Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa mapema, kwa sababu ya kuwepo kwa saratani ya matiti, kuna dalili ambazo zikijitokeza zinapaswa kutolewa taarifa mara moja bila kuchelewa kama ifuatavyo.
Mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa mara moja.
1. Kuwepo kwa uvimbe kwenye matiti, kuwepo kwa fundi gumu kama mbegu ndani ya titi au kwapani, hizi ni Dalili za kuripoti mara moja pindi zinapotokea inawezekana kubwa Dalili ya saratani ya matiti au pengine ni ugonjwa wa kawaida unaohitaji tiba mara moja,
2. Pengine matiti yanaweza kuwa na joto la hali ya juu na Dalili za wekundu zinaweza kujitokeza kama si wekundu inaweza kuwa na rangi nyeusi kwenye matiti na kwa wakati mwingine kuna hali ya kubadilika kwa umbo la titi na kuwa kubwa kuliko kawaida au pengine na maumivu yanaongezeka kadri ya ukubwa wa titi linavyoongezeka.
3. Na dalili nyingine ni ngozi kujikunja au kubwa na vitundu na kuifanya iwe na ganda la chungwa kwa dalili hii hakuna maumivu yoyote yanayoweza kujitokeza bali ukilipapasa titi linakuwa gumu na labda Chuchu ndiyo inakuwa inawasha na kutoa maji na pengine hizo Chuchu na sehemu nyingine za titi kubonyea kwa ndani .
4. Dalili nyingine ni pamoja na Chuchu kwa na maumivu makali na pengine kama kutoa maji maji kama hali haikutibiwa inaweza kuleta matatizo makubwa ambayo kuja kuyatibu ni shida kubwa, kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa kama mama ananyonyesha na Dalili hizi zinajitokeza hapaswi kabisa kumnyonyesha mtoto anapaswa kutoa taarifa mara moja na kupata huduma hospitalini.
5. Kwa hiyo tunapaswa kuwa macho na makini kuhusu Dalili hizi hatari kwenye matiti, na tunapaswa kuelimisha jamii kujua wazi kubwa hizi zinaweza kuwa ni Dalili za saratani ya matiti, ila mwenye tatizo la namna hii anapaswa kupima na kujua kubwa ni saratani kweli kwa sababu kuna na magonjwa mengine yenye dalili kama hizi. Kwa hiyo saratani ya matiti ipo na inaweza kutibiwa hasa hasa mgonjwa akiwa mapema hospitalini.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamin C
Soma Zaidi...Vitamini C ni moja kati ya vitamini muhimu sana katika kuboresha ufanyaji kazi wa mfumowa kinga mwilini yaani immune system. Katika post hii utakwenda kujifunza kazi za vitamini C mwilini
Soma Zaidi...Hizi ni aina za vyakula ambavyo husaidia katika kuongeza damu kwa wajawazito na watoto.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madini ya Shaba mwilini,ni madini ambayo ufanya kazi mbalimbali mwilini, kama ifuatavyo
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha kwa ufupi vyakula vya kuviepuka kama una presha ya kupanda.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu upungufu wa vitamini C mwilini
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya majani ya mstafeli dhidi ya bakteria na fangasi, pamoja na kutibu saratani mbalimbali na upambana na fangasi na bakteria kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...