image

NI ZIPI KAZI ZA PROTINI MWILINI?

Makala hii inakwenda kukuletea kazi kuu za protini na vyakula vya protini katika miili yetu. Mkala hii itakusaiidia kujuwa namna ya kupangilia lishe yako kiusalama zaidi baada ya kujuwa kazi za protini katika miili yetu.

KAZI ZAPROTINI NA VYAKULA VYA PROTINI MWILINI

Kwa kuwa sasa tunajua vyanzo vya protini sana ni vyemna tukaziona kazi za protini ndani ya miili yetu. Waandishi wengi wamekuwa wakiandika kazi za protini, na kuziorodhesha katika kazinyingi. Lakini katika makala hii itakuletea kazi zilizo kuu za protini. Kazi za protini mwilini:- Kujenga mwili; Kupona kwa vidonda na majeraha Kutengeneza antibody (kinga za mwili) Kutengeneza hemoglobin (chembechembe zaseli nyekundu za damu) Kutengeneza enzymes zinatumika katika kumeng;enya chakula Kutengeneza homoni Kuthibiti kichakati na shughuli za ndani ya seli Huhusika katika kutengeneza tishu (nyama na misuli) ndani ya mwili Nywele, kope, nyusi, vinyweleo na kucha hutokana na rotini  

 

1. Kujenga mwili; protini huhusika katika kujenga mwili, na uponaji wa vidonda na majeraha. Mwili kukua vyema na kujengenka vyema protini inahitajika katika kuhakikisha hili linafanyika. Ulaji wa protini ya kutosheleza uanaweza kuufanya mwili uwe katika umbo jema na lililojengeka vyema. Endapo mwili utapata majeraha protini itahusika katika kuziba majeraha na vidonda katika eneo husika. Kama wanavyosema mwili haujengwi kwa matofali, lakini unaweza kusema kuwa protini ndio tofali la kuujenga mwili.  

 

2. Hutumika katika kutengeneza antibodies; hizi ni chembechembe za protini zinazopatikana kwenye damu. Chembechembe hini ni muhiu sana katika mfumo wa kinga. Hizi huweza kuulinda mwili dhidi ya mashambulizi ya maradhi na watutu waletao maradhi. Protini inahitajika ili kutengenezwa kwa chembechembe hizi kufanyike. Hivyo unaweza kusema kuwa protini ni muhumu katika mfumo wa kinga mwilini.  

 

3.Utengenezwaji wa hemoglobin; hemoglobin ni aina za protini, na hii huhusika katika usafirishaji wa hewa ya oksijen na kabondioxide ndani ya miili yetu. Hemoglobin ni chembechembe ambazo ninakazi ya kuchukuwa hewa ya okijeni baada ya mtu kuivuta na kuipeleka kwenye moyp ambapo husambazwa, kwenda maeneo mengine. Kisha hemoglobinhukusanya hewa chafu nyenye kabondaiyokasaidi na kuipeleka kwenye mapafu. Ijapokuwa hemoglobin ni chembehembe za protini lakini pia imetokana na madini ya chuma. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kuathiri mfumo wa damu.  

 

4. Utangenezwaji wa enzymes. Hizi ni chembechembe zinazotambulika kama biological catalyst, yaani ni vichochezi vya kuchochoea michakato ya kikemikali iendelee kufanyika ndani ya miili etu. Enzymes huchukuwa nafasi kubwa katika kumenge’enya chakula katika hutau zote na katika maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Enzmes zinaweza kupatikana mdomoni, tumboni na katika utumbo mdogo. Umeng’enywaji wa chakula ili tupate vurutubisho enzymes hutumika.  

 

5. Utengenezwaji wa homoni; ili mwili uweze kutengeneza homoni unahitaji protini. Homoni ni chembechembe za kikemikali ambazo husaidia katika kufanya kazi nyingi na tata mwilini. Utengenezwaji wa mayai kwa wanawake na mbegu za uzazi kwa wanaume unahitaji homon. Urekebishwaji wa sukari pia unahitaji homoni. Ilijasho liweze kutoka homoni huhusika katika kurekebisha joto mwilini. Homoni zinakazi nyingi sana mwilini. Lakini jambo la msingi kufahamu hapa ni kuwa homoni hutengenezwa kwa protini.  

 

6. Utengenezwaji wa nywele na vinyweleo na kope pia hutokana na protini. Kama nilivyotangulia kukueleza kuwa protini ni matofali ya kuijenga miili yetu na hii ndio maana yake. Hata nywele zetu kama hatutapata protini ya kutosha katu huwezi kuna na nywele nzuru, na zenye afya ya kutosheleza. Nywele zinaweza kuwa katika hali isiyo ya kawiada ka hutapata protini ya kutosha.  





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1521


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Vyakula na vinywaji hatari na vilivyo salama kwa mgonjwa wa kisukari
Hapa utajifunza vyakula hatari kwa mgonjwa wa kisukari, pia utajifunza vyakula salama anavyotakiwa ale mgonjwa wa kisukari, Pia ujajifunza njia za kujikinga na kisukari Soma Zaidi...

Fahamu vyakula vya nyuzinyuzi
Posti hii moja kwa moja inaenda kuelezea vyakula vya nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye matunda na mboga mboga. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Tangawizi
Soma Zaidi...

Faida za kula Ndizi
Kuna faida kubwa za kiafya kwa kula ndizi, soma makala hii mpaka mwisho Soma Zaidi...

Faida za apple kwa Mama mjamzito
Posti hii inahusu zaidi faida za apple kwa mama mjamzito, ni faida anazozipata mama akiwa mjamzito kwa sababu ya kuwepo kwa vitamini mbalimbali kwenye apple ambavyo usaidia katika makuzi ya mtoto.I Soma Zaidi...

Umuhimu wa kutumia maharage kwa wingi
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia maharage kwa wingi, maharage ni aina ya chakula ambacho upatikanaji wake ni rahisi na watu wengi hawajui kwa ulaji wa maharage una faida kubwa sana mwilini kwa hiyo tunapaswa kuangalia faida za maharage kama ifua Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Epo ama tufaha
Soma Zaidi...

KITABU HA MATUNDA
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

Kazi za madini ya zinki
Posti hii inahusu zaidi juu ya madini ya zinki na faida zake katika mwili wa binadamu, Soma Zaidi...

Fahamu vitamini C na kazi zake, vyakula vya vitamini C na athari za upungufu wake.
kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu. Soma Zaidi...

Vyakula na ugonjwa wa kisukari
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya vyakula vimpasavyo mgonjwa wa kisukari Soma Zaidi...

Je ,mafua yanayojirudia Mara kwa Mara hasa wkati was baridi ,au vumbi likiingia puan chafya haziishi,Hilo nalo ni upungufu wa vitamin c?
Soma Zaidi...