Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuangalia kama mtoto anapumua pindi anapozaliwa,tunajua kabisa ili kujua na kuelewa kama mtoto yuko hai ni lazima kuangalia upumuaji wa mtoto,ambapo tunaitambua pale anapolia tu.
1. Kwanza kabisa wakati tunapokuwa tunapangusa mtoto tunapaswa kuangalia upumuaji wake kwa kuangalia Dalili zote za upumuaji.
2.Vile vile Tunapaswa kusikiliza sauti inayotoka wakati wa kupumua na kuangalia jinsi kifua kinavyocheza cheza kwa kutumia sauti tunaweza kugundua kuwa mtoto yuko hai na anaweza.
3.Vili vile tunapaswa kuangalia kama mtoto anapumua haraka haraka na kwa urahisi au kuangalia kama mtoto analia kwa sababu kulia ni Dalili mojawapo ya kupumua kwa mtoto.
4. Na pia mtoto anapaswa kuonekana anapitisha hewa kwenye pua kwa urahisi sio kwa shida, ukiona anapitisha hewa kwa shida hiyo ni Dalili kwamba kuna Tatizo ambalo halijaenda sawa na pia ni lazima kumshughulikia mtoto.
5. Kwa kawaida mtoto anayepumua vizuri ni yule ambaye analia tu baada ya kuzaliwa, anapumua vizuri na kwa haraka haraka na upumuaji wake ni wa kawaida hakoromi au hakuna kitu chochote kinacholeta shida wakati wa upumuaji.
6. Na mtoto ambaye hapumui vizuri ni yule ambaye anahangaika wakati wa kupumua na anapumua kwa kutumia hewa nzito na pumzi haieleweki au kwa wakati mwingine hakuna kupumua kabisa, hali ya namna hii ikitokea huduma inapaswa kutolewa haraka.
7. Kwa wakati mwingine kuna watoto ambao wanazaliwa na hewa yao inakuwa ya shida na kwa wakati mwingine wanazaliwa wakiwa hawapumui kabisa kwa hiyo tunapaswa kuwasaidia kwa kufungua sahemu muhimu kama vile kwenye mdomo, kwenye pua au kifuani labda kuna baadhi ya vitu ambavyo vimefunga hewa isiweze kupita.
8. Pamoja na upumuaji wa shida kwa watoto kuna baadhi ya watoto wanaozaliwa wakiwa na uzito mkubwa na wanahitaji uangalizi wa karibu ili waweze kupata huduma kwa sababu walicheleweshwa wanaweza kupata matatizo mbalimbali.
9. Kwa hiyo baada ya kugundua kubwa mtoto anapumua vizuri na hana tatizo lolote ni lazima kumpeleka kifuani mwa Mama ili aendelee kuishi hapo kwa ajili ya kupata joto la Mama na kwa wale ambao hawapumui ni vizuri kabisa kuwahi kuwapeleka kwenye vituo vya afya kwa ajili ya uangalizi zaidi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuhusu kwa mimba kutoka kabla ya mda wake,ni kitendo ambacho mimba utoka kabla ya wiki ishilini na na nane.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo anyopaswa kujua akiwa mjamzito. Ni mambo muhimu ya kuzingatia kwa mama akiwa mjamzito.
Soma Zaidi...Kondo la nyuma ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamziti,kondo la nyuma husaidia katika kazi mbalimbali katika ukuaji wa mtoto.
Soma Zaidi...Kufanya tendo la ndoa wakati wa ujauzito kina faida nyingi kwa mama na mtoto. Miongni mwa faida hizo ni kuimarisha mfumo wa kinga wa mama, kumuondolea stress na ukuajinmzuri wa mimba
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupima mimba kwa kutumia chumvi sukari na sabuni
Soma Zaidi...Unataka kujuwa sababu za mjamzito kutokwa na damu, utelezi ama majimaji kwenye uke wake. Na dalili gani zinaashiriwa na majimaji haya
Soma Zaidi...Hivi unadhani kuharisha ni katika dalili za mimba, vipi kuhusu kutopata choo pia inaweza kuwa ni ujauzito?
Soma Zaidi...Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii
Soma Zaidi...