Kama tulivyokwisha kuona kuwa malaria inaweza kuambukizwa kwa kung'atwa na mbu aina ya anophelesi.
Kama tulivyokwisha kuona kuwa malaria inaweza kuambukizwa kwa kung'atwa na mbu aina ya anophelesi. basi tambua kuwa ni mbu jike tu ndiye huweza kuambukiza malaria. basi hapa nitakueleza namna ambavyo malaria huweza kutokea.
kwanza kabisa lazima kuwepo kwa vimelea vya malaria aidha kwa mtu ama kwenye mwili wa mbu jike aina ya anophelesi. vimelea hivi vya malaria vinaanza kuzaliana kwenye mwili wa mbu jike. baada ya siku 10 mpaka 18 vimelea hivi vinakomaa na kuwa kimelea kipya kinachojulikana kama sporozoite. Kisha hivi vimelea vingi vinahamia kwenye tezi za mate za mbu na hatimaye kuingia kwenye mate ya mbu.
Mdomo wa mbu una mirija mikuu miwiliu. Mmoja ni wa kunyonyea damu na mwingine ni wa kutolea mate. Wakati anapong'ata mtu mate yake huingia kwenye mwili wa mtu. Mate haya yakiwa yana vimelea vya malaria (sporozoite) vijidudu hivi huingia kwenye mwili wa mtu. Na hapa hatua nyingine ya vimelea hivi inaanza.
Vimelea hivi (sporozoite) vinapoingia kwenye mwili wa mtu moja kwa moja vinaelekea kwenye ini. na huko huanza kukuwa na kuwa schizonts baadaye hupasuka na kutoa merozoites hivi ni vimelea vipya vilivyokomaa. vimelea hivi kama havitapatiwa dawa ya kuondolewa vitaendelea kwenye mfumo wa damu na kuanza kushambulia seli nyekundu za damu.
Baada ya merozoite kupatikana huelekea kwenye mfumo wa damu na kuanza kushambulia seli hai nyekundu za damu na kuanza kuzaliana humo kwa mara nyingine na kuleta vimelea vipya vitambulikavyo kama schizont na baadaye kupasuka na kutoa vimlea waitwao merozoites.
Na hapa sasa vimelea hawa wapya wanaanza kushambulia seli hai nyekundi na kuzaliana humo kisha seli hupasuka na kuleta vimelea wengi zaidi. Na kuanzia hapa ndipo mgonjwa sasa ataanza kuona dalili za malaria kama homa, maumivu ya kichwa, tumbo, misuli na viungo, kichefuchefu, kutapika na kuharisha.
Kama vimelea hivi havitatibiwa athari zaidi itatokea na kuanza kushambulia maeneo mengine ya mwili kama ini, figo, mapafu na moyo. hapa mgonjwa ataweza kuchanganyikiwa, matatizo ya ini na figo, kupumua kwa shida ama kuhohoa. Kama mgonjwa hatatibiwa athari zaidi inaweza kutokea kama kupoteza fahamu na hatimaye kifo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi maambukizi kwenye uume, maambukizi hata utokea kwenye kichwa Cha uume kwa kitaalamu huitwa Balanitis, zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za maambukizi ya Homa ya inni, Homa ya inni usababishwa na virusi viitwavyo Hepatitis B, huwapata watu wote hasa wale wenye umri chini ya miaka mitano.
Soma Zaidi...Hivi umeshawahikujiuliza kuhusu tezi dume. Wacha nikujuze kitu kimoja, ni kuwa tezi dume huwapata watu kuanziamiaka 40 na kuendelea. Na ifahamike kuwa tezi dume sio busha ama ngiri maji. Pia itambulikekuwa rozi dumehutibika.
Soma Zaidi...Uchovu wa joto ni hali ambayo dalili zake zinaweza kujumuisha kutokwa na jasho kubwa na mapigo ya haraka, ambayo ni matokeo ya joto la mwili wako. Ni mojawapo ya magonjwa matatu yanayohusiana na joto, huku tumbo la joto likiwa kali zaidi na Kihar
Soma Zaidi...Watoto wachanga ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano, watoto hawa hushambulia na maginjwa mara kwa mara na kusababisha ukuaji wao kuwa dunk,
Soma Zaidi...Swali hili limeulizwa na mdau mmoja. Kuwa endapo mtu atafanya ngono zembe na akapata virusi je ataweza kuambukiza.
Soma Zaidi...Psti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Maambukizi ya tezi za mate ambao hujulikana Kama MABUSHA (mumps) ni maambukizi ya virusi ambayo kimsingi huathiri tezi mojawapo ya jozi tatu za tezi za mate zinazotoa mate, zilizo chini na mbele ya masikio
Soma Zaidi...Wajawazito wanaposumbuliwa na ugonjwa wa UTI, dalili za UTI na namna ya Kujikinga na UTI
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi huduma anayopaswa kupata mgonjwa wa ndengue, kwa sababu tunafahamu wazi Ugonjwa huu hauna dawa ila kuna huduma muhimu ambayo anaweza kupata na akaendelea vizuri.
Soma Zaidi...Kisonono ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wa zinaa ambao wanaweza kuwaambukiza wanaume na wanawake. Kisonono mara nyingi huathiri urethra, puru au koo. Kwa wanawake, ugonjwa wa kisonono unaweza pia kuambukiza kizazi.
Soma Zaidi...