Yale waumini wanayowajibika kujiepusha nayo kwa mnasaba wa aya tulizozipitia (17:23-40) ni haya yafuatayo:
(a) Kujiepusha na kumshirikisha Allah (s.w)
Kumshirikisha Allah (s.w) ni kujaalia kuwa Allah (s.w) anao washirika wake wanaomsaidia katika kuendesha masuala mbali mbali katika mchakato mzima wa maisha ya dunia. Allah (s.w) hushirkishwa kinadharia na kiutendaji.
Allah (s.w) hushikirishwa kinadharia kwa kujaalia kiumbe kisicho na uwezo wowote, kama vile sanamu, jiwe kubwa, mti mkubwa, majini, malaika, n.k.; kuwa ni mungu na kukielekea kwa maombi na kukitegemea kama apasavyo kuombwa na kutegemewa Allah (s.w). Hii ni shiriki katika Dhati ya Allah (s.w). Pia Allah (s.w) hushirikishwa kinadharia, kwa kumnasibisha na kiumbe au kukipachika kiumbe sifa anazostahiki kusifiwa kwazo. Hii ni shiriki katika sifa za Allah (s.w).
Allah (s.w) hushirikishwa kiutendaji kwa kutiiwa kanuni na sharia na kufuatwa miongozo ya maisha iliyotungwa na watu kinyume na mwongozo wa maisha wa Allah (s.w) kupitia kwa Mitume wake na Vitabu vyake. Kumtii yeyote kinyume na kanuni na sharia za Allah (s.w) ni kumshirikisha Allah (s.w) katika Mamlaka yake. Na kupitisha hukumu yoyote kinyume na alivyohukumu Allah (s.w) ni kumshirikisha katika Hukumu zake. Shirk ndio kiini na chanzo kikuu cha maovu yote duniani na ndio msingi mkuu wa dhuluma (rejea Qur-an 31:13)
Umeionaje Makala hii.. ?
Kwa hakika binaadamu ameumbwa, hali ya kuwa mwenye pap atiko.
Soma Zaidi..."Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu
Soma Zaidi...Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu.
Soma Zaidi...عَنْ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَيْضًا قَالَ: " بَيْنَمَا نَحْنُ جُلُوسٌ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم ذَاتَ يَوْمٍ، إذْ ?...
Soma Zaidi...Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu.
Soma Zaidi...Ni lipi lengo kuu la Elimu katika uislamu (Edk form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...