Maradhi ya macho, dalili zake na matibabu yake

Maradhi ya macho, dalili zake na matibabu yake

Makala hii itakufundisha maradho makuu ya macho, matibabu yake na tiba zake

Download Post hii hapa

Maradhi ya macho, dalili zake na matibabu yake

MARADHI YA MACHO



Matatizo ya macho yapo mengi katika jamii, lakini mara nyingi matatizo ya macho yanatibika iwapo mgonjwa ataonana na daktari mara atakapoona dalili. Miongoni mwa matatizo ya macho ni kupoteza uwezo wa kuona.



1.Kutoona karibu (long sightedness)
Tatizo hili mara nyingi huwatokea watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea.



Dalili
A.Katika mazingira ya kawaida anaona sawa sawa
B.Kushindwa kusoma herufi ndogo ndogo
C.Kushindwa kufanya kazi za sehemu ndogo ndogo mfano kutunga sindano.



Matibabu: Kutumia miwani ya kusomea.



2.Kutoona Mbali (short sightedness)
A.Hayana umri maalum
B.Myopia – haoni mbali vizuri
C.Hyperopia – haoni mbali na kichwa kinauma akikosa kuvaa miwani yenye namba ndogo kusaidia lense.



NB: Mgonjwa anasoma karibu bila miwani
Matibabu: Kutumia miwani ya kuonea mbali



3.Mtoto wa Jicho (cataract)
Dalili
A.Kidoto cheupe katikati ya kioo cheusi cha jicho (kinafunika mboni ya jicho)
B.Kidoto cheupe kisichobadilika kwa mwangaza
C.Kupunguza nuru ya macho



NB - Mtu anaweza kuzaliwa nacho au kupata ukubwani, inaweza kuwa kwenye jicho moja au yote. Mgonjwa huona mchanganyiko wa rangi anapoangalia mwangaza kama taa za umeme au gari.



Matibabu
Mtoto wa Jicho huwa anatibika kwa upasuaji mdogo na kumuwezesha mgonjwa kuona tena.



4.Presha ya macho (glaucoma)
Tatizo hili husababishwa na kuongezeka presha ya jicho (intraocular pressure) kutokana na kukosekana uwiano wa mzunguko wa majimaji ndani ya jicho (aqueous fluid) kinachotoka kidogo kuliko kinachoingia.



Matokeo
Glaucoma hukandamiza na kuuharibu mshipa wa fahamu ya jicho na kusababisha kupungua kwa nuru na baadae kupoteza nuru ya macho.



Matibabu: Kuonana na daktari kwa ushauri na dawa




5.Macho tongo
Hutokea ama kwa mtu mmoja mmoja, makundi au kwa msimu.



Sababu:
Vimelea ambavyo huzaliwa kwenye sehemu za uchafu Wakati wa msimu huambukiza kwa kukosa elimu ya afya, kwa mfano kutokuosha mikono baada ya kuamkiana na mgonjwa mwenye maradhi haya au kutumia vifaa vya macho kwa zaidi ya mtu mmoja kama vile miwani.



Dalili
A.Kuhisi kama kuna mchanga ndani ya jicho
B.Kuvimba mifuniko ya macho bila kupoteza nuru.
C.Macho kuwa mekundu sana (conjuctivitis)
D.Kutoka tongo kila mara



Matibabu
Mgonjwa atumie dawa alizoandikiwa na daktari tu, kwani dawa za matone za macho ni nyingi na zina kazi tofauti.



6.Matatizo ya sehemu nyeusi ya jicho (cornea)
Kuna matatizo manne makubwa
1. Kovu - kidoto/kibaka cheupe
2. Kidonda - kidoto kijivujivu
3. Kuingiwa na kitu - kemikali,mdudu, vumbi n.k
4. Kutoboka na kutoa maji.
Indhari: hali ya pili mpaka ya nne zikitokea mgonjwa akimbizwe
hospital wakati jicho limefunikwa baada ya huduma ya kwanza



Dalili
KOVU
1.Haina maumivu
2.Jicho haliwi jekundu
3.Jicho halivimbi
4.kupungua nuru jicho



KIDONDA
A.Kinayo maumivu
B.Jicho lililoathirika huwa
C.jekundu
D.Jicho kupunguka nuru
E.Kuuma jicho kwenye
F.mwangaza
G.Kutoka machozi
H.Jicho kuvimba



Kidonda kinaweza kusababishwa na bakteria, fangas, ukosefu wa vitamin A au kwa kuumia mfano; kujichoma na kitu chenye ncha au kitu kigumu, kuingiwa na kitu jichoni, kuungua au kuingia kemikali jichon.



