Kujiepusha na ubadhirifu (israfu) na ubakhili
Kujiepusha na ubadhirifu (israfu) na ubakhili
(b)Kujiepusha na Ubadhirifu (israfu)
Ubadhirifu ni utumiaji wa mali au kitu chochote kile chenye thamani kama vile muda, zaidi kuliko mahitajio. Pia kutoa mali au huduma na kuwapa watu wasiostahiki ni katika kufanya ubadhirifu. Vile vile kutumia mali au muda katika yale yaliyoharamishwa, ni katika israfu. Ubadhirifu wa aina zote umekatazwa katika Uislamu na afanyae ubadhirifu ni rafiki yake shetani.
(c)Kujiepusha na ubakhili
Ubakhili ni kinyume cha ubadhirifu.Ubakhili ni kitendo cha kuwanyima msaada wale wanaostahiki wakati uwezo wa kuwasaidia upo. Pia ni katika kufanya ubakhili kwa mtu kujinyima mahitaji muhimu ya maisha kama vile lishe bora, mavazi na makazi bora na huku anauwezo. Katika kutumia na kutoa misaada, Waumini wanatakiwa wawe kati na kati:
"Wala usifanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue ovyo ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa na kufilisika ”(17:29)
"Na (katika waja wa Rahman ni) wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa kati kati baina ya hayo." (25:67)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Muhtasari wa madili malezi ya jamii kama ilivyobainishwa katika Qur-an
(v)Kuwaombea dua wazazi.
Soma Zaidi...Uovu wa kumzulia Muumini Uzinifu na Maovu mengine na Hukumu dhidi ya Wazuaji
Kumzulia mtu mtwahirifu kuwa amefanya tendo la zinaa pasina kuleta ushahidi stahiki ni tendo ovu mno mbele ya Allah (s.
Soma Zaidi...Dhana ya ibada kwa mtazamo wa uislamu..
Mtazamo wa uislamu juu ya ibada (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu (EDK form 1: mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Soma Zaidi...