Kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa.

Posti hii inahusu zaidi sababu za kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa,ni Dalili ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha estrogen kwenye mwili ukilinganisha na homoni ya projestoren.

Kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa.

1. Kama tulivyotangulia kusema kwamba kukosa Ute wakati wa tendo la ndoa ni Dalili ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha estrogen kuliko progesterone ila kuna dalili nyingine ambazo zinaweza kutokea kwa sababu ya kukosa Ute wakati wa kujamiiana ni kama ifuatavyo.

 

2. Kukosa hisia na hamu ya kufanya mapenzi.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo hali ya mtu kukosa hisia kabisa na hamu ya kufanya mapenzi inaisha hali ambayo inasababisha wanafamilia kupata shida kwa sababu ya mmoja wapo kushindwa kutimiza wajibu kwa mwingine, kama ikitokea kwa familia ni kitendo cha kukaa na kuongea ili kuweza kupata suluhisho na kupata matibabu mapema.

 

2. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Kuna wakati mwingine  kunakuwepo na malalamiko wakati wa kufanya tendo la ndoa kwa sababu ya kuwepo kwa maumivu makali yanayosababishwa na michubuko ya maumivu kwa sababu ya msuguano unaosababishwa na uume wakati wa tendo la ndoa, hali hii ikitokea usababisha mmoja kuchukia tendo la ndoa kwa sababu ya kuwepo kwa misuguano wakati wa tendo.

 

3.uwepo kwa damu baada ya tendo la ndoa.

Kwa sababu ya kuwepo kwa misuguano mikali wakati wa tendo la ndoa usababisha kutokwa na damu baada ya tendo hali hii inaweza kuwepo kwa mda wa siku moja au mbili kwa sababu ya kuwepo kwa misuguano.

 

4. Hedhi kukosa mpangilio maalumu.

Kwa sababu ya kukosa Ute ina maana kwamba kuna homoni ambayo inazalisha Ute kupungua hata hivyo na katika sehemu mbalimbali za via vya uzazi usababisha hedhi kukosa mpangilio.

 

5. Kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko mbalimbali kwenye mwili, tatizo hili mara nyingi uwapata wale wanaotumia sana au waliowahi kutumia uzazi wa mpango kwa matumizi ya P2, vitanzi, sindano, vidonge na aina yoyote ya uzazi wa mpango isipokuwa za asili.

 

6. Kwa hiyo hali hiyo ikitokea kwa familia ni vizuri kabisa kutafuta matibabu mapema ili kuweza kuepuka matatizo ya kuchepuka kwenye familia kwa sababu ya mmoja kati ya wana familia hana kabisa hamu ya mapenzi na mwingine anayo.

 Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/12/Tuesday - 03:05:01 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2704


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-