Indhari: Iwapo jicho litaumia lifunike jicho lisipate mwangaza kisha mpeleke mgonjwa hospitali.



7. Kemikali na kuungua
Kama mgonjwa ameingia kemikali kama vile acid, alkali, saruji, chokaa mtie maji ya mchuruziko kwa takriban dakika 15 mfululizo na baadae mpeleke hospitali




8.Macho kuwasha na kutokwa na machozi (conjuctivitis)
Huwakumba zaidi watoto wa umri kati ya miaka 5 -15 ambao hupendelea kucheza sehemu za vumbi au kwenye muangaza mkali (pwani yenye mchanga mweupe sana)



Watu wazima wenye kufanya kazi kwenye viwanda vinavozalisha vumbi, na wenye pumu ya muda mrefu.



Dalili
A.Macho kuwasha (Nuru ya macho haipungui)
B.Macho kubadilika rangi (kahawia)
C.Kutokwa na machozi mengi (sana)
D.Kushindwa kuangalia kwenye muangaza mkali



Matibabu
Kusafisha macho mara kwa mara kwa maji safi.
Kutumia dawa kwa maelekezo ya daktari



9.Kinundu katika mfuniko wa juu au chini wa jicho



DALILI
A.Kinundu kisichouma
B.Mara nyingi hupona wenyewe au unaweza kukikanda kwa maji ya uvuguvugu.
C.Kisipopona au kitakapokuwa kikubwa huhitaji upasuaji mdogo.



10.Uvimbe katika mfuniko wa jicho (cellulitis)



A.uvimbe kwenye mifuniko ya jicho
B.inaweza kuzuwia jicho kucheza (kutembea tembea)
C.mara nyingi hutokea baada ya kusambaa kwa maambukizo
D.ya socket ya jicho kutoka pembezoni kwa saines (sinusitis) za pua
E.husababisha kupoteza nuru za macho



Matibabu: Mpeleke mgonjwa kwa daktari wa masikio, pua na koo (ENT).





                   



Download Post hii hapa

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 5383

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Elimu kuhusu HIV na UKIMWI
Elimu kuhusu HIV na UKIMWI

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu elimu ya kuhusu HIV na UKIMWI

Soma Zaidi...
Dalilili za homa ya manjano
Dalilili za homa ya manjano

posti hii inahusu dalili za Homa ya Manjano ni maambukizi ya virusi yanayoenezwa na aina fulani ya mbu. Maambukizi hayo ni ya kawaida zaidi na kuathiri wasafiri na wakazi wa maeneo hayo.

Soma Zaidi...
   Fahamu Ugonjwa wa kipindupindu.
Fahamu Ugonjwa wa kipindupindu.

Kipindupindu ni ugonjwa wa bakteria ambao kawaida huenezwa kupitia maji machafu. Kipindupindu husababisha Kuhara na Upungufu wa maji mwilini.

Soma Zaidi...
Dalili za coma
Dalili za coma

Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la kichwa , Kiharusi, Tumor ya ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi, kama vile Kisukari au maambukizi.

Soma Zaidi...
Je vidonda Mara nyingi vitakuwa maeneo gan ya mwili?
Je vidonda Mara nyingi vitakuwa maeneo gan ya mwili?

Je vidonda Mara nyingi vitakuwa maeneo gan ya mwili? Hili ni swali lililoulizwa kuhusu vidonda vya tumbo, kuwa vinakaa wapi katika mwili.

Soma Zaidi...
Dalili za miguu kufa ganzi
Dalili za miguu kufa ganzi

Posti hii inahusu zaidi dalili mbalimbali ambazo Uweza kujitokeza na kuona kwamba ni Dalili za miguu kufa ganzi, pengine utokea kwa watu wote na pengine huwa ni kwa ghafla

Soma Zaidi...
Sababu za maumivu ya tumbo
Sababu za maumivu ya tumbo

hapa utajifunza maradhi mbalimbali yanatopelekea kuwepo kwa maumivu ya tumbo

Soma Zaidi...
ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO: maumivu ya tumbo, kichwa, kutapika damu, kichefuchefu, miwasho
ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO: maumivu ya tumbo, kichwa, kutapika damu, kichefuchefu, miwasho

ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO Kukaa na minyoo na kutoitibu kwa muda mrefu kunaweza kusababisha madhara mengi hususani kwenye ini na maeneo mengine ya mfumo wa kumeng’enya chakula.

Soma Zaidi...
Je utaweza kuambukiza HIV ukiwa unatumia PrEP?
Je utaweza kuambukiza HIV ukiwa unatumia PrEP?

Swali hili limeulizwa na mdau mmoja. Kuwa endapo mtu atafanya ngono zembe na akapata virusi je ataweza kuambukiza.

Soma Zaidi...