Faida za kula Pilipili
Usiogope kuwashwa, kula pilipili ni nzuri kwa afya yako ia virutubisho vingi sana
14.Pilipili kali. Watu wengi wamekuwa wakiacha kutumia pilipili etu kwa sababu ya ukali wake. Ila itambulike kuwa ijapokuwa ni kali lakini ila faida nyingi sana kwa afya ya mtu. Pilipili pia ina vitamini c ndani yake kwa kiasi. Vitamini hivi ni muhimu sana katika mfumo mzima wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na wadudu shambulizi.
Pilipili zote zina vitamin A, C na K lakini pilipili nyekundu zimezidi wenzie. Wataalamu wa afya wanazungumza kuwa antioxidant, vitamin A na C vilivyomo kwenye pilipili husaidia katika kuzuia maradhi ya saratani na baadhi ya maradhi yanayohusiana na kuzeheka, na pia husaidia katka kuboresha mfumo wa kinga. Pia vitamin K husaidia katika kuganda kwa damu, kuimarisha mifupa pia husaidia katika kulinda seli.
Pilipili nyekundu ni chanzo kizuri cha carotenoid ambayo hutambulika kama lycopene, hii ni mujarabu sana katika kuzuia mwili kupata maradhi ya saratani ya kibofu, njia ya uzazi kwa kinamama na saratani ya kongosho.pia kuna carotenoid inayotambulika kama cryptoxanthin hii nayo hujulikana kwa uwezo wake wa kupambana na kuzuia mwili kupata saratani ya mapafu inayohusiana na uvutaji wa sigara.
Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa pilipili husaidia katika kurekebisha mapigo ya moyo na kuongeza joto la mwili kwa muda wa dakika 20 baada ya kuila. Hii inaonesha kuwa mwili utakuwa na uwezo wa kuunguza mafuta na cholesteral za ziada kwa muda huo. Pia tafiti nyingine zinaonesha kuwa pilipili husaidia katka kupunguza athari za vidonda vya tumbo kwani husaidia katika kuuwa bakteria ndani ya tumbo.
Ndani ya pilipili kuna antioxidant iitwayo piperine. Wataalamu wa afya wanadai kuwa ulaji wa antioxidant husaidia katika kuimarisha afya ya mtu. Piperine inatambulika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti na kulinda uharibifu wa seli. Pia ulaji wa pilipili husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo.
Kwa ufupi pilipili husaidia sana kwa afya ya mlaji. Pia pilipili husaidia katika kuulinda mwili dhidi ya maradhi ya kisukari, saratani na maradhi ya moyo. Afya ya ubongo, kuimarisha mapigo ya moyo pamoja na kupunguza mgando wa mafuta kwenye mirija ya damu. Pilipili husaidia katika kuufanya mwili uweze kunyonya virutubisho muhimu kutoka kwenye chakula.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitau cha Fiqh π2 kitabu cha Simulizi π3 Simulizi za Hadithi Audio π4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π5 Kitabu cha Afya π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Vyakula bora kwa ajili ya afya ya macho.
βMacho ni moja ya viungo muhimu zaidi vinavyokuunganisha na ulimwengu, lakini mara nyingi tunayasahau hadi pale tunapoanza kupata changamoto za kuona. Kama ilivyo viungo vingine, macho yanahitaji virutubisho maalum ili yasibadilike ubora kadiri umri unavyosonga mbele. Makala haya yanakupa orodha ya vyakula bora unayoweza kuingiza kwenye sahani yako leo ili kuimarisha uwezo wako wa kuona
Soma Zaidi...Faida za kiafya za kula njegere, kunde, mbaazi, njugu mawe na maharage
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula njegere, kunde, mbaazi, njugu mawe na maharage
Soma Zaidi...Fahamu virutubisho vya wanga na kazi zake, vyakula vya wanga na athari za upungufu wake
Hapa tutaona kuhusu virutubisho vya wanga, kazi zake na athari za upungufu wake
Soma Zaidi...Faida za chungwa na chenza ( tangarine)
Somo hili litakwenda kukueleza kuhusu faida za chungwa na chenza mwilini
Soma Zaidi...