HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYOKA

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYOKA

Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu.

Download Post hii hapa

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYOKA

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYOKA


Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu. Ni vigumu kuwatofautisha wenye sumu na wasio na sumu kwani wakati mwengine wanafanana sifa. Wataalamu wameweka njia kadhaa za kuweza kuwajuwa weenye sumu. Nyoka mwenye sumu ana sifa zifuatazo


1.kichwa chake kipo katika pembe tatu


2.Rangi zake zinameremeta sana


3.Mboni ya Macho yao yamefanana na macho ya paka


4.Wanapoogelea kwenye maji miili yao inaelea juu



Tmbua kuwa sifa hizi hata nyoka wasio na sumu wamaweza kuwa nazo. Kuwa makini na kaa mbali na nyoka wa aina yeyote kama huna ujuzi na utambuzi huu. Mtu aliyengatwa na nyka mwenye sumu ataonyesha dalili zifuatazo:-


1.Uchovu

2.Kizunguzungu

3.Anaweza kuzimia

4.Kichefuchefu

5.Kuharisha

6.Kutapika

7.Mapigo ya moyo kuongezeka kwa kasi

8.Misuli kukosa uweze wa kutanuka na kusinyaa

9.Kuvimba eneo alipong’atwa.



Ukiona mtu ameng’atwa na nyoka na akaonyesha dalili hizi, wahi kuomba msaada ili awahishwe ituo cha afya kwa haraka. Hakikisha unampatia huduma ya kwanza ili kupunguza athari za kusambaa kwa sumu mwilini. Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka inaweza kuwa kwa nama zifuata zo:-




1.mtulize mgonjwa nafsi yake, mpe maneno matamu na ya kutuliza. Hii itasaidia moyo kupunguza kazi ya kusambaza damu mwilini, hivyo sumu haita sambaa kwa kasi.


2.Muweke mgonjwa chini, na katu usimtembeze, mlaze chini kwa namna ambayo sehemu alipong’atwa itakuwa chini. Kwa mfano kama ameng’atwa mguuni, unaweza kumuwekea kitu kichwani akaegemea kwa mto ili sehemu ya mguuni iwe chini.


3.Ondoa mengo ya nyoka kwa uangalifu na katu usimishe eneo alilongatwa na nyoka.


4.Kama mgonjwa ana kizunguzungu, ama baridi mfunike kwa nguo ili kumuongezea joto


5.Chukuwa maelezo kuhusu aina ya nyoka, hii itasaidia wataalamu wa afya kujuwa tiba sahihi.


6.Osha eneo kwa kupitishia maji kwa juu na katu usisugue ama kuminya jeraha.



Usifanye vitu hivi:
1.Usinyonye sumu kwa mdomo wako
2.Usimpe mgonjwa chakula wala maji
3.Usimtembeze mgojwa
4.Usitumie barafu sehemu yenye jeraha
5.Usifunge kwenye jeraha eti kuzuia mzunguo wa damu.



                   

Download Post hii hapa

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Huduma Main: Afya File: Download PDF Views 3413

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Namna ya kusaidia vijana wakati wa kubarehe
Namna ya kusaidia vijana wakati wa kubarehe

Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia vijana wakati wa kubarehe, ni njia za kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa na mwelekeo ,

Soma Zaidi...
Njia za kupunguza uzito na kitambi
Njia za kupunguza uzito na kitambi

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kupunguza tatizo la kuwepo kwa uzito mkubwa pamoja na kitambi

Soma Zaidi...
Huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes  simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri
Huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri

Post hii inahusu zaidi tiba na huduma kwa wenye ugonjwa wa herpes simplex au vipele kwenye midomo na sehemu za siri.

Soma Zaidi...
Athari ya kutotibu maambukizi ya kwenye kibofu cha mkojo
Athari ya kutotibu maambukizi ya kwenye kibofu cha mkojo

Post hii inahusu zaidi athari za kutotibu maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo, nimatazito yanayoweza kutokea iwapo ugonjwa huu hautatibika.

Soma Zaidi...
Hatari ya uzito mkubwa
Hatari ya uzito mkubwa

Posti hii inahusu zaidi hatari zilizopo kwa mtu mwenye uzito mkubwa,kwa sababu ya kuwepo kwa uzito mkubwa na pia unene usio wa kawaida usababisha mtu kuwa na matatizo mbalimbali hasa saratani za kila sehemu kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
Huduma ya kwanza kwa mwenye uchafu kwenye sikio.
Huduma ya kwanza kwa mwenye uchafu kwenye sikio.

Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kqa mgonjwa aliyeingiliwa na kitu au uchafu kwenye sikio.

Soma Zaidi...
Madhara ya kunywa pombe kiafya
Madhara ya kunywa pombe kiafya

Posti hii inahusu zaidi madhara ya kunywa pombe kiafya, ni madhara ambayo utokea kwa watu wanaokumywa pombe kwa kupita kiasi kwa hiyo wanapaswa kupunguza kunywa pombe baada ya kujua madhara yake.

Soma Zaidi...
Faida za seli
Faida za seli

Posti hii inahusu zaidi faida za seli. Seli ni chembechembe hai za mwili ambazo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu.

Soma Zaidi...
Imani potofu kuhusu kifua kikuu
Imani potofu kuhusu kifua kikuu

Posti hii inahusu zaidi imani potofu waliyonayo Watu kuhusu ugonjwa wa kifua kikuu, hizi ni imani ambazo uwepo kwenye jamii na pengine uweza kuaminika lakini si za ukweli.

Soma Zaidi...