image

Limao (lemon)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula limao

.limao (lemon).

Ni katika matunda yenye uchachu na pia huwa na vitamini c vingi sana. Limau husaidia katika kufanya afya ya moyo kuwa madhubuti kwa kuwa husaidia katuka kupunguza mafuta ndani ya damu na kushusha shinikizo la damu.

 

Pia tafiti nyingine za kisayansi zinaonesha kuwa limau husaidia katika kuzuia ongezeko la uzito mwilini. Pia tafiti nyingine zimeonesha kuwa tunda hiliu husaidia katika kuzuia tatizo la kidney stones yaani mawemawe yanayokaa kwenye figo.

 

6.Embe (mango). Tunda hili ni chanzo kizuri sana cha vitamini c. Pia embe lina kambakamba fiber ambazo zina faida nyingi za kiafya kama tulivyoona hapo juu. Embe pia lina antioxidanta na ant-inflammatory ambazo kwa pamoja husaidia katika kuukinga mwili na maradhi ya kisukari.

 

8.Tikiti (watermelon). Tunda hili pia ni katika matunda yenye vitamin C na A kwa wingi. Tafiti za kisayansi pia zinaonesha kuwa tunda hili lina antioxidant ambazo ni pamoja na lycopene, carotenoid na cucurbitacin E. Hizi husaidia katika kuzuia mwili usipate saratani au kupunguza athari za saratani. Tikiti husaidia katika kupata choo kwa urahisi.

 

Antioxidant zilizopo kwenye tunda hili husaidia kuzuia saratani ya mfumo wa mmengenyo wa chakula na kuota kwa vimbe ambazo ni viashiria vya saratani. Lycopene husaidia katika kuimarisha afya ya moyo kwa kuwa zina uwezo wa kupunguza cholesterol na shinikizo la damu. Katika matunda yote tikiti linajulikana kuwa ndio tunda lenye maji mengi. Lina asilimia 92% ya maji.

 

Ndani ya tikiti kuna virutubisho kama vitamini C, Vitamin A, vitamini B1, B5, na B6. pia kuna madini ya potassium, magnesium. Vitamin C ni antioxidant ambayo husaidia katika kuzuia uharibifu wa seli kutokana na mionzi. Ndni ya tikiti kuna carotenoid hizi ni chembechembe ambazo mwili huweza kuzibadilisha na kuwa Vitamini A. pia chembecheme ziitwazo lycopene hizi ndizo zinazolipa tikiti rangi nyekundu. Chembechembe hizi zinafaida chingi za kiafya mwilini.

 

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa tikiti lina chembechembe ambazo husaidia kuatika kupunguza athari za ugonjwa wa saratani. Mingoni mwa chembechembe hizo ni lycopene. Kitaalamu hizi huitwa anti-cancer. Hizi hupunguza athari za saratani kwa kuwa hupunguza uzalishaji wa IGF (Insulin-like Growth Factor) hii ni aina ya protini ambayo hutumika katika uzalishaji wa seli yaani cell division. Wataalamu wa sayansi wanaeleza kuwa IGF ina mahusiano makubwa na ugonjwa wa saratani. Pia ndani ya tikiti kuna cucurbitacin Eb hii husaidia katika kuzuia uotaji wa uvimbe wa saratani (growth of tumor).

 

Tikiti husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya moyo kama vile kiharusi, shambulio la moyo na presha. Tafiti zinaonesha kuwa lycopene husaidia katika kupunguza kiwango cha cholesterol na kupunguza shinikizo la damu.pia lycopene husaidia katika kupunguza unene wa ukuta wa mishipa ya artery (mishipa mikubwa ya damu). pia tikiti lina citrulline, ambazo ni amino acid hizi husaidia katika kutanua mishipa ya damu hivyo kupunguza presha (yaani shinikizo la damu). pia vitamini na madini mengine tulotaja huko juu ambayo yamo kwenye tunda hili husaidia katika afya ya moyo. Kama vitamini A, B6 na C pia madini ya magnesium na potassium.

 

Tikiti ni tunda safi kwa afya ya ngozi na nywele. Uwepo wa vitamini A na C kwenye tunda hili kunalifanya tunda hili liwe muhimu katika nyanya hizi za ubora wa ngozi na nywele. Vitamin C husaidia mwili wako kutengeneza collagen, hizi ni protini ambazo hizi huweza kufanya ngozi yako iwe laini na rahisi kukunyika na kuzifanya nywele zako ziwe na afya na mathubuti. Pia vitamin A kusaidia katika kutengenezwaji wa seli mwilini hivyo husaidia katika ukuaji wa nywele. Bila ya vitamini A ngozi yako itaonekana kavu na isiyo ya kawaida. Vitamini A na C husaidia katika kuzuia ngozi yako kuungua na jua.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1257


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula Spinachi
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula magimbi
Soma Zaidi...

Faida kula fenesi
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula fenesi Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kungumanga/nutmeg
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kungumanga/nutmeg Soma Zaidi...

utaratibu wa lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

Rangi za matunda
Fida za matunda huanzia kwenye rangi zake, je unajuwa kama rangi ya matunda inaeleza jambo? Soma Zaidi...

Vyakula vyenye vitamini C kwa wingi
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya vyakula vyenye vitamini C kwa wingi Soma Zaidi...

Kazi za protini mwilini ni zipi?
Virutubisho vya protini vina kazi nyingi mwilini. Zifuatazo ndio kazi protini mwilini Soma Zaidi...

Naombakujua kujua Kama huu uyoga unasaidia kansa Kama kwawazee
Mpaka sasa hakuna dawa ya kuponyesha saratani wala kinga ya saratani. Hata hivyo vipo vyakula ambavyo vinakadiriwa kuwa hupunguza hatari ya kuweza kupata saratani. Je unadhani uyoga ni moja ya vyakula hivyo? Soma Zaidi...

Nanasi (pineapple)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kula nanasi Soma Zaidi...

Faida za kula kabichi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kabichi Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula samaki
Posti hii itakwenda kukupa faida za kula samaki kwenye mwili wako. Soma Zaidi...