadh!  Kuna kitu zaidi kinachowaangusha watu kifudifudi motoni kama si mavuno ya ndimi zao?

Imesimuliwa na At-Tirmidhi na ni hadithi Hasan.



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Views 1333

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 ai web app     👉5 Kitabu cha Afya     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Dua za kuwaombea wazazi

Kwenye Quran kuna duaambazo Allah ametufundisha tuziombe kwa ajili ya wazazi, familia na kwa ajili yetu wenyewe.

Soma Zaidi...
DUA YA MUUMINI NA DUA YA KAFIRI

DUA YA KAFIRI NA DUA YA MUUMINI.

Soma Zaidi...
JINSI YA KUOMBA DUA ILI IKUBALIWE NA ALLAH

Kukubaliwa kwa dua kunategemea mahusiano yako na Allah. hata hivyo kuna baadhi ya mabo ukiyafanya dua yako inaweza kukubaliwa kwa haraka zaidi. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kuomba dua ikubaliwe.

Soma Zaidi...
ni nyakati zipi ambazo dua hukubaliwa kwa haraka?

Dua ni moja ya ibada ambazo zinamfanya mja awe karibu na Mweznyezi Mungu. Allah amesisitiza tumuombe dua kwa shida zetu zote, pia akaahidi kuwa atatujibu maombi yetu muda wowote tutakao muomba. Sasa ni zipi nyakati nzuri zaidi kuomb adua?

Soma Zaidi...