Huduma kwa mama mwenye mimba ambayo inataka kutoka.

Huduma kwa mama mwenye mimba ambayo inataka kutoka.

Post hii inahusu zaidi huduma kwa mama ambaye mimba inataka kutoka, mimba za aina hiyo kwa kitaalamu huitwa inevitable pregnant ni lazima itoke tu hata kama kuna juhudi mbalimbali za wataalamu mimba hii utoka kabisa.

Huduma kwa mama mwenye mimba inayotaka kutoka.

1. Kwanza kabisa napenda kuwakumbushia kwamba aina ya mimba hii huwa na dalili zote za mimba kutoka ambazo ni pamoja na kutokwa kwa damu nyingi ambayo uandamana na maumivu makali ya tumbo hasa tumbo la chini.kama mama ataangaliwa na wataalamu wa afya mimba uonekane kwenye mlango wa kizazi na mara nyingi kichanga kinakuwa kimeshakufa tayari kwa hiyo mama ufanyiwa uangalizi wa karibu ili kuhakikisha kwamba mimba inatoka kwa utaratibu bila kuasili maisha ya mama.

 

 

 

 

2. Kama mimba iko chini ya miezi mitatu au wiki kumi na mbili kusafishwa kunapaswa kufanyika  kwa kutumia njia ya kitaalam ambayo inaitwa manual vacuum evacuation, kwa hiyo ni vizuri kabisa akina Mama kuelewa siku zao za mimba ili kuweza kupata huduma inayofaa endapo matatizo kama haya yakitokea.

 

 

 

 

3 . Kama mimba ipo zaidi ya miezi minne au zaidi ya wiki kumi na mbili mama anapaswa kupewa dawa za kuanzisha uchungu ili kuweza kujifungua kawaida dawa hizo huitwa oxtocini na siku zote upitishwa kwenye mirija ya damu, mama anapaswa kupewa taarifa zote hatua kwa hatua na pia aambiwe lengo la kupewa dawa za kuanzisha uchungu.

 

 

 

 

 

4. Pia mama anapaswa kutiwa moyo na kumhakikishia usalama na kumwambia kwamba ni hali ambayo utokea akina Mama wengi na pia urudia hali ya kawaida.

 

 

 

 

5. Pia jamii na watu wa karibu wa mama wanapaswa kumtia moyo  mama na kuachana na mila na desturi za kwamba mimba kutoka ni aibu kwa ukoo kwa hiyo wasimtenge mama bali na wenyewe wapewe elimu kuhusu namna ya kumsaidia na kumtunza mama pale atakaporudi kwa hali ya kawaida.

 

 

 

 

6. Pia mama anapaswa kuambiwa wazi wazi siku za kubeba mimba nyingine na afahamu kwamba baada ya mimba kutoka ndani ya siku ishirini na moja anaweza kubeba mimba nyingine kwa hiyo anapaswa kutumia uzazi wa mpango ili kuepuka kubeba mimba nyingine kabla ya viungo havijawa na nguvu kuweza kutunza mimba, kwa hiyo mama akitoa mimba anapaswa kubeba mimba nyingine baada ya miezi sita.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views: 2289

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 web hosting     👉3 ai web app     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Nahitaji kufaham siku ya kumpatia mimba make wangu, yeye hedhi yake ilianza talehe22

Je na wewe ni moja kati ya wake ambao wanahitajivkujuwa siku za kupata mimba. Ama siku za competes mwanamke mimba. Post hii ni kwa ajili yako.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume

Post hii itakwenda kukuletea orodha ya vyakla vinavyoaminika kuongeza nguvu za kiume.

Soma Zaidi...
Dalili za kuvimba kwa ovari.

  Posti hii inazungumzia kuhusiana na kuvimba kwa ovari kunakosababishwa na maambukizo ya bakteria na kawaida huweza kusababishwa na magonjwa sugu katika Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke.

Soma Zaidi...
Kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa.

Posti hii inahusu zaidi sababu za kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa,ni Dalili ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha estrogen kwenye mwili ukilinganisha na homoni ya projestoren.

Soma Zaidi...
Mabadiliko ya via vya uzazi kwa Mama mjamzito.

Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye via vya uzazi kwa wajawazito, tunajua kuwa Mama akibeba mimba tu kuna mabadiliko utokea katika sehemu mbalimbali za mwili.

Soma Zaidi...
Malezi ya mtoto mchanga na mama mjamzito

Post hii itakwenda kukuletea mambo kadhaa yanayohusiana na malezi bora ya mama mjamzito na mtoto mchanga

Soma Zaidi...