Post hii inahusu huduma ya kwanza kwa mtu aliyeingiwa na uchafu au kitu chochote sikioni. Sikio ni mojawapo ya milango ya fahamu ambapo hutumika kusikia, Kuna wakati vitu uingia ndani yake na kuleta madhara
Dalili za mtu aliyeingiza kitu chochote sikioni inawezekana kuwa maharage, mahindi, wadudu na vitu vingine kama hivyo ambavyo hupendelewa na watoto.
Dalili za mtu aliyeingiza kitu sikioni
1. Maumivu makali
2. Maambukizi kwenye sikio
3. Kuvimba ndani ya sikio
4. Sikio kuwa jekundu
5. Kushindwa kusikia vizuri
6. Kutoka uchafu sikioni
Vifuatavyo ni vitu vinavyoweza kuingia sikioni
1. Maharage
2. Mahindi
3. Wadudu
4. Mchanga
5. Toyi
6. Makaratasi madogo madogo
Tufanyeje Ili kuepusha Hali ya kuingia maharage, mahindi na vitu vingine kwenye sikio?
1. Watoto wanapaswa kuwa na mwangalizi wakati wa kucheza
2. Watoto wadichezee vitu kama maharage na mahindi
3. Watoto na watu wazima wawe na tahadhari hasa sehemu zile zenye wadudu kama vile nyuki na wadudu wengine wanaoweza kuingia masikio.
Huduma ya kwanza
1. Usitumie vitu kama msumari, ama kijitu kuchokoa sikio ili kutoa kitu kilichoingia, kufanya hivi kunaweza kuingiza zaidi hicho kitu
2. Kama kitu kinaonekana kitoe kwa upole kwa kukishika, kama kwa kutumia vipanio maalumu vidogovidogo kama tweezers
3. inamisha sikio kwa hali ambayo tundu iliyoingiwa na kitu itaelekea chini
4. kama aliyeingia ni mdudu tumia mafuta yaliyo na uvuguvugu, yaingize sikioni kisha inamisha kichwa kama ulivyofanya hapo juu. Usitumie njia hii kwa kitua ambacho kio mdudu.
5. tumia maji, ingiza sikioni ili hicho kitu kitoke pamoja na maji. Unaweza kutumia bomba la sindano kufanya hivi.
6. mpeleke mmgonjwa kituo cha afya kama kitu kitashindikana kutoka.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Posti hii inahusu zaidi au inapinga Imani potofu ambayo utokea kwenye jamii kwamba unaweza kuambukizwa Ukimwi kwa vitu ambavyo haviusiani na namna mtu anavyoweza kuambukizwa Ukimwi,Ila mapendekezo kuwa watu wanapaswa kujua kuwa huwezi kuambukizwa Ukimwi k
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kupanda
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi za ini, kwa kawaida tunafahamu kwamba ini ni sehemu muhimu kwenye mwili wa binadamu kwa sababu ni.likikosa kufanya kazi yake maisha ya binadamu yanakuwa hatarini kwa sababu mbalimbali.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na kumsaidia mwenye aliyeumwa na nyuki.nyuki na wadudu ambao wakikushambulia Sana na ukikosa msaada unaweza kufa au kuwa katika Hali mbaya.
Soma Zaidi...Unyanyasaji wa kimwili. Unyanyasaji wa watoto kimwili hutokea wakati mtoto amejeruhiwa kimwili kimakusudi. Unyanyasaji wa kijinsia. Unyanyasaji wa watoto kingono ni shughuli yoyote ya kingono na mtoto, kama vile kumpapasa, kushikana mdomo na sehemu
Soma Zaidi